Serikali ilihusika kusababisha ajali ya basi la TAQWA na lori la AZAM

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Serikali ilihusika kusababisha ajali ya basi la TAQWA na lori la AZAM

Namsikitikia sana dereva wa lori la Azam na msaidizi wake walivyopotezewa maisha yao kwa uzembe wa dereva wa Taqwa na Tanroads. Nasikitika pia kwa maisha yaliyopotea ya abiria wasio na hatia. Jibu la haraka la mkuu wa polisi na mkuu wa wilaya ya Biharamulo ni kuwa ajali ilisababishwa na uzembe wa madereva. SIO KWELI.

Barabara eneo la Lusahunga ina mashimo mashimo, na mengine ni makubwa kiasi cha kuweza kusababisha ajali endapo dereva atalikwaa bila tahadhari. TANROADS wanafanya ukarabati usioisha wa kufukia mashimo yale. Kwa kujihami ili wasigongwe na magari, vibarua wa TANROADS huweka mawe makubwa barabarani ili magari yapunguze mwendo. Pia huweka kibao chenye maneno, "man at work."

Kilichotokea Lusahunga ni kwamba, mawe makubwa yalipangwa karibu kabisa na mashimo yaliyokuwa yakizibwa na kibao kiliwekwa karibu kabisa na mawe yale. Dereva mzembe wa Taqwa alipuuza kibao kilichokuwa kimeziba mawe yale na pengine angekisukumia pembeni tu na kujiendea zake na mbio kama kawaida. Lakini kutahamaki aliona mzigo wa mawe makubwa mbele tu ya kibao na hivyo akahamia upande wa kulia na kukutana na dereva wa Azam ambaye alikuwa akijitembelea kwenye site yake na kilichofuata wote mnakifahamu.

Ni makosa basi kwa mkuu wa polisi kuhitimisha kwa kusema ajali ilisababishwa na uzembe wa madereva. Alipaswa kusema ajali ilisababishwa na uzembe wa dereva wa Taqwa na wafanyakazi wa Tanroads.

chanzo cha habari : dereva wa lori la mafuta T909 ASU aliyekuwa eneo la tukio akielekea Bujumbura na ambaye yuko tayari kuhojiwa na kuelezea ukweli huo bila woga.
 
Watanzania tuna matatizo sana. Kila siku lawama juu ya serikali. Kama dereva mwenye uzoefu kwanini unakimbiza gari sehemu ya hatari au barabara mbovu? Tuwe wastarabu mwisho mtu atamlaumu mamake kwanini kamleta duniani.
 
Sijamtetea dereva mwenye makosa. Lakini, ni sahihi kwa TANROADS kupanga mawe barabarani badala ya kutimia taratibu sahihi za kiusalama? Ni haki pia kumbebesha lawama dereva wa Azam ambaye alipamiwa na basi? Ni sahihi kuelezea chanzo cha ajali kabla ya kujiridhisha kuwa ni sahihi?
 
Ukweli ni adui wa watendaji wengi wa serikali ya Tanzania. Sioni shida yoyote kama mkuu wa polisi angesema wazi kuwa ajali ilisababishwa na Tanroads na Taqwa. Hii inapelekea serikali kutowajibika. Tufanye nini basi? Tuwafundishe watoto wetu kusema ukweli! Hata kizazi hiki kikiisha basi watapata ustawi wa taifa hili.
 
Sijamtetea dereva mwenye makosa. Lakini, ni sahihi kwa TANROADS kupanga mawe barabarani badala ya kutimia taratibu sahihi za kiusalama? Ni haki pia kumbebesha lawama dereva wa Azam ambaye alipamiwa na basi? Ni sahihi kuelezea chanzo cha ajali kabla ya kujiridhisha kuwa ni sahihi?
we mjinga kweli wasipange mawe kwa madereva bangi kama huyo unayemtetea wa Taqwa ushasema alipuuzia kibao cha tahadhari sasa hebu elezea usalama wa wajenzi wa barabara hiyo katika hali ya uwendawazimu wa madereva
 
Hili la kuniita mjinga siliafiki na sitakuita mjinga ili nisije na mimi kuwa mjinga. Ni ujinga kwa watumishi wa TANROADS kujikinga na ajali kwa kutumianjia zinazosababisha ajali na kuua watu. Na mbaya zaidi wakati ajali inatokea hawakuwepo lakini mawe yao yalikuwepo.
 
Back
Top Bottom