Serikali ingetumia mfumo huu kukomesha ukosefu wa ajira nchini

karv aveki

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
219
500
Kwa siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la ukosefu wa ajira nchini unalotokana na
1)mfumo mbovu wa elimu uliopo
2)Uchu na uroho wa madaraka
3)Undugu ukabila na ukanda
4) Rushwa

Kutokana na visababishi hivyo nilikuwa na mapendekezo yafuataya japo

KWA SERIKALI & MASHIRIKA BINAFSI
1)Kuwepo na database katika vyuo vyote nchini ambapo sekta binafsi na serikali wafate waajiriwa vyuoni ili kuepusha baadhi ya visababishi hapo juu hasa cha 3 na 4
2)Katika kuajiri kwa kuwa wahitimu wengi huwa wanaenda kwenye mafunzo kwa vitendo suala la uzoefu eti miaka kumi au ishirini liondolewe
3)Watu kuacha kujilimbikizia vyeo na kukaimu nafasi za watu badala yake mtu mmoja cheo kimoja haileti maana mtu huyo huyo anakitengo hiki halafu anapewa kingine asimamie wakati angeweza kupatikana mtu akafanya kazi vizuri tu
4)Kutoruhusu wazee kuongeza umri wa kustaafu kwa kisingizio chochote kile maana kuna baadhi wa wazee hadi miaka 70 mtu bado anakula pesa ya serikali huku vijana wanaumia
5)Kubadili mitaala ya elimu itakayo endana na hali ya maisha ya sasa
6)Kupunguza tozo na riba katika mikopo ya vijana ili wengi wao waweze kujiajiri na kupunguza hatua za ufuatiliaji na upatikanaji wa vibali mbali mbali

KWA MZAZI NA MUHUSIKA
1)Acha kusoma kitu kwa kufuata mkumbo kisa rafiki yako anasomea kitu fulani na wewe hiko hiko maana wengine washaandaliwa mazingira tayari
2)Mzazi usimlazimishe mtoto kusomea kitu fulani eti kisa tu mtoto wa fulani alisomea kitu kama hicho na ameajiriwa jua nyakati zinabadilika
3)Wazazi punguzeni kuwaomba watoto hela zao za boom kwani wanaweza kuzitunza na kufanyia mtaji baadae
4)Vijana punguzeni kubeti ulevi na uzinzi hasa mkiwa vyuoni kwani kufanya ivyo mnapunguza uaminifu badala yake iyo pesa iwekeze kufungua hata electroniki money transfer ili baadae ije kukusaidia
5)Angalia uelekeo wa maisha ya sasa kabla hujaamua kusomea kitu fulani


KAMA NA WEWE UNA MAPENDEKEZO YAKO ONGEZA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom