itagata
JF-Expert Member
- Sep 4, 2011
- 210
- 71
Ndugu wana Jamiiforums
Kwanza nianze kwa kuipongeza timu yetu ya taifa (Taifa Stars) kwa kufuzu kushiriki fainali za kombe la Mataifa ya Africa zitakazofanyika nchini Morocco. Ni hatua nzuri na ya kujivunia kuona soka la Tanzania linazidi kukua na kuonesha mwanga mwema wa mafanikio. Pia ni hatua nzuri kwa sasa serikali ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi wa viwanja vya michezo Mkoani Arusha, Dodoma na pia kuendeleza ukarabati wa kiwanja cha Benjamini Mkapa. Hii kwa njia moja ama nyingine vitaongeza chachu ya timu za mataifa mbalimbali kutumia viwanja vyetu hali itakayoongeza mapato ya nchi pia kuifanya Tanzania kujulikana zaidi kimataifa.
Pamoja na mafanikio yanayoanza kujitokeza katika sekta ya michezo mbalimbali ni wakati sasa wa serikali kuwekeza zaidi katika michezo kama chanzo cha ajira kwa vijana wetu. Kwa maoni yangu, naishauri serikali kuwekeza zaidi katika michezo mbalimbali kwa kujenga shule moja maalum ya michezo katika kila mkoa nchini. Shule hizi Pamoja na kufundisha elimu ya kawaida zijikite zaidi kwenye michezo kwa kufundisha michezo ya Mpira wa Miguu, Ukocha, Uamuzi na usimamizi wa michezo (Sports Management) kwa ujumla.
Pia shule hizi zitoe mafunzo ya michezo mingine kama Riadha, Mpira wa Mikono na hata kurusha matufe. Shule hizi zikijengwa, kila mkoa ufanye utaratibu maalum wa kutafuta vipaji vya michezo katika shule za mkoa husika na wanafunzi watakaogundulika kuwa wana vipaji basi wakusanywe kwenye hizo shule kwa lengo la kuendeleza vipaji vyao.
Katika kuboresha zaidi, yaandaliwe mashindano maalum ya shule za michezo ili kuzishindanisha na katika mashindano hayo kwa kupitia Wizara ya Michezo na Utamaduni, iwakaribishe ma-scout (Wasaka Vipaji) kutoka maeneo mbalimbali duniani watakaosaidia kuchukua vijana wetu wenye vipaji kupata ajira nje ya nchi na kuongeza pato la taifa.
Tanzania ni nchi kubwa yenye vipaji vingi ambavyo vinapaswa kulelewa toka hatua ya chini. Imekuwa ni ajabu Pamoja na ukubwa wa nchi yetu lakini tumekuwa tukipeleka wanamichezo wachache sana katika mashindano ya kimataifa wakati juhudi zikiwekezwa vizuri nchi inaweza kuwa tishio katika Nyanja ya michezo mbalimbali duniani.
Hatua hii itakwenda sanjari na juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu ya michezo nchini Pamoja na juhudi mbalimbali za wadau wa michezo kama Azam Media ambayo imewekeza zaidi kwenye michezo na kuifanya ligi yetu kuwa bora zaidi Afrika Mashariki na kati.
Kwa kutekeleza haya, nchini itaweza kuwa na Wachezaji, wataalam wa kutosha kama Waamuzi, Makocha wa Mpira Pamoja na wataalam mbalimbali wanaohusika na usimamizi wa michezo mbalimbali ambao watasimamia michezo ndani na nje ya nchi.