Serikali iko wapi kwenye suala la mchele feki?

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Maadui wakubwa wa Tanzania ni maradhi, ujinga na umaskini.

Hili la watu kulishwa mchele feki linaondoa vita ya maadui wetu watatu. Kwani kutokana na watu kula mchele huo wa "plastic" adui maradhi tunamkaribisha kwa mikono miwili.

Siku za karibuni kuna video nyingi zimekuwa zinazunguka mitandaoni kuonyesha watu wakidundisha wali kama kitenesi. Na jibu la mwisho kutoka serikalini lilikuwa hata mchele wa kawaida ukiiva sana unadunda.

Lakini je kudunda kule ndio kumeanza leo? Kwani siku zote tulikuwa hatuli wali? Mbona haya hayakuwepo?

Kama kufunga chipsi tu kwenye mfuko wa plastic kuna madhara kiafya vipi kuhusu kula wali wa plastic?

Kama serikali inasema taarifa hizo ni uongo na waliorecord sura zao zinaonekana je sheria ya mtandao iko kwa maswala y siasa tu, kwanini hawa watu wasitumike kupata ushahidi?
"Ni bora simu feki kuliko chakula feki"
 
mkuu hawa watu huwa wanasubiri ripoti za mezani wengi huwa hawataki kuchunguza kwa kina. kuna mamlaka ya chakula na dawa nayo imekaa kimya kiukweli zile video za wachina lazima tuogope kuwa kuna uwepo wa mchele kama huu ikizingatiwa kuwa china mojawapo ya nchi tunayofanya nayo biashara kwa asilimia kubwa bidhaa nyingi tunachukua huko. tunahitaji wafanye uchunguzi wa kina kutupa majibu sahihi sio kusubiri ripoti za mezani. anyway ngoja nikanunue kule mbeya maana hakuna bandari kusema watauleta huo wa plastic
 
Ndo maana tunataka ushahidi, serikali ifuatilie leads tupate ushahidi. Wewe lini umeona wali unadunda
Ebu acha hizo bwana! TFDA waliomba mwenye ushahidi awasiliane nao hakuna ata mtu aliyejitokeza..!
 
Anyway ila ujue serikali haifanyi kazi katika mitandao ujue, ndiyo maana ya kuwa na taasisi km TFDA.
Mbona watu wanashikwa kwa uchochezi wa mitandao. Mbona habari nyingi za mitandaoni wanatoa ufafanuzi kwanini kimya kwenye hili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom