Serikali imechemka tena, au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imechemka tena, au?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sosoliso, May 15, 2009.

 1. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Serikali, kupitia mamlaka ya mawasiliano, imetangaza kuandikishwa kwa watumiaji simu wa mitandao yote hapa Tanzania. Maana yake ni kwamba, kabla ya kumiliki simcard, unatakiwa utambuliwe wewe ni nani, unakaa wapi na shughuli unayoifanya. Then utoe iwe ni kitambulisho, kadi ya kupigia kura, leseni au barua toka kwa mtendaji au mwenyekiti wa serikali za mitaa. Wametoa sababu ya wao kufikia maamuzi hayo. Kwanza wanasema ni kuzuia wizi wa simu, halafu kuzuia matusi, vitisho na manyanyaso yanayofanyika kwa sasa. Maana wanadai ukishasajili, basi itakuwa rahisi kufuatilia namba ya simu yenye utata na kumfahamu mwenyewe.
  Upande wa pili, kuna watumiaji ambao hawapendezwi na suala zima la kujisajili ili kuweza kutumia simu. Suala la simu ni suala huru ambalo halihusiani na mtumiaji kuingiliwa haki zake za faragha. Anaweza kutumia simu leo, kesho akabadilisha nk. Kuna baadhi ya watu wako very sensitive na haki zao za faragha. Wana JF, mnasemaje kuhusu hii debate?
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mchango wangu wa haraka haraka ni kwamba serikali haijachemsha hata kidogo. Tena nashangaa walikuwa wapi siku zote bila kufanya ili zoezi. Matumizi ya simu za mkononi yanaweza hata kuhatarisha usalama wa nchi kwani hata ukiweza kunasa kinachozumgumzwa, anayezungumza yuko eneo gani n.k lakini bado huwezi kujua anayezumgumza ni nani.

  Nchi nyingine huwezi kwenda ukanunua simcard kama inavyofanyika hapa kwetu. Ili uweze kununua simcard kwa nchi za wenzetu, inabidi uonyeshe wewe ni nani na wajue unafanyakazi gani, unaishi wapi na vitu kama hivyo la sivyo hawakuuzii simcard. Kama unazo document zinazokubalika, basi kuna form inajazwa unasaini na unapewa copy ya hiyo karatasi.

  Hili ni zoezi muhimu ila kufanikiwa kwake kutakuwa kugumu ikitiliwa maanani kwamba tayari watu walio wengi wanazo hizo simcard na wengine uenda wasijitokeze kuziandikisha.

  Tiba
   
 3. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Nadhani kuna tatizo la nini kitangulie. Nilitegemea mambo ya vitambulisho vya uraia kwanza ndo mambo ya kusajili simu yaje kwani watu hatuna identity then unataka uandikishe simu haitakuwa that effective. Baada ya vitambulisho vya uraia then hizo issue za phone registration zije.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sio lazima vitambulisho vya uraia vianze, kama ingekuwa hivyo hata account za benki, ID za makazini na kila sehemu tungesema tusubiri.... lets not complicate issues here!!

  the move is good but somehow late; tusajili simu na matatizo mengi ya mawasiliano yatapungua... kwani enzi zile za ttcl si ilikuwa kila mtu kasajiliwa; was that intrution of privacy??

  sjdgqew lbxcq-;uie;
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  akishatukanwa kigogo basi hatua huchukuliwa.
  sie tunaotukanwa na kutishiwa kila siku hata turipoti vipi wanaiweka ktk low profile priority.
  Tanzania nia nia nia nia
   
 6. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapa nafikiri serikali ipo sawa ingawa sasa kwa hali uliyombele yetu naona imekaa kisiasa zaidi. Ukisema unataka kumtambua mtu ndio mwanzo wa kuwapoteza watu hasa wale wenye kuona nyufa za viongozi na serikali kwa ujumla wake. Je kutakuwa na uwezekano wowote wa shirika la simu kuweza kuhifadhi data zangu pale pindi nitakapoongea ukweli kuhusu kingozi fulani kachemka? Na je nitaweza kulishtaki Kampuni kwa kile tunasema wamekiuka terms na privacy yangu?

  Wazo ni zuri ila naona limekaa kisiasa mno na hasa vile ilivyosisitizwa kwamba lazima kabla ya December mwaka huu
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nchi nyingi kama sio zote zilizoendela duniani huwezi kununua sim card bila kuonyesha kitambulisho au passport na details zako zinahifadhiwa. Kwahiyo ni sawa kabisa kwa serikali kufanya hivyo.
   
Loading...