Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 309
Kufuatia mikakati ya nchi za Kenya, Uganda and Rwanda kuiengua nchi yetu kwenye mipango ya jumuia ya Afrika Mashariki nashauri yafuatayo yafanyike haraka iwezekanayo ili kuliwezesha taifa kuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo kwa haraka na kwa gharama kidogo ili kuhakikisha kuwa mizigo ya nchi marafiki kama Burundi na DRC inapitia Dar.
Naamini njia hii ni rahisi na ikitekelezwa ipasavyo itawezesha kupatikana pesa nyingi na kwa haraka bila kuliweka taifa rehani.
- Serikali iitishe hambee ya wananchi wote ili kuchangia mfuko utakaowezesha ujenzi wa reli hii kwa haraka, kwa mfano ikiwaomba wananchi wake wachangie angalau 1,000 kila mtu ndani ya mwaka mmjo serikali inaweza kukusanya zaidi ya bil.100, mchango huu uwe wa hiari au
- Serikali ikaribishe wananchi wake kununua hisa kwenye kampuni ya reli, hisa hizi ziuzwe kwa bei ndogo kabisa ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kushiriki, hamasa iwekwe kwa wananchi wengi zaidi kuchangia ili kuliwezesha taifa kuwa na uwezo wa kushindana kibiashara na mataifa mengine kwa kupunguza gharama za usafirishaji/uzalishaji
Naamini njia hii ni rahisi na ikitekelezwa ipasavyo itawezesha kupatikana pesa nyingi na kwa haraka bila kuliweka taifa rehani.