Serikali ilitizame hili

Aug 30, 2022
5
4
Nani atutetee nani atusemee maisha yame badilika hakuna wa kuongea kila mtu anaogopa kusema ata pale unapo stahili haki hakuna kusema maana siasa ina tupoteza, wao walitaka tufanye kazi na maisha ya endelee.

Pia kazi ndiyo chachu ya maendeleo yetu pamoja na taifa, ila pindi unapo fanya kazi akuna uhuru wala amani. Machinga pamoja na wajasiriamali wanazidi kuumia na kunyanyaswa kila siku.

Nani awasemee? Maisha yamebadilika, haki imetoweka, sasa twaona giza matumaini kwa vijana walio jiajiri pamoja na wa mama yamepotea. Nani awasemee, migambo wame tanda mjini kwa kuwakimbiza machinga na wajasiliamali wadogo wadogo na huku mitaani wenyeviti na watendaji wamekuwa wakiwakamata na kukamata bidha ama biashara zao.

Imekua ikijitokeza mara kwa mara, nani awasemee vilio vyao? Ni juu ya serikali, wamekuwa wakilia na kuugulia maumivu, serikali iliagiza machinga na wajasiriamali wadogo wadogo wapewe maeeneo ya biashara walipewa. Ila changamoto ni maeneo, miundombinu ya maeneo sio rafiki kwa biashara.
 
Back
Top Bottom