Serikali imebariki gharama hizi za matibabu?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Ni kweli kuwa serikali imekuwa ikiongeza bajeti ya afya mwaka hadi mwaka. Ni kweli kuwa kutokana na serikali kuongeza bajeti ya afya, sasa tumeshuhudia Kila Wilaya imejengwa Hospitali ya Wilaya. Si tu kujenga hospital ya Wilaya, sasa nguvu kubwa imeelekezwa kwenye kujenga vituo vya afya katika Kila kata na zahanati katika kila kijiji.

Ni kweli kuwa hii ni hatua kubwa katika kuleta mapinduzi katika afya ya Binadamu. Ni kweli kuwa duniani kote maendeleo ya Taifa yanategemea zaidi afya ya Mwanadamu. Binadamu akiwa dhoofu kiafya basi ni ngumu Kwa Taifa kupata maendeleo kwani mwili wenye afya ndio unaochochea kufanya kazi.

Bahati mbaya ukweli wa haya huku mtaani hali haiko hivyo. Ni ukweli kuwa bado Wananchi wanajiuliza tafsiri halisi ya afya bora. Wananchi niliozungumza nao Wanasema kabla ya kuongeza bajeti katika afya walikuwa wanapata huduma bora kuliko ilivyo sasa.

Mhe Ummy Mwalimu unayo kazi kubwa ya kutafsiri dhana halisi ya bajeti na tiba bora iliyo halisi kwa binadamu. Bajeti iakisi gharama halisi ya matibabu.

Nitoe mifano michache . Wananchi nilioongea nao wanasema Mama Mja mzito ambaye anajifungua kwa oparesheni kwa sasa gharama yake inafikia Tshs300,000/=. Wananchi wanadai hii haijawahi kutokea. Wananchi hawa wanadai Kwa sasa kujifungua ni sawa na suala la anasa. Mkazi wa Mbalizi Mkoani Mbeya ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema Mwanamke akijifungua kwa njia salama unaweza kulipa kuanzia tshs25000/=

Mkazi huyo alisema kwa kuwa kujifungua Kwa njia ya oparesheni ni gharama kubwa, sasa kuna hospital ambazo ukienda lazima mwanamke achanwe Kwa kuwa imekuwa kawaida. Alisema utadhani hospital zingine zinafanya biashara kwa kuwa wanakazania oparesheni kuliko wakati wowote. Mkazi huyo alisema Wanawake wengi baada ya kugundua hilo wanashindwa kuwahi clinic Kwa kuhofia watafanyiwa oparesheni. Wanategea siku za mwisho akipata uchungu wa kujifingua ndipo aende. Alisema wengine wanaona Bora wajifungulie nyumbani na watozwe faini kuliko kwenda kifanyiwa opatesheni.

Pamoja na haya, duru za uchunguzi zimeonyesha ni kweli kuwa gharama za mwanamke kujifingua zimeongezeka mara dufu wakati zilipaswa kupungua kutokana na serikali kuongeza uwekezaji. Si kujifungua tu, bali utaratibu wa zamani wa mtu akiumwa na kukosa dawa unarejea. Ukisha pimwa unaelekezwa kwenda kununua dawa nje.

Swali linakuja, ni kweli kuwa maduka binafsi yana dawa kuliko hospital za serikali? Maduka binafsi yanapata wapi dawa kama hospital hazipo? Je, haya maduka binafsi yana hisa na watumishi wa hospital? Haya maswali yanakosa majibu.

Mwisho, ninauona wajibu mkubwa wa serikali kulishughulikia hili hususani afya ya binadamu. Nchi yetu inahitaji watu kuzaliana ili kuweza kujipatia maendeleo. Huwezi kupata maendeleo kama huna watu na huwezi kuwa na watu kama kuzaa inakuwa ni anasa. Mtu anapotaka kujifungua anaanza tena kufikiria gharama za hospitali. Waziri wa afya ni Mwanamke, Rais wa nchi ni Mwanamke, ninadhani combination hii iwe tiba kwa wanawake ambao sasa kupata watoto wameanza kuona kero.

Tafakari.
 
CCM pamoja na watawala wote wanatibiwa bure au kulipiwa na serikali kupitia kodi za umma popote pale duniani ndiyo maana hawajui machungu ya kulipa hizi gharama kubwa za matitabu, fuatilia ukurasa wa Malisa ndiyo utajua kuwa tuna serikali ya hovyo bora hata ya wakolini vitu vingi vilikuwa bure.
 
Back
Top Bottom