IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Hili nalo litapita, sijui tumlaumu JK ama wale waliomtangulia kwa kufisadi fedha za watz
Hili nalo litapita...
Hapana Mkuu, halitapita isipokuwa tutalipitisha
Katika Hali iliyokuwa inatarajiwa kabisa, serikali ya Mheshimiwa Kikwete haina pesa kwa sasa za kulipa mishahara ya wafanyakazi wake na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kwa habari za uhakika wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wameandikiwa barua kuambiwa hakuna mishahara mpaka pale serikali itakapotuma pesa. Mwanzoni tuliambiwa hapa JF kulikuwa na uwezekano wa kuwalipa tarehe 5/9.2008 lakini sasa ni mpaka serikali itakapotuma pesa.
Kama hilo halitoshi vyuo vyote vya serikali ambavyo vilikuwa vifunguliwe mwishoni mwa mwezi wa 8 hafitafunguliwa mpaka tarehe 29/9/2008. Tayari wanafunzi wote wameshataarifiwa kuhusu kuahirishwa huku. Hii ni kutokana na bodi ya mikopo kutopatiwa fungu lake la mikopo mpaka sasa hivi.
Hivi hili la kusema pesa zote za EPA (karibia billioni 200) ziingizwe serikalini sio katika kujaribu kuficha kwamba serikali haina pesa kwa sasa?
Jamani suala la mishahara kwenye secta binapsi wangewaachia waajiri wenyewe waamue. Haiwezekani serikali itoe tamko mwalimu wa shule binafsi alipwe 350,000 wkt wa serikalini analipwa 150,000/=.
Pili house girl akilipwa sh 65,000/= je wewe unayemlipa huyu binti shi 65,000 wewe unalipwa shilling ngapi?????.
Sio Serikali inakurupuka tu kuamua mambo ianze yenyewe kwenye secta zake kupandisha mishahara ndio na secta binafsi zifate.
Kwa mtaji huu ajira nyingi sana zitapungu na lile swala la Mh. Rais kuongeza ajira 1,000,000 jalitawezekana na matokeo yake zitapungua ajira 900,000/=
Watanzania tuwe macho.
Serikali haina hela ilikuwa inasubiri bajeti ipite kwanza, baada ya ku-overspend bajeti iliyopita, yaani jamani hata hizi nazo zinatakiwa kuwa data? Pleasee!
No,jamani mbona mnatia chumvi sana?Hao wafanyakazi wa serikalini ambao mnasema hawajalipwa ni wepi?Mimi niko serikalini.Mshahara uliochelewa ni wa mwezi uliopita tuu, ambao leo tarehe 01.09.2008 tayari umeshatoka.Naomba tujaribu kuwa na facts, tusipotoshe watu.Ni kweli serikali yetu ina makosa mengi,lakini pale panapokuwa na ukweli tuuseme kama ulivyo.
No,jamani mbona mnatia chumvi sana?Hao wafanyakazi wa serikalini ambao mnasema hawajalipwa ni wepi?Mimi niko serikalini.Mshahara uliochelewa ni wa mwezi uliopita tuu, ambao leo tarehe 01.09.2008 tayari umeshatoka.Naomba tujaribu kuwa na facts, tusipotoshe watu.Ni kweli serikali yetu ina makosa mengi,lakini pale panapokuwa na ukweli tuuseme kama ulivyo.