Mchele original unadunda kama kitenesi pia

T3RN3K

Member
May 30, 2011
92
125
Habari zenu wakuu, kumekuwa na uvumi wa mchele feki au mchele wa plastiki. Na moja ya njia iliyosambaa ya kugundua mchele huo ni kuudundisha. Sasa leo na mimi nkasema wacha nijaribu kudundisha wali wangu... Heh! Si ukadunda, halafu mchele wenyewe nlkuwa nimenunua super market maarufu hapa mjini. Nikaingiwa na wasiwasi, nikasema ngoja nifanye research yangu online kama kawaida yangu, coz huwa sipelekeshwi na rumors.

Kutokana na research yangu, nimegundua kuwa uvumi huu upo karibu kwenye developing countries zote duniani. Na hakuna hata nchi iliyoprove ni kweli kuna mchele feki.

Nikazama mpaka youtube nikakutana na engineer kutoka India anatolea ufafanuzi mzuri sana, kwa sababu na wao hii rumor imesambaa sana. Akatengeneza mchele wa plastic na akaenda shambani kununua mchele original.

Akagundua kwamba.
1. Mchele original unadunda pia
2. Mchele feki haushikamani wala haufinyangwi

Link ya video:
Sisemi kama hakuna mchele feki, nachosema tujaribu kupata mchele wa mashambani na dukani na tuangalie kama inadunda au la! ili tuwe na uhakika zaidi kwasababu hata jamaa anasema tunaamini sana hizi rumors kwa sababu tulikuwa hatujui kama mchele wa kawaida nao unadunda pia.

Mimi hapa mama watoto bado haamini, hataki kabsa kula wali.
 

Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,027
2,000
Nyie kuleni tu huo ubwabwa. Toka mlikotoka huko mmekula vingapi? Ukifuatilia sana mambo mengine utajikuta unaishi kwa kunywa maji tu.
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,441
2,000
Miaka yangu yote ya kulima mpunga....

Kupika wali kutokana na mchele wa kitoka shamba moja kwa moja


Sijawahi ona wali ukidunda....


Huyo jamaa wa yuutyubu anatulaghai tu

Big up to my wife wako...
 

T3RN3K

Member
May 30, 2011
92
125
Miaka yangu yote ya kulima mpunga....

Kupika wali kutokana na mchele wa kitoka shamba moja kwa moja


Sijawahi ona wali ukidunda....


Huyo jamaa wa yuutyubu anatulaghai tu

Big up to my wife wako...
Duh! Mbona mnazidi kunitisha!! Sitaki kuamini kama nimelishwa plastic mpaka na mimi niupate mpunga na niujaribu wali wake!
 

T3RN3K

Member
May 30, 2011
92
125
yote kwa yote mchele wa plastiki upo au haupo
Inavyosemekana kilo moja ya plastic ni gharama sana kuliko kilo moja ya mchele, kwahyo mtu hawezi kutengeneza mchele wa plastic halafu akauze kwa bei ya mchele wa kawaida au bei ya chini zaidi. Kwa kigezo hicho wanasema unaweza usiwepo, kama upo basi ni wa material nyingne lakini sio plastic.

Mchele wa kutengeneza pia upo, yaani artificial rice, lakini huu umetengenezwa kutoka kwenye mchele usiofaa (broken rice) na kuongezewa virutubisho zaidi. Na unaruhusiwa. Cheki hapa Artificial rice - Wikipedia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom