Serikali imeshindwa kuwatibu wasomi wake -

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Nilikuwa napitia kwenye website ya UDSM na nimejikuta nakumbana na butwaa kubwa pale nilipokutana na tangazo la watawala kuwa wanafunzi wote wanapaswa kujilipia sh.laki moja kila mwaka kwa ajili ya matibabu, huku wakiwa bado wengine wanalipiwa 20%ya ada tuu.

Huu kwangu ni uonevu wa hali ya juu kama serikali inashindwa kuwatibu wasomi wake inafanya kazi gani basi?

Kwani wanaofanya haya maamuzi waliwahi kudaiwa kulipia fedha za matibabu?

Kwa nini wasiamue kuwa zile zilizoibiwa kule BOT/EPA zirudishwe ili kulipia matibabu ya wanafunzi?

Kwa nini iwe ni lazima mwanafunzi kutibiwa chuoni?kwa nini isiwe kuwa kila mwanafunzi aende akajitibie nje ama ndani ya chuo huku akilipia gharama za matibabu kwani huu mpango wa kulipia laki kila mwanafunzi ni mradi wa wajanja pale mlimani.

Kuna haja ya kila mwanafunzi kukataa uonevu huu wa kusikitisha ama ni kwa vile nyerere amekufa ndio maana ?

Wanafunzi na haswas wa pale mlimani sharti waache kuvalishwa t/shirts za kijanaina kuimba nambari one namabri one kwani wanaonekana kama mandondocha.Tembelea www.udsm.ac.tz
 
Hiyo 100,000 ni kama Insurance! Ukimwambia mwanafunzi anatoka Ngara aweke akiba na akiugua ndo ajitibu ni ngumu! Nakumbuka rafiki yangu aliugua kweli in 1990s na kulazwa Health Center UD 3 months -sasa kama ni yeye kujilipia ingekuwa ngumu!

Kama hii pesa inaliwa- sijui ni another issue!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom