Azimio la TANU ndio hili la ASP liko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azimio la TANU ndio hili la ASP liko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Dec 26, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by amini // 25/12/2011 // Habari // No comments

  [​IMG]CHAMA CHA MAPINDUZI
  AZIMIO LA ARUSHA
  NA
  SIASA YA TANU JUU YA
  UJAMAA NA KUJITEGEMEA
  Imetolewa na Idara ya Habari,
  TANU, Dar es Salaam, 1967
  1
  SEHEMU YA KWANZA
  Imani ya Tanu
  SIASA YA TANU NI KUJENGA NCHI YA UJAMAA, MISINGI YA UJAMAA
  IMETAJWA KATIKA KATIBA YA TANU, NAYO NI HII
  Kwa kuwa TANU inaamini:-
  (a) Kwamba binadamu wote ni sawa;
  (b) Kwamba kila mtu anastahili heshima;
  (c) Kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya
  kushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, ya
  Mikoa hadi Serikali Kuu;
  (d) Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo
  yake, ya kwenda anakotaka, wa kuamini dini anayotaka na
  wa kukutana na watu mradi havunji Sheria;
  (e) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii
  hifadhi ya maisha yake na ya mali yake aliyonayo kwa
  mujibu wa Sheria;
  2
  (f) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki
  kutokana na kazi yake
  (g) Kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili
  wanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana
  kwa vizazi vyao;
  (h) Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwenda
  sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia
  muhimu za kuukuza uchumi; na
  (i) Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe,
  kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili
  kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya
  mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine
  na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani
  na siasa ya watu wote kuwa sawa.
  MADHUMUNI YA TANU
  Kwa hiyo basi, makusudi na madhumuni ya TANU yatakuwa kama
  hivi yafuatavyo:-
  (a) Kuudumisha uhuru wa nchi yetu na raia wake;
  3
  (b) Kuweka heshima ya mwanadamu kwa kufuata barabara
  kanuni za Tangazo la Ulimwengu la Haki za Binadamu.
  (c) Kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa na Serikali ya
  watu ya kidemokrasia na ya kisoshalist;
  (d) Kushirikiana na vyama vyote vya siasa katika Afrika
  vinavyopigania uhuru wa bara lote la Afrika;
  (e) Kuona kwamba Serikali inatumia mali yote ya nchi yetu kwa
  kuondoshea umaskini; ujinga na maradhi;
  (f) Kuona kwamba Serikali inasaidia kwa vitendo kuunda na
  kudumisha vyama vya ushirika;
  (g) Kuona kwamba kila iwezekanapo Serikali inashiriki hasa
  katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu;
  (h) Kuona kwamba Serikali inatoa nafasi zilizo sawa kwa wote,
  wake kwa waume, bila kujali rangi, kabila, dini au hali;
  (i) Kuona kwamba Serikali inaondoa kila namna ya dhuluma,
  vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu;
  4
  (j) Kuona kwamba Serikali ya nchi yetu inasimamia barabara
  njia kuu za kuzalisha mali na inafuata siasa ambayo
  itarahisisha njia ya kumiliki kwa jumla mali za nchi yetu;
  (k) Kuona kwamba Serikali inashirikiana na dola nyingine katika
  Afrika katika kuleta Umoja wa Afrika.
  (l) Kuona kwamba Serikali inajitahidi kuleta amani na salama
  ulimwenguni kwa njia ya Chama cha Umoja wa Mataifa.
  5
  SEHEMU YA PILI
  SIASA YA UJAMAA
  (a) Hakuna Unyonyaji:
  Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi: haina
  ubepari wala ukabaila. Haina tabaka mbii za watu: tabaka ya
  chini ya watu wanaoishi kwa kufanya kazi, na tabaka ya juu ya
  watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa
  kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi
  hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi
  aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali
  hayapitani mno.
  Katika nchi ya Ujamaa kamili watu peke yao ambao huishi
  kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao
  ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao,
  kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya
  kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe.
  Nchi yetu ni nchi ya Wakulima na Wafanya kazi, lakini sin
  chi ya Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na
  vishawishi vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza
  ikapanuka na kuenea.
  6
  (b) Njia kuu za uchumi ni chini ya wakulima na wafanya
  kazi:
  Namna ya pekee ya kujenga na kudumisha ujamaa ni
  kuthibitisha kuwa njia kuu zote za uchumi wa nchi yetu
  zinatawaliwa na kumilikiwa na Wakulima na Wafanyakazi
  wenyewe kwa kutumia vyombo vya Serikali yao na Vyama
  vyao vya Ushirika. Pia ni lazima kuthibitisha kuwa Chama
  kinachotawala ni Chama cha wakulima na wafanyakazi.
  Njia kuu za Uchumi ni: kama vile ardhi, misitu, madini,
  maji, mafuta na nguvu za umeme; njia za habari, njia za
  usafirishaji; mabenki, na bima; biashara na nchi za kigeni na
  biashara za jumla; viwanda vya chuma, mashini, silaha, magari,
  simenti, mboleo; nguo, na kiwanda cho chote kikubwa
  ambacho kinategemewa na sehemu kubwa ya watu katika
  kupata riziki zao au kinachotegemewa na viwanda vingine;
  mashamba makubwa na hasa yale yanayotoa mazao ya lazima
  katika viwanda vikubwa.
  Baadhi ya njia hizi na nyingine zisizotajwa hapa hivi sasa
  zinamilikiwa au kutawaliwa na Serikali ya Wananchi.
  7
  (c) Kuna Demokrasi:
  Nchi haiwi ni ya Ujamaa kwa sababu tu njia zake kuu au
  zote za uchumi hutawaliwa na humilikiwa na Serikali. Sharti
  Serikali iwe inachaguliwa na kuongozwa na Wakulima na
  Wafanya kazi wenyewe. Serikali ya Makaburu wa Rhodesia au
  Afrika ya Kusini ikitawala au kumiliki njia zote za uchumi, hiyo
  itakuwa ni njia ya kukomaza Udhalimu siyo njia ya kuleta
  Ujamaa. Hakuna Ujamaa wa kweli pasipo na Demokrasi ya
  kweli.
  (d) Ujamaa na Imani:
  Lakini Ujamaa hauwezi kujijenga wenyewe. Kwani
  Ujamaa ni imani. Hauna budi kujengwa na watu wanaoamini
  na kufuata kanuni zake. Mwana-TANU wa kweli ni Mjamaa, na
  Wajamaa wenzie, yaani waamini wenzie katika imani hii ya
  kisiasa na uchumi ni wote wale wanaopigania haki za wakulima
  na wafanyakazi katika Afrika na po pote duniani. Wajibu wa
  kwanza wa mwana-TANU na hasa kiongozi wa TANU, ni kutii
  kanuni hizi za ujamaa hasa katika maisha yake mwenyewe. Na
  hasa mwana-TANU kiongozi hataishi kwa jasho la mtu
  mwingine au kufanya jambo lo lote ambalo ni la kibepari au
  kikabaila.
  8
  Utimizaji wa shabaha hizo na nyinginezo zinazofuatana na
  siasa ya ujamaa unategemea sana viongozi kwa sababu ujamaa
  ni imani na ni vigumu kwa viongozi kujenga siasa ya ujamaa
  ikiwa hawaikubali imani hiyo.
  9
  SEHEMU YA TATU
  SIASA YA KUJITEGEMEA
  Tunapigana vita:
  TANU ina vita vya kulitoa Taifa letu katika hali ya unyonge na
  kulitia katika hali ya nguvu; vita vya kuwafanya wananchi wa
  Tanzania (na wananchi wa Afrika) watoke katika hali ya dhiki na
  kuwa katika hali ya neema.
  Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha,
  na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya
  tuonewe, tunyonywe, na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi;
  mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena.
  Mnyonge hapigani kwa Fedha:
  Lakini ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua
  silaha; kwani silaha tuliyochagua ni fedha. Tunataka kuondoa
  unyonge wetu kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo
  sisi wenyewe hatuna. Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu, na
  vitendo vyetu ni kama tumekata shauri kwamba bila fedha mapinduzi
  yetu hayawezekani. Ni kama tumesema, “Fedha ndiyo msingi wa
  maendeleo. Bila fedha hakuna maendeleo”!
  10
  Hii ndiyo imani yetu ya sasa. Viongozi wa TANU mawazo yao ni
  kwenye fedha. Viongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi,
  mawazo yao na matumaini yao ni kwenye fedha. Viongozi wa
  wananchi na wananchi wenyewe katika TANU, NUTA, Bunge, UWT.,
  Vyama vya Ushirika, TAPA na makundi mengine ya wananchi,
  mawazo yao na maombi yao na matumaini yao ni FEDHA. Ni kama
  wote tumekubaliana na tunasema kwa sauti moja, “Tukipata fedha
  tutaendelea, bila fedha hatutaendea”!
  Mpango wetu wa maendeleo ya miaka mitano shabaha zake
  kwa kifupi ni shibe zaidi, elimu zaidi na afya zaidi. Na silaha yetu
  tuliyotilia mkazo sana ni fedha. Ni kama tumesema, “Katika miaka
  mitano ifuatayo tunakusudia kujiongezea shibe, elimu na afya, na ili
  kutimiza shabaha hizo tunatumia $ 250,000,000”. Kama tumetaja na
  tunapotaja vyombo vingine vya kututimizia shabaha hizo tunavitaja
  kama nyongeza tu; lakini chombo kikubwa katika akili zetu, silaha
  kubwa katika mawazo yetu, ni FEDHA.
  Mheshimiwa Mbunge anaposema kuwa wananchi wa sehemu
  yake wana shida ya maji, je Serikali ina mpango gani wa kuondoa
  shida hiyo? Jibu analotaka ni kwamba: Serikali inao mpango wa
  kuwapa maji wananchi wa sehemu hiyo – KWA FEDHA.
  Mbunge mwingine anaposema kuwa sehemu yake haina
  barabara au shule au hospitali au vyote, je, Serikali ina mpango gani?
  11
  Naye pia jibu ambalo angependa kupewa ni kuwa Serikali inao
  mpango safi kabisa wa kutengeneza barabara au kujenga shule au
  hospitali au vyote kwa wananchi wa sehemu ya Mbunge Mheshimiwa
  huyo – kwa FEDHA.
  Kiongozi wa NUTA anapoikumbusha Serikali kuwa mishahara ya
  chini kwa wafanyakazi wengi bado ni midogo mno na nyumba
  wanazolala si nzuri, je, Serikali inao mpango gani? Jibu apendalo
  kusikia ni kuwa Serikali inao mpango maalum wa kuongeza
  mishahara na kujenga majumba bora – KWA FEDHA.
  Kiongozi wa TAPA anaposema kuwa wanazo shule nyingi sana
  ambazo hazipati msaada wa Serikali. Je Serikali ina mpango gani wa
  kuzisaidia shule hizo, jibu analopenda kusikia ni kuwa Serikali iko
  tayari kabisa kesho asubuhi kuzipa shule hizo msaada unaotakiwa -
  wa FEDHA!
  Kiongozi wa Chama cha Ushirika akitaja shida yo yote ya
  mkulima jibu apendalo kusikia ni kuwa Serikali itaondoa shida hizo za
  mkulima – kwa FEDHA. Mradi kila shida inayolikabili Taifa letu
  wananchi tunawaza Fedha, Fedha, Fedha!
  Mwaka hata mwaka kila Wizara na kila Waziri hufanya
  makadirio yake ya matumizi – yaani fedha wanazohitaji mwaka huo
  kwa kazi za kawaida na mipango ya maendeleo. Waziri mmoja tu na
  12
  Wizara moja tu hushughulikia pia kufanya makadirio ya mapato. Ni
  Waziri wa Fedha. Kila Wizara ina mipango mizuri sana ya
  maendeleo. Wizara zinapoleta makaidirio yao ya matumizi huwa
  zinaamini kwamba fedha zipo ila mkorofi ni Waziri wa Fedha na
  Wizara yake. Na kila mwaka lazima Waziri wa Fedha na Wizara yake
  awaambie Mawaziri wenzake na Wizara zao kwamba hakuna fedha.
  Na kila mwaka Wizara zote huinung’unikia Wizara ya Fedha kwa
  kupunguza Makadirio yao ya matumizi.
  Kadhalika Wabunge na Viongozi wengine wanapodai Serikali
  itimize mipango mbali mbali huwa nao wakiamini kwamba fedha zipo
  ila mkorofi ni Serikali. Lakini kukataa huku kwa Wizara, na Wabunge
  na Viongozi wengine hakuwezi kuondoa ukweli; nao ni kwamba
  Serikali haina fedha.
  Na kusema kuwa Serikali haina fedha maana yake ni nini?
  Maana yake ni kuwa Wananchi wa Tanzania hawana fedha. Kiasi
  walichonacho hutozwa kodi, na kodi hiyo ndiyo inayoendesha
  shughuli za Serikali hivi sasa na maendeleo mengine ya nchi.
  Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidi za maendeleo kwa fedha
  tunataka Serikali itumie fedha zaidi. Na kama Serikali haina fedha
  zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi.
  Ukidai Serikali itumie fedha zaidi unataka izipate; na njia ya
  kuzipata ni kodi. Kudai Serikali itumie fedha nyingi bila kukubali kodi
  13
  zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi
  bila kutaka Ng’ombe akamuliwe tena. Lakini kukataa huku kukiri
  kwamba tunapodai Serikali itumie fedha zaidi nia yetu ni kutaka
  Serikali iongeze kodi kunaonyesha kuwa tunatambua ugumu wa
  kuongeza kodi. Tunatambua kuwa ng’ombe hana maziwa zaidi;
  kwamba hata ng’ombe mwenyewe angependa ayanywe maziwa hayo
  au yanywewe na ndama wake au yauzwe yamfae yeye na jamaa
  yake; utashi huo hauwezi kuondoa ukweli kwamba hana maziwa
  zaidi.
  Fedha kutoka nje ya Tanzania, Je?
  Njia moja tunayotumia kujaribu kuepukana na lazima hii ya kukiri
  kodi zaidi ikiwa twataka fedha zaidi ni kutilia sana mkazo fedha za
  kutoka nje ya Tanzania. Fedha hizi za kutoka nje ni za aina tatu:-
  (a) Zawadi: Yaani Serikali ya nje iipe Serikali yetu fedha za bure
  tu kama sadaka kwa ajili ya mpango fulani wa maendeleo.
  Wakati mwingine shirika lo lote la nje liipe Serikali yetu au
  Shirika jingine katika nchi yetu msaada fulani kwa ajili ya
  maendeleo.
  (b) Mkopo: Sehemu kubwa ya fedha tunazotazamia kupata
  kutoka nchi za kigeni si zawadi au sadaka, bali ni mkopo.
  Serikali ya nje au Shirika la nje, kama vile Benki, hukopesha
  14
  Serikali yetu fedha fulani kwa ajili ya kazi zetu za
  maendeleo. Mkopo huu huwa una masharti yake ya kulipa,
  kama vile muda wa kulipa, na kima cha faida.
  (c) Raslimali ya Kibiashara: Aina ya tatu ambayo pia ni kubwa
  kuliko ya kwanza, ni ile ya fedha za watu au makampuni
  yanayotaka kuja katika nchi yetu kuanzisha shughuli mbali
  mbali za uchumi kwa manufaa yao wenyewe. Na sharti
  kubwa walitakalo jamaa hawa wenye fedha zao ni kwamba
  shughuli yenyewe iwe ni ya faida – kwao – na pia kwamba
  Serikali iwaruhusu kuondoa faida hiyo Tanzania na kuipeleka
  kwao. Hupenda pia kwa jumla Serikali iwe na siasa
  wanayokubaliana nayo au ambayo haihatarishi uchumi wao.
  Hizo ndizo njia tatu kubwa za kupata fedha kutoka nje ya
  nchi yetu. Kuna mazungumzo mengi ajabu juu ya jambo hili
  la kupata fedha kutoka nchi za kigeni. Serikali yetu na
  viongozi wetu wa makundi mbalimbali hawaachi kufikiria njia
  za kupata fedha kutoka nje. Na tukizipata au japo tukipata
  ahadi tu ya kuzipata mara magazeti yetu, au radio zetu na
  viongozi wetu hutangaza jambo hilo ili kila mtu ajue kuwa
  neema imekuja au iko njiani inakuja. Tukipata msaada
  hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; tukipata kiwanda
  kipya hutangaza; tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda
  kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au
  15
  shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda, mara
  hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo
  hayo. Na kisa? Ni kuwajulisha wananchi kwamba, tunaanza
  mazungumzo ya neema!
  TUSITEGEMEE FEDHA KULETA MAENDELEO
  Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu
  kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini.
  Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza
  kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka
  nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni ujinga kwa sababu mbili.
  Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo
  zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani
  ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga
  viwanda katika nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo.
  Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi zote
  zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa
  msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata
  katika nchi ile ile, matajiri huwa hawatoi fedha zao kwa hiari ili
  zisaidie Serikali kuondoa dhiki.
  Njia ya kuzipata fedha za matajiri ili zisaidie umma ni kuwatoza
  kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi. Ndiyo
  16
  maana japo tungewakamua vipi wnanachi na wakazi wa Tanzania,
  matajiri na maskini, hatuwezi kupata fedha za kutosha kutimiza
  mipango yetu ya maendeleo. Wala duniani hakuna Serikali ambayo
  yaweza kuyatoza kodi mataifa yenye neema, yakipenda yasipende, ili
  kusaidia mataifa yenye dhiki. Hata hizo zisingelitosha. Hakuna
  Serikali ya Dunia nzima. Fedha ambazo nchi zenye neema hutoa
  huwa kwa wema wao, au hiari yao au kwa manufaa yao wenyewe.
  Haiwezekani basi, tupate fedha za ktuosha kwa njia hiyo.
  MISAADA NA MIKOPO
  VITAHATARISHA UHURU WETU
  Pili, japo kama tungeweza kuzipata; hivyo ndivyo tunavyotaka
  kweli? Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli
  hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya
  Taifa jingine kwa maendeleo yake. Hata kama pangetokea Taifa au
  mataifa ambayo yako tayari kutupa fedha zote tunazohitaji
  kuendesha mipango yetu ya maendeleo isingekuwa sawa kwa nchi
  yetu kuipokea misaada hiyo bila kujiuliza matokeo yake yatakuwa nini
  kwa Uhuru wetu na uzima wetu.
  Msaada ambao ni kama chombo cha kuongeza juhudi, au
  nyenzo ya juhudi, ni msaada ambao una manufaa. Lakini msaada
  17
  unaoweza ukawa sumu ya juhudi si msaada wa kupokea bila kujiuliza
  maswali.
  Kadhalika mikopo. Kweli mkopo ni bora kuliko misaada ya
  “bure”. Mkopo nia yake ni kuongeza jitihada au kuifanya jitihada
  itoe matunda mengi zaidi. Sharti moja la mkopo huwa ni kuonyesha
  jinsi utavyoweza kuulipa. Maana yake ni kwamba sharti uonyeshe
  kuwa unakusudia kuufanyia kazi itakayoleta manufaa ya
  kukuwezesha kuulipa.
  Lakini hata mikopo ina kikomo. Sharti upime uwezo wa kulipa.
  Tunapokopa fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama
  tulivyokwisha sema Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha watu
  maskini mikopo ambayo inawazidi kimo si kuwasaidia bali ni
  kuwaumiza. Na hasa inapokuwa, mikopo hiyo ambayo wanatakiwa
  walipe haikuwafaidia wao, bali ilifaidia watu wachache tu.
  Na Viwanda vya wenye raslimali zao je? Ni kweli tunavitaka.
  Hata tumepitisha katika Bunge sheria ya kulinda raslimali ya wageni
  wanaoanzisha mipango mbali mbali ya uchumi katika nchi yetu. Nia
  yetu na matumaini yetu ni kuwafanya waone kuwa Tanzania ni nchi
  inayofaa kuingiza raslimali zao. Kwani raslimali yao itakuwa salama
  italeta faida. Na faida hiyo wenyewe wataweza kuiondoa bila
  vipangimizi. Tunayo matumaini ya kupata fedha za maendeleo mbali
  mbali kwa njia hii. Lakini hatuwezi kupata za kutosha. Lakini hata
  18
  kama tungeweza kuwaridhika kabisa Wageni hao na Makampuni
  hayo mpaka yakubali kuanzisha mipango yote ya uchumi tunayohitaji
  katika nchi yetu, hivyo ndivyo tunavyotaka kweli?
  Kama tungeweza kushawishi wenye raslimai wa kutosha kutoka
  Amerika, na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na
  mipango mingine yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii, hivi
  kweli tungekubali bila kujiuliza maswali? Tungekubali kweli kuacha
  uchumi wetu wote uwe mikononi mwa wageni kwa ajili ya kupata
  faida na kuipeleka katika nchi zao? Hata kama wasingedai
  kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali faida yote watakayopata
  wataitumia hapa hapa Tanzania kwa maendeleo zaidi. Hivi kweli
  tungekubali jambo hili bila kujiuliza hasara zake kwa Taifa letu? Huu
  Ujamaa tunaosema kuwa ndiyo shabaha yetu tungeujengaje?
  Twawezaje kutegemea nchi za nje na Kampuni za nje kwa
  misaada na mikopo na raslimali kwa maendeleo yetu bila kuhatarisha
  uhuru wetu? Waingereza wana methali isimayo “Amlipaye mwimbaji
  ndiye huchagua wimbo”. Tutawezaje kutegemea nchi za kigeni na
  Makampuni ya kigeni kwa sehemu kubwa ya maendeleo yetu bila
  kuzipa nchi hizo na makampuni hayo sehemu kubwa ya uhuru wetu
  wa kutenda tupendavyo. Ukweli wenyewe ni kwamba hatuwezi.
  Tukariri basi. Tumefanya makosa kuchagua fedha, kitu
  ambacho hatuna, kiwe ndicho chombo kikubwa cha mipango yetu ya
  19
  maendeleo. Tunafanya makosa kudhani kuwa tutapata fedha kutoka
  nchi za kigeni. Kwanza, kwa sababu kwa kweli hatuwezi kupata
  fedha za kutosha kwa maendeleo yetu. Na pili, hata kama
  tungeweza, huko kutegemea wengine kungehatarisha uhuru wetu na
  siasa nyingine za nchi yetu.
  TUMEKAZANIA MNO VIWANDA
  Kwa sababu ya kutilia mkazo fedha tumefanya kosa kubwa la
  pili. Tumekazania mno viwanda. Kama vile tulivyosema “Bila Fedha
  hakuna maendeleo,” ni kama twasema pia “Viwanda ndiyo
  maendeleo. Bila viwanda hakuna maendeleo”. Hii ni kweli siku
  tutakapokuwa na fedha nyingi, tutaweza kusema kwamba
  tumeendelea. Tutaweza kusema, “tulipoanza mipango yetu tulikuwa
  hatuna fedha za kutosha na upungufu huu wa fedha ulitupunguzia
  nguvu za kuendesha maendeleo yetu haraka zaidi. Lakini leo
  tumeendelea na tunazo fedha za kutosha”. Tumeendelea,kwa hiyo,
  tunazo fedha za kutosha”. Yaani fedha zetu zitakuwa zimeletwa na
  maendeleo.
  Kadhalika siku tutakapokuwa na viwanda tuna haki ya kusema
  kuwa tumeendelea. Maendeleo yatakuwa yametuwezesha kupata
  viwanda. Kosa tunalofanya ni kudhani kwamba maendeleo yetu
  yataanza kwa viwanda. Ni kosa maana hatuna uwezo wa kuanzisha
  viwanda vingi vya kisasa katika nchi yetu. Hatuna fedha
  20
  zinazohitajiwa na hatuna ufundi unaohitajiwa. Haitoshi kusema kuwa
  tutakopa fedha na kuazima mafundi kutoka nje kuja kuanzisha
  viwanda hivyo. Kosa hili jibu lake ni lile lile kwamba hatuwezi kupata
  fedha za kutosha na kuazima mafundi wa kutosha kutuanzishia
  viwanda hivyo tunavyotaka. Na pia kwamba hata kama tungeweza
  kupata msaada huo kuutegemea huko kunaweza kukapotosha siasa
  yetu ya Ujamaa. Siasa ya kualika msululu wa mabepari kuja kuhozi
  viwanda katika nchi yetu ingefanikiwa kutupatia viwanda vyote
  tunavyotaka, basi ingefanikiwa pia kuzuia maendeleo ya Ujamaa. Ila
  labda tuwe tunaamini kwamba bila kujenga ubepari kwanza hatuwezi
  kujenga Ujamaa.
  TUMJALI ZAIDI MKULIMA VIJIJINI
  Vile vile mkazo wa fedha na wa viwanda unatufanya tukazanie
  zaidi maendeleo ya mijini. Tunatambua kuwa hatuwezi kupata fedha
  za kutosha kuleta maendeleo katika kila kijiji na ambayo yatamfaa
  kila mwananchi. Tunajua pia kuwa hatuwezi kujenga kiwanda katika
  kila kijiji ili kisaidie kuleta maendeleo ya fedha na viwanda katika kila
  kijiji; jambo ambalo tunajua kuwa haliwezekani. Kwa ajili hiyo, basi,
  fedha zetu huzitumia zaidi katika miji na viwanda vyetu pia hujengwa
  katika miji.
  Na zaidi ya fedha hizi huwa ni mikopo. Japo zijenge shule,
  hospitali, majumba au viwanda ni fedha za mikopo. Hatimaye lazima
  21
  zilipwe. Lakini ni dhahiri kwamba haziwezi kulipwa kwa fedha
  zinazotokana na maendeleo ya mijini au maendeleo ya viwanda.
  Hazina budi zilipwe kwa fedha tunazopata kutokana na vitu
  tunavyouza katika nchi za nje. Kutokana na viwanda vyetu hatuuzi
  na kwa muda mrefu sana hatutauza vitu vingi katika nchi za nje.
  Viwanda vyetu zaidi ni vya kutusaidia kupata vitu hapa hapa
  ambavyo mpaka sasa tunaviagiza kutoka nchi za nje. Itapita miaka
  mingi kabla ya kuweza kuuza katika nchi za nje vitu vinavyotokana na
  viwanda vyetu.
  Kwa hiyo ni dhahiri kwamba fedha tutakazotumia kulipa madeni
  haya ya mikopo ya fedha kwa maendeleo na viwanda mijini
  hazitatoka mijini na wala hazitatokana na viwanda. Zitatoka wapi,
  basi? Zitatoka vijijini na zitatokana na KILIMO. Maana ya ukweli huu
  ni nini? Ni kwamba wale wanaofaidi maendeleo yanayotokana na
  fedha tunazokopa sio kwa kweli watakaozilipa. Fedha zitatumika
  zaidi katika miji lakini walipaji watakuwa zaidi ni wakulima.
  Jambo hili linafaa kukumbukwa sana, maana kuna njia nyingi
  za kunyonyana. Tusisahau hata kidogo kwamba wakaaji wa mijini
  wanaweza wakawa wanyonyaji wa jasho la wakulima wa vijijini.
  Hospitali zetu kubwa zote ziko katika miji. Zinafaidia sehemu ndogo
  sana ya wananchi wa Tanzania. Lakini kama tumezijenga kwa fedha
  za mkopo walipaji wa mkopo huo ni wakulima, yaani wale ambao
  hawafaidiwi sana na hospitali hizo. Mabarabara ya lami yako katika
  22
  miji, kwa faida ya wakaaji wa mijini na hasa wenye magari. Kama
  mabarabaraba hayo tumeyajenga kwa fedha za mikopo walipaji ni
  wakulima; na fedha zilizonunua magari yenyewe zilitokana na mazao
  ya wakulima. Taa za umeme, maji ya mabomba, mahoteli na
  maendeleo mengine yote ya kisasa yako zaidi katika miji. Karibu
  yote yametokana na fedha za mikopo na karibu yote hayana faida
  kubwa kwa mkulima, lakini yatalipwa kwa fedha zitakazotokana na
  jasho la mkulima. Tusisahau jambo hili.
  Japo tunapotaja unyonyaji hufikiria mabepari, tusisahau kuwa
  bahari ina samaki wengi. Nao hutafunana. Mkubwa hutafuna mdogo
  na mdogo naye humtafuna mdogo zaidi. Katika nchi yetu twaweza
  kugawa wananchi kwa njia mbili. Mabepari na Makabaila upande
  mmoja; na wafanya kazi na wakulima upande mwingine. Pia
  twaweza tukagawa wakaaji wa mijini upande mmoja na wakulima wa
  vijijini upande mwingine. Tusipoangalia tutakuja kugundua kuwa
  wakaaji wa mijini nao ni wanyonyaji wa wakulima.
  WANANCHI NA KILIMO
  Maendeleo ya nchi huletwa na watu, hayaletwi na fedha.
  Fedha ni matokeo siyo msingi wa maendeleo. Ili tuendelee twahitaji
  vitu vine: (i) Watu; (ii) Ardhi; (iii) Siasa safi na (iv) Uongozi bora.
  Nchi yetu ina zaidi ya watu milioni kumi na eneo la eka 362,000.
  23
  MAENDELEO YATALETWA NA KILIMO
  Sehemu kubwa ya eneo hili ni yenye rutuba na mvua ya
  kutosha. Nchi yetu inaweza kutoa mazao ya aina mbali mbali
  ambayo tunayahitaji kwa chakula na kwa fedha.
  Mazao ya chakula (na fedha kama tukiyatoa kwa wingi) ni
  kama vile mahindi, mchele, ngano, maharage, karanga n.k. Mazao
  ya fedha ni kama vile mkonge, pamba, kahawa, tumbaku, pareto,
  chai n.k.
  Pia nchi yetu ni nzuri sana kwa ufugaji wa ng’ombe, mbuzi,
  kondoo, kuku n.k. Pia twaweza kuvua samaki katika maziwa, bahari
  na mito.
  Wakulima wetu wako katika sehemu ambazo zaweza kutoa
  mazao haya, kama si yote walau mawili matatu au hata zaidi. Kila
  mkulima wetu aweza akaongeza mazao haya ili ajipatie chakula kingi
  zaidi au fedha nyingi zaidi. Na kwa sababu nia kubwa ya
  maendeleo ni kupata chakula zaidi na fedha zaidi kwa ajili ya
  kujipatia mahitaji yetu mengine, ndiyo kusema kuwa jitihada ya
  kuongeza mazao ni jitihada, na kwa kweli ndiyo jitihada peke yake,
  ambayo italeta maendeleo, yaani chakula zaidi na fedha zaidi kwa
  kila mwananchi.
  24
  MASHARTI YA MAENDELEO
  (a) Juhudi:
  Kila mwananchi anataka maendeleo, lakini si kila mwananchi
  anaelewa na kukubali masharti ya maendeleo. Sharti moja
  kubwa ni JUHUDI. Twendeni vijijini tuzungumze na wananchi
  kuona kama inawezekana au haiwezekani wananchi kuongeza juhudi.
  Kwa mfano, katika miji, mfanyakazi wa mshahara hufanya kazi
  kwa saa saba na nusu au nane kutwa kwa muda wa siku sita au sita
  na nusu kwa juma. Tuseme saa 45 kwa juma, kuondoa majuma
  mawili au matatu ya livu, katika mwaka mzima. Ndiyo kusema
  mfanya kazi wa mjini hufanya kazi ya saa 45 kwa juma kwa majuma
  48 au 50 kwa mwaka.
  Katika nchi kama yetu muda huu ni mdogo kwa kweli. Nchi nyingi
  hata zilizoendelea kutuzidi – hufanya kazi kwa muda mrefu zaidi
  kuliko saa 45 kwa juma. Si jambo la kawaida nchi changa kuanza na
  muda mfupi kama huo. Jambo la kawaida ni kuanza na muda mrefu
  zaidi na kuupunguza kila nchi inavyozidi kuendelea. Sisi kwa kuanza
  na muda mfupi huu na tunapodai muda mfupi zaidi kwa kweli tunaiga
  nchi zilizoendelea. Na kuiga huku kunaweza kukaleta majuto. Lakini
  hata hivyo wafanya kazi wa mishahara hufanya kazi ya saa 45 kwa
  juma; livu yao kwa mwaka haizidi majuma manne.
  25
  Yafaa kujiuliza wananchi wakulima hasa wanaume, hufanya kazi kwa
  saa ngapi kwa juma na miezi mingapi kwa mwaka. Ni wengi mno
  ambao hawatimizi hata nusu ya wastani wa mfanyakazi wa
  mshahara.
  Ukweli wenyewe ni kwamba vijijini kina mama hufanya sana kazi.
  Pengine hutimiza saa 12 au 14 kutwa. Hawana Jumapili, na hawana
  livu. Kina mama wa vijijini hufanya kazi zaidi kuliko mtu mwingine ye
  yote katika Tanzania. Lakini kina baba wa vijijini (na baadhi ya kina
  mama wa mijini) nusu ya maisha yao ni livu. Nguvu hizi za mamilioni
  ya kina baba vijijini na maelfu ya kina mama wa mijini ambazo hivi
  sasa hazifanyi kazi yo yote ila kupiga soga, kucheza ngoma na
  kunywa pombe, ni hazina kubwa yenye manufaa zaidi kwa maendeeo
  ya nchi yetu kuliko hazina za mataifa matajiri.
  Tutafanya jambo la faida kubwa kwa nchi yetu kama tukienda vijijini
  na kuwaambia wananchi kwamba wanayo hazina hii na kwamba ni
  wajibu wao kuitumia kwa faida yao wenyewe na faida ya Taifa letu.
  (b) Maarifa:
  Sharti la pili la maendeleo ni MAARIFA. Juhudi bila maarifa haiwezi
  kutoa matunda bora kama juhudi na maarifa. Kutumia jembe kubwa
  badala ya jembe dogo, kutumia jembe la kuvutwa na ng’ombe badala
  26
  ya jembe la mkono, kutumia mbolea badala ya ardhi tupu,
  kunyunyizia dawa ili kuuwa wadudu, kujua ni zao gani lifaalo
  kupandwa na zao gain lisilofaa, kuchagua mbegu vizuri kabla ya
  kuzipanda, kujua wakati mzuri wa kupanda, wakati wa kupalilia n.k.,
  ni maarifa yanayowezesha juhudi kutoa mazao mengi zaidi.
  Fedha na wakati tunaotumia kuwapa wakulima maarifa haya ni fedha
  na wakati uletao faida kubwa zaidi kwa nchi yetu kuliko fedha na
  wakati mwingi tunaotumia katika mambo mengi tunayoyaita
  maendeleo.
  Jambo hili kwa kweli tunalifahamu. Katika mpango wetu wa miaka
  mitano, mipango inayoendelea vizuri na hata kuzidi makisio ni ile
  inayotegemea juhudi ya wananchi wenyewe. Pamba, kahawa,
  korosho, tumbaku, pareto ni mazao yaliyoongezeka kwa haraka sana
  katika muda wa miaka mitatu iliyopita. Lakini ni mazao ambayo
  yameongezeka kwa sababu ya juhudi na uongozi wa wananchi, siyo
  kwa sababu ya fedha.
  Kadhalika wananchi kwa juhudi zao wenyewe na maelekezo au
  msaada kidogo wametimiza mipango mingi sana ya maendeleo huko
  vijijini. Wamejenga shule, dispensary, majumba ya maendeleo,
  wamechimba visima, mifereji ya maji, mabwawa, mabarabara,
  wamejenga mabirika ya kukoshea mifugo na kujiletea wenyewe
  27
  maendeleo ya aina mbali mbali. Kama wangengoja fedha
  wasingeyapata maendeleo hayo.
  JUHUDI NI SHINA LA MAENDELEO
  Mipango inayotegemea fedha inakwenda vizuri lakini kuna mingi
  ambayo imesimama na yumkini mingine haitatimizwa kwa sababu ya
  upungufu wa fedha. Lakini kelele zetu bado ni kelele za fedha.
  Juhudi yetu ya kutafuta fedha inazidi kuongezeka! Sio kwamba
  tuipunguze, bali, badala ya safari nyingi ndefu na zenye gharama
  kubwa za kwenda kutafuta fedha za maendeleo yetu, itafaa kufunga
  safari kwenda vijijini kuwafahamisha na kuwaongoza wananchi katika
  kujiletea maendeleo kwa juhudi yao wenyewe. Ndiyo njia ya kweli ya
  kuleta maendeleo kwa kila mtu.
  Hii maana yake si kwamba tangu sasa hatutajali fedha, wala
  hatutajenga viwanda au kufanya mipango yo yote ya maendeleo
  inayohitaji fedha. Wala siyo kusema kuwa tangu sasa hatutapokea
  wala kutafuta fedha kutoka nchi za nje kwa ajili ya maendeleo yetu.
  LA, SIVYO. Tutaendelea kutumia fedha; na mwaka hata mwaka
  tutatumia fedha nyingi zaidi kwa maendeleo yetu ya aina mbali mbali
  kuzidi mwaka uliopita. Kwani hiyo itakuwa ni dalili moja ya
  maendeleo yetu.
  28
  Lakini hii ni kusema kwamba tangu sasa tutajua nini ni shina na nini
  ni tunda la maendeleo yetu. Katika vitu viwili hivyo FEDHA na WATU,
  ni dhahiri kwamba watu na JUHUDI yao ndiyo shina la maendeleo,
  fedha ni moja ya matunda ya juhudi hiyo.
  Tangu sasa tutasimama wima na kutembea kwa miguu yetu badala
  ya kupinduka na kuwa miguu juu vichwa chini. Viwanda vitakuja, na
  fedha zitakuja, lakini msingi wake ni WANANCHI na JUHUDI yao na
  hasa katika KILIMO. Hii ndiyo maana ya kujitegemea. Kwa hiyo
  basi, mkazo wetu na uwe:-
  (a) Ardhi na Kilimo.
  (b) Wananchi.
  (c) Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na
  (d) Uongozi bora.
  (a) Ardhi:
  Kwa kuwa uchumi wa Tanzania unategemea na utaendelea
  kutegemea kilimo na mifugo, Watanzania wanaweza kuyaendesha
  maisha yao barabara bila ya kutegemea misaada kutoka nje kwa
  matumizi bora ya ardhi hiyo. Ardhi ni ufunguo wa maisha ya
  binadamu kwa hiyo Watanzania wote waitumie ardhi kama ni
  raslimali yao kwa maendeleo ya baadaye. Kwa kuwa Ardhi ni mali ya
  Taifa, Serikali ni lazima iangalie kuwa ardhi inatumiwa kwa faida ya
  29
  Taifa zima na wala isitumiwe kwa faida ya mtu binafsi au kwa watu
  wachache tu.
  Ni wajibu wa TANU kuona kuwa nchi yetu inalima chakula cha
  kutosha na kutoa mazao ambayo yataleta fedha nchini kwa kuuzwa
  katika nchi za ng’ambo. Ni wajibu wa Serikali na Vyama vya Ushirika
  kuona kuwa wananchi wanapatiwa vyombo, mafunzo ya uongozi
  unaohitajika katika kilimo na ufugaji wa kisasa.
  (b) Watu:
  Kuiwezesha siasa ya kujitegemea itekelezwe vizuri, wananchi ni budi
  wajengwe moyo na shauku ya kujitegemea. Wajitegemee katika
  kuwa na chakula cha kutosha, mavazi ya kufaa na mahali pazuri pa
  malazi.
  Katika nchi yetu kazi iwe ni kitu cha kujivunia. Bali uvivu, ulevi na
  uzururaji uwe ni jambo la aibu kwa kila mwananchi. Katika upande
  wa ulinzi wa Taifa, wananchi wawe macho na vibaraka waliomo
  nchini ambao wanaweza kutumiwa na maadui wa nje wenye nia
  mbaya ya kuliangamiza Taifa hili na wawe tayari kulilinda Taifa
  inapolazimika kufanya hivyo.
  30
  (c) Siasa Safi:
  Msingi wa siasa ya kujitegemea lazima uambatane na siasa ya
  Ujamaa ya TANU. Ili kuzuia unyonyaji ni lazima kila mtu afanye kazi
  na aishi kwa jasho lake yeye mwenyewe. Na ili kuleta usawa wa
  kugawana mapato ya nchi ni lazima kila mtu atimize wajibu wake
  kwa kufanya kazi kwa bidii zake zote. Asiweko mtu wa kwenda kwa
  ndugu yake na kukaa kwa muda mrefu bila kufanya kazi kwa sababu
  atakuwa anamnyonya yule ndugu yake. Vile vile mtu ye yote
  asiruhusiwe kuzurura zurura hovyo mijini au vijijini bila kufanya kazi
  ya kumwezesha kujitegemea mwenyewe bila kuwanyonya ndugu
  zake.
  TANU inaamini kuwa kila anayelipenda Taifa lake ni budi aweze
  kulitumikia kwa kujitolea nafsi yake na kushirikiana na wananchi
  wenzake kwa kuijenga nchi kwa manufaa ya watu wote. Ili
  kudumisha Uhuru wa nchi yetu na raia zake barabara ni budi
  kujitegemea kwa kila hali bila kwenda kuomba misaada nchi zingine.
  Kujitegemea kwa mtu mmoja ni kujitegemea kwa nyumba kumi.
  Kujitegemea kwa nyumba zote kumi za balozi ni kujitegemea kwa
  tawi zima. Kujitegemea kwa matawi ni kujitegemea kwa Wilaya
  ambayo ni kujitegemea kwa Mkoa. Kujitegemea kwa Mikoa yote ni
  kujitegemea kwa Taifa lote ambalo ndilo lengo letu.
  31
  (d) Uongozi Bora:
  TANU inatambua umuhimu wa kuwa na Uongozi Bora. Tatizo lililopo
  ni ukosefu wa mipango maalum ya kuwafundisha Viongozi na kwa
  hiyo Ofisi Kuu ya TANU ni budi itengeneze utaratibu maalum kuhusu
  mafundisho ya Viongozi tangu wa Taifa zima hadi Mabalozi ili
  waielewe siasa yetu na mipango ya uchumi. Viongozi ni lazima wawe
  mfano mzuri kwa wananchi kwa maisha yao na vitendo vyao pia.
  32
  SEHEMU YA NNE
  UANACHAMA
  Tangu Chama kilipoanzishwa, tumethamini sana kuwa na
  wanachama wengi iwezekanavyo. Hii ilifaa wakati wa kupigania vita
  vya kumng’oa mkoloni. Hivyo ndivyo ilivyobidi TANU kufanya kwa
  wakati huo. Lakini sasa Halmashauri Kuu inaona kuwa wakati
  umefika wa kutilia mkazo kwenye imani ya Chama chetu na siasa
  yake ya Ujamaa.
  Kifungu cha Katiba ya TANU kinachohusu uingizaji wa mtu kwenye
  Chama kinachohusu uingizaji wa mtu kwenye Chama kifuatwe na
  ikiwa inaonekana kuwa mtu haelekei kuwa anakubali imani,
  madhumuni na sheria na amri za Chama, basi asikubaliwe kuingia.
  Na hasa isisahauliwe kuwa TANU ni Chama cha wakulima na
  wafanyakazi.
  33
  SEHEMU YA TANO
  AZIMIO LA ARUSHA
  Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika
  Community Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka
  29/1/67, inaazimia ifuatavyo:-
  A. VIONGOZI
  1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au
  mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au
  kikabaila.
  2. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote.
  3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.
  4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi
  5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
  6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu
  ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama
  vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya
  34
  Kiserikali. Viongozi kutokana na kifungu cho chote cha
  Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye
  vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki
  kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe).
  B. SERIKALI NA VYOMBO VINGINE
  1. Inaipongeza Serikali kwa hatua zote ilizokwisha chukua
  mpaka hivi sasa katika kutimiza siasa ya Ujamaa.
  2. Inaihimiza Serikali, bila kungojea Tume ya Ujamaa, ichukue
  hatua zaidi za kutimiza siasa yetu ya Ujamaa kama
  ilivyoelezwa katika Tamko la TANU juu ya Ujamaa.
  3. Inahimiza Serikali kutengeneza mipango yake kwa
  kutegemea uwezo wa nchi hii kuiendesha mipango hiyo na
  wala isitegemee mno mikopo na misaada ya nchi za
  ng’ambo kama ilivyofanya katika mpango wa maendeleo ya
  miaka mitano. Halmashauri Kuu ya Taifa inaazimia mpango
  huo urekebishwe ili ulingane na siasa ya kujitegemea.
  4. Serikali ione kuwa mapato ya wafanyakazi nje ya Serikali
  hayapitani mno na yale ya wafanya kazi Serikalini.
  5. Serikali itilie mkazo sana njia za kuinua maisha ya wakulima.
  35
  6. Inahimiza NUTA, Vyama vya Ushirika, TAPA, UWT, TYL.,
  mashirika yote ya Serikali, kuchukua hatua ili kutekeleza
  siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
  C. UANACHAMA
  Wanachama wafundishwe kwa ukamilifu imani ya TANU ili
  waielewe, na wakumbushwe wakati wote umuhimu wa kuishika
  imani hiyo.
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145

  Pamoja na kutambua udikteta wa chama hicho sasa ni miaka 50 lakini bado mmekikumbatia kama malaika!

  Na bado hamuishi kulalamika kwamba hakijawatendea hili na lile ili mpate uungwaji mkono na watanzania wengine. Mkiambiwa hicho chama na serikali yake haviwezi kutekeleza mahitaji na matakwa yenu mnafumba macho na kujifanya vipofu!
   
Loading...