Serikali imenitapali zaidi ya milioni 10

Harald Dad

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2016
Posts
353
Reaction score
263
Watanzania wenzangu naombeni ushauri wenu, hapa nilipo nimevurugwa vibaya sana kwa sasa kila ninalojaribu kufanya kwangu naliona kama halina tija tena kwangu.

Hali hii imenijia baada ya kugundua kuwa serikali ya Tz ilinilaghai na kisha kunitapeli zaidi ya sh.milioni 10. Mara nyingi nawaza na kujiuliza hivi hawa akina Karl Peter na sisi akina Chief Mangungo wa Msovero bado tupo dunia ya sasa? Kwa nini mikataba hewa kama ile ile ya kikoloni bado ipo?

Au wakoloni wamekuja tena na mambo yao yale yale? Nahisi wakoloni ni wale wale ila tu wamebadilika tu rangi walikuja weupe wa sasa ni weusi. Wanatuaminisha karatasi nyeupe tuiite nyeusi na nyeusi tuiite nyeupe. May mosi nilikuwa hapa Mbeya jambo la kushangaza mc wao Mavunde kabla ya mkuu kufika alisisitiza sana akija tu tujitahidi kuonyesha nyuso za furaha na tumshangilie kwa furaha. Nilijiuliza sana ya nn kujifanyisha kuwa nina furaha usoni wakati moyoni ninalia? Kwa nn niishangilie serikali hii wakati wao mimi wamenitapeli. Serikali iliyochukua zaidi ya 10 milioni huku mm wakinitunuku karatasi?

Wamechukua hela yangu na mm wamenipa karatasi ety wenyewe wakaliita degree huu ni utapeli kama ilivyovyo utapali mwingine. Mungu anawaona wakuu.

2020 is around the corner.
 
Pole sana .Anza kulima matikitiki ya mvua huko mbeya
 
Umeandika maneno mengi lakini dhamira au wazo kuu LA andiko lako halieleweki. Hujaeleza umetapeliwa namna gani hizo milioni kumi. Uliahidiwa kulipwa baada ya kushangilia au ulitajwa kama mfanyakazi bora alaf hukukabidhiwa zawadi husika?. Umetumia nguvu nyingi kuandika na umetupatia kazi ya kusoma andiko lakimi hujakidhi haja ya wasomaji. Wakati mwingine, unapoandika kwaajili ya umma na hasa unapoituhumu mamlaka za nchini, ongeza umakini.
Watanzania wenzangu naombeni ushauri wenu, hapa nilipo nimevurugwa vibaya sana kwa sasa kila ninalojaribu kufanya kwangu naliona kama halina tija tena kwangu. Hali hii imenijia baada ya kugundua kuwa serikali ya Tz ilinilaghai na kisha kunitapeli zaidi ya sh.milioni 10. Mara nyingi nawaza na kujiuliza hivi hawa akina Karl Peter na sisi akina Chief Mangungo wa Msovero bado tupo dunia ya sasa? Kwa nini mikataba hewa kama ile ile ya kikoloni bado ipo? Au wakoloni wamekuja tena na mambo yao yale yale? Nahisi wakoloni ni wale wale ila tu wamebadilika tu rangi walikuja weupe wa sasa ni weusi. Wanatuaminisha karatasi nyeupe tuiite nyeusi na nyeusi tuiite nyeupe. May mosi nilikuwa hapa Mbeya jambo la kushangaza mc wao Mavunde kabla ya mkuu kufika alisisitiza sana akija tu tujitahidi kuonyesha nyuso za furaha na tumshangilie kwa furaha. Nilijiuliza sana ya nn kujifanyisha kuwa nina furaha usoni wakati moyoni ninalia? Kwa nn niishangilie serikali hii wakati wao mimi wamenitapeli. Serikali iliyochukua zaidi ya 10 milioni huku mm wakinitunuku karatasi? Wamechukua hela yangu na mm wamenipa karatasi ety wenyewe wakaliita degree huu ni utapeli kama ilivyovyo utapali mwingine. Mungu anawaona wakuu.2020 is around the corner.
 
mbona ameeleweka aya ya mwisho. alisoma hadi kutunukiwa cheti/degree kwa gharama ya 10m lakini haoni faida yake (hana ajira).

reply ya kwanza aliyejibu matikiti amemuelewa
Umeandika maneno mengi lakini dhamira au wazo kuu LA andiko lako halieleweki. Hujaeleza umetapeliwa namna gani hizo milioni kumi. Uliahidiwa kulipwa baada ya kushangilia au ulitajwa kama mfanyakazi bora alaf hukukabidhiwa zawadi husika?. Umetumia nguvu nyingi kuandika na umetupatia kazi ya kusoma andiko lakimi hujakidhi haja ya wasomaji. Wakati mwingine, unapoandika kwaajili ya umma na hasa unapoituhumu mamlaka za nchini, ongeza umakini.
 
Ndio nyie mliambiwa kuwa akiwaangalia nyuso zenu ni kama za watumishi wa Mungu..kumbe moyoni mlikuwa na yenu
 
Na ndomana kila ck huwa nasema kwa elimu tz usijiwekeze sana kwenye elimu yaan elimu ya tz na mfumo wake unamtengeneza mwanafunzi kuajiriwa na sio kujiajiri,karibuni kwenye ulimwengu wa biashara yaan raha teleee
 
Duu we jamaa kichwan ngumu umeshindwa kuelewa fumbo Dogo km hilo kweli duuu
Umeandika maneno mengi lakini dhamira au wazo kuu LA andiko lako halieleweki. Hujaeleza umetapeliwa namna gani hizo milioni kumi. Uliahidiwa kulipwa baada ya kushangilia au ulitajwa kama mfanyakazi bora alaf hukukabidhiwa zawadi husika?. Umetumia nguvu nyingi kuandika na umetupatia kazi ya kusoma andiko lakimi hujakidhi haja ya wasomaji. Wakati mwingine, unapoandika kwaajili ya umma na hasa unapoituhumu mamlaka za nchini, ongeza umakini.
 
mbona ameeleweka aya ya mwisho. alisoma hadi kutunukiwa cheti/degree kwa gharama ya 10m lakini haoni faida yake (hana ajira).

reply ya kwanza aliyejibu matikiti amemuelewa
Bora wewe umekuwa msomi mwenzangu hawa wenzetu walioishia la saba hawawezi kuona kitu maana wao walizoea mambo ya "spoon feeding" so siwezi kuwalaumu maana ndio ukomo wao wa fikra.
 
Na ndomana kila ck huwa nasema kwa elimu tz usijiwekeze sana kwenye elimu yaan elimu ya tz na mfumo wake unamtengeneza mwanafunzi kuajiriwa na sio kujiajiri,karibuni kwenye ulimwengu wa biashara yaan raha teleee
Asante sana mkuu binafsi nimekuelewa sana
 
Umeandika maneno mengi lakini dhamira au wazo kuu LA andiko lako halieleweki. Hujaeleza umetapeliwa namna gani hizo milioni kumi. Uliahidiwa kulipwa baada ya kushangilia au ulitajwa kama mfanyakazi bora alaf hukukabidhiwa zawadi husika?. Umetumia nguvu nyingi kuandika na umetupatia kazi ya kusoma andiko lakimi hujakidhi haja ya wasomaji. Wakati mwingine, unapoandika kwaajili ya umma na hasa unapoituhumu mamlaka za nchini, ongeza umakini.
Huwezi elewa kwa kuwa ndio ukomo wako wa kufikiri umekomea hapo
 
Back
Top Bottom