Serikali iitishe harambee tuimarishe reli ya Dar - Kigoma - Mwanza

Serikali iitishe harambee tuimarishe reli ya Dar - Kigoma - Mwanza

Mkuu mbona kama kuna kasi ya kufufua reli ya kati ni ndogo sana, wanakazia barabara tu sijui kwa nini - hivi tungekuwa serious tukazungumza na wachina mbona ukarabati wa reli ya kati ungechukua muda mdogo sana, kwanza ballast zinapatikana locally, sleepers zinaweza kumiminwa huko Mbeya TAZARA kiwanda cha kumimina sleepers kilijengwa siku nyingi na wachina, kitu ambacho kinge agizwa kutoka nje ni reli tu - sasa tatizo liko wapi?? Wakati mwingine nakuwa na feeling kwamba labda wafanya biashara wenye trucks za kubeba mizingo wanataka project hii isi-take off - kusua sua kumezidi ni as if Serikali haijui umuhimu wa usafirishaji kupitia njia ya reli, kama hawawezi basi wawape watu binafsi/wawekezaji.
 
hawa jamaa akili zao ziko kwenye kuiba tu na ndio maana hata maswala kama haya huwa hawayafikirii na ndio sababu ya nchi kuwa hapa tulipo.
Nalog off
 
Maendeleo ya nchi yanaletwa na wananchi, ukweli wa Tz ni wazalendo sana,tatizo hatuna leader's ndio tatizo Mwigulu Nchemba wewe unaingia humu haya mawazo uwe unampelekea mkuu wa kaya
 
Last edited by a moderator:
Mi nadhani tukutane wana jf ili tupange utekelezaji wa jambo hili wakuu then tuijulishe serikali mipango yetu.yapo mambo mengi ya namana hii tutayafanya kusaidia nji yetu./
 
Ntemi Kazwile

Naunga Mkono hoja kwa maana wakati umefika sasa wa kuwashirikisha wananchi tena kwa kuwapa hisa kwenye mashirika na Miradi, Ila cha kwanza ni kuhakikisha management za Kiswahili zina pigwa chini na Inatangazwa nafasi ya kazi na kupata Bosi au CEO ambaye ni mwajiriwa na anapewa Goals za kutimiza na kuacha kufanya haya makitu kwa siasam

Mfano mzuri wa uchangiaji ni huu wa 1000 kwa simu kila mwezi ambapo kwa Mujibu wa TRA wanakusanya si chini 18Bil kila mwezi na Kwa Mwaka hii ni zaidi ya 200Bil.

Just Imagine hela hizi zingekuwa zinakwenda moja kwa moja kwenye miradi na wannachi wana iona mfano Mahospitali, Shule za Boarding za ukweli kama za Enzi hizo.

Hila kinachofanyika sasa ni kuchukua hizi hela na kuziingiza funguu kuu ambapo wanaendelea kuzifuja na kujilipa posho.
 
Mkuu, mimi naamini kama kuna uwazi na uwajibikaji wa kutosha, kuna Watz kibao ambao wanaweza kujitoa. Sisi sote ni mashuhuda kwenye shughuli za kijamii kama arusi na misiba. Mimi nakumbuka mwanzoni mwa mwezi huu school mate wetu mmoja alifariki, ingawa mshikaji alikuwa ameshakuwa tapeli lakini huwezi kuamin kwani pesa ya kusafirishi mwili kwa ndege na kukodisha gari la kuupeleka kijiji kwao zilipatikana kwa njia ya simu ndani ya siku moja!
 
Mkuu
Mie naona ndo njia rahisi ya kuharakisha maendeleo, na kutengeneza ajira za kusaza. Maana hapo utakuwa umevuka vikwazo vya rushwa, tatizo la kuwaambia watoe kodi ya pesa kuna watu hawazi ona pesa inapitia kwake na asiibe, yani ni ugonjwa asipoiba anajisikia vibaya mno. Njia nzuri ni kuwa bypass kwa kuuza commodity-to-commodity.

Harafu hapo unakuwa na mass market, ambayo ndo kodi utapata indirectly kuzidi hata ile ambayo wangekupa directly. Yani unakuwa umeuua ndege wawili miundo mbinu unayo na bado pesa unapata.

That is true mkuu
 
harambee? are u out of ur mind??? kodi na pAYE tunazokatwa zinaenda wapi? mirahaba ya madini na utalii pesa zake ziko wapi? pesa zinazopatikana bandarini na TRA ziko wapi? kwa nn shirika la reli lisijiendeshe kifaida kuna mwenye jibu? unataka kutafuta solution rahisi?
 
Mkuu mbona kama kuna kasi ya kufufua reli ya kati ni ndogo sana, wanakazia barabara tu sijui kwa nini - hivi tungekuwa serious tukazungumza na wachina mbona ukarabati wa reli ya kati ungechukua muda mdogo sana, kwanza ballast zinapatikana locally, sleepers zinaweza kumiminwa huko Mbeya TAZARA kiwanda cha kumimina sleepers kilijengwa siku nyingi na wachina, kitu ambacho kinge agizwa kutoka nje ni reli tu - sasa tatizo liko wapi?? Wakati mwingine nakuwa na feeling kwamba labda wafanya biashara wenye trucks za kubeba mizingo wanataka project hii isi-take off - kusua sua kumezidi ni as if Serikali haijui umuhimu wa usafirishaji kupitia njia ya reli, kama hawawezi basi wawape watu binafsi/wawekezaji.
Wamiliki wa hizo 18-wheelers ndio wako against na kufufuliwa na kuimarishwa kwa reli. Walifanya kila hila ya kumng'oa waziri Nundu. Bw. Nundu alikuwa na mikakati mikubwa ya kuifufua TRC.
Bandari bila reli ni sawa na gari bila engine
 
Kufuatia mikakati ya nchi za Kenya, Uganda and Rwanda kuiengua nchi yetu kwenye mipango ya jumuia ya Afrika Mashariki nashauri yafuatayo yafanyike haraka iwezekanayo ili kuliwezesha taifa kuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo kwa haraka na kwa gharama kidogo ili kuhakikisha kuwa mizigo ya nchi marafiki kama Burundi na DRC inapitia Dar.
  • Serikali iitishe hambee ya wananchi wote ili kuchangia mfuko utakaowezesha ujenzi wa reli hii kwa haraka, kwa mfano ikiwaomba wananchi wake wachangie angalau 1,000 kila mtu ndani ya mwaka mmjo serikali inaweza kukusanya zaidi ya bil.100, mchango huu uwe wa hiari au
  • Serikali ikaribishe wananchi wake kununua hisa kwenye kampuni ya reli, hisa hizi ziuzwe kwa bei ndogo kabisa ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kushiriki, hamasa iwekwe kwa wananchi wengi zaidi kuchangia ili kuliwezesha taifa kuwa na uwezo wa kushindana kibiashara na mataifa mengine kwa kupunguza gharama za usafirishaji/uzalishaji

Naamini njia hii ni rahisi na ikitekelezwa ipasavyo itawezesha kupatikana pesa nyingi na kwa haraka bila kuliweka taifa rehani.
Isingekuwa taabu kabisa, ila kwa jinsi nchi yetu ilivyoharibika, mkakati wa namna hiyo ukiletwa utaishia kuwa ulaji wa watu fulani kama tulivyozoea...
 
Naunga mkono hoja!

KWA JINSI NILIVYO NA UCHUNGU NA USAFIRI WA RELI YA KATI,MIE NITATOA NG'OMBE WANGU MMOJA DUME!

Ila nihakikishiwe tu pesa zitakazopatikana kutokana na kuuzwa ng'ombe huyo hazitachakachuliwa!
 
🙂 🙂 Mie pia nitatoa dume moja la ng'ombe kama tulivyofanya wakati wa vita vya nduli
 
Kwa hili sitakuwa tayari mpaka pale haya yatakapofanyika: Twiga wetu 8 watakaporejeshwa nchini,pesa ya Kagoda irudishwe hazina na wahusika wahukumiwe,pesa ya Epa irudishwe hazina na wahusika wahukumiwe n.k ...baada ya hatua hizi kufanikiwa naomba kwa pamoja tuchangie harambee ya kufufua reli.
 
Back
Top Bottom