Serikali iitishe harambee tuimarishe reli ya Dar - Kigoma - Mwanza

Serikali iitishe harambee tuimarishe reli ya Dar - Kigoma - Mwanza

Kufuatia mikakati ya nchi za Kenya, Uganda and Rwanda kuiengua nchi yetu kwenye mipango ya jumuia ya Afrika Mashariki nashauri yafuatayo yafanyike haraka iwezekanayo ili kuliwezesha taifa kuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo kwa haraka na kwa gharama kidogo ili kuhakikisha kuwa mizigo ya nchi marafiki kama Burundi na DRC inapitia Dar.
  • Serikali iitishe hambee ya wananchi wote ili kuchangia mfuko utakaowezesha ujenzi wa reli hii kwa haraka, kwa mfano ikiwaomba wananchi wake wachangie angalau 1,000 kila mtu ndani ya mwaka mmjo serikali inaweza kukusanya zaidi ya bil.100, mchango huu uwe wa hiari au
  • Serikali ikaribishe wananchi wake kununua hisa kwenye kampuni ya reli, hisa hizi ziuzwe kwa bei ndogo kabisa ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kushiriki, hamasa iwekwe kwa wananchi wengi zaidi kuchangia ili kuliwezesha taifa kuwa na uwezo wa kushindana kibiashara na mataifa mengine kwa kupunguza gharama za usafirishaji/uzalishaji

Naamini njia hii ni rahisi na ikitekelezwa ipasavyo itawezesha kupatikana pesa nyingi na kwa haraka bila kuliweka taifa rehani.
ni wazo zuri lakini tatizo wenye malori watakubali? rejea kauli za Maige za kupata hela za kununua nyumba ya usd 700,000.00.
Pili cost ni ngapi? ni hiyo uliyo taja 100billion? tupo tayari kununua
 
Mimi kwa hili niko na tayari elfu kumi zipo tayari, fanyeni haraka mkuu.

Kaka kwa hili hata wakikata elfu kum na tano kwa mwezi kwa mwaka mzima kwenye mshahara wangu sitalalamika!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mkuu wazo lako ni zuri sana

Lakini nadhani kama serikali ikipata muwekezaji wa maana kutoka nje au ndani mwenye uwezo wa kuitengeneza vizuri reli ya kati basi tutafika mbali.

Yale yale ya Magufuli aliyomwambia J.K, "Nenda baba nenda. Tena ikibidi safiri kila pembe ya dunia kutembeza bakuli kwa wawekezaji."

Ccm hamtumii akili kabisa. Ndio maana kila siku viongozi wasema nchi masikini
 
Wazo zuri. Financing reli yote yenye urefu takribani km 2,000 (kumbuka reli inazunguka sana) tunaweza hitaji kama tillioni 15 hivi (Railway Finance). It is say 4 years project...
Tunaweza kugawana hivi:
  1. 40% -Government (each year 10%)
  2. 20% - International institutions/countries (EU, IMF, nchi zingine wapenda maendeleo)
  3. 15% - Organizations and companies in the country (mining, communication, banking, institutions, business entities etc)
  4. 25%- wananchi wote kwa hiari yao
 
Mkuu,
DRC kwa sasa anajenga barabara toka Sumbawanga hadi Kasanga ziwa Tanganyika,hii inamaana kwamba atakiwa anatoa mizigo Dar kupitia Mbeya-Sumbawanga then anapeleka katika bandari yake anayojenga hapo kasanga ili avushe kiurahisi kwenda DRC.
Sasa reli ya kati imeishia Mpanda mkoani Katavi,hii ina maana tukivuta reli toka Mpanda hadi Kasanga tutamkamua jamaa kwani atatumia reli Dar-tabora-mpanda-kasanga,then tutamkamua na njia ya barabara Dar-mbeya-sumbawanga-kasanga.

Inaonekana haya mambo yanawezekana basi tulianzisheni!
 
Wazo zuri. Financing reli yote yenye urefu takribani km 2,000 (kumbuka reli inazunguka sana) tunaweza hitaji kama tillioni 15 hivi (Railway Finance). It is say 4 years project...
Tunaweza kugawana hivi:
  1. 40% -Government (each year 10%)
  2. 20% - International institutions/countries (EU, IMF, nchi zingine wapenda maendeleo)
  3. 15% - Organizations and companies in the country (mining, communication, banking, institutions, business entities etc)
  4. 25%- wananchi wote kwa hiari yao

Mimi naamini hiki kitu kinawezekana kama kuna will power ya watawala na spirit is correct, wasije kuingiza kuwa ooh ccm imefanya nii, no waseme Watanzania wamewezesha hili
 
Wazo zuri. Financing reli yote yenye urefu takribani km 2,000 (kumbuka reli inazunguka sana) tunaweza hitaji kama tillioni 15 hivi (Railway Finance). It is say 4 years project...
Tunaweza kugawana hivi:
  1. 40% -Government (each year 10%)
  2. 20% - International institutions/countries (EU, IMF, nchi zingine wapenda maendeleo)
  3. 15% - Organizations and companies in the country (mining, communication, banking, institutions, business entities etc)
  4. 25%- wananchi wote kwa hiari yao
 
Harambee ya nini? wakati wana kila kitu.
Mie ningewashauri ya kwamba,
-Nzega resolute mining wape wawakezaji wachimbe miaka 10, harafu hao wawekezaji wajenge bandari kubwa za kutosha Tanga, Mtwara na Dar.

-Nyamongo mining wape wawakezaji wachimbe miaka 10, watengeneze electrical power source kwa maji/uranium utoshe kuendesha mahitaji yetu yote mhimu na usalie kuwauzia jirani kama watahitaji.

-Biharamulo mining wape wawekezaji wachimbe miaka 10, wakujengee viwanja vya ndege vya kimataifa mwanza, dar,kigoma na mbeya.
-Gas mtwara wape miaka 20, wajenge reli na train za kasi zinazotumia umeme, kutoka mtwara hadi mipakani kote huko kusini. kutoka dar mpaka mipakani mwa burundi,rwanda na congo, kutoka Tanga mpaka mpakani mwa kenya na ziwa victria.

Ukiamaliza hapo shusha bei ya mizigo za bandari kwa bei nusu ya wengine wote washindani, kwenye bandari na aiport. Ondoa ukiritimba wote, mbona hapo utanifaika sana na unaendelea kwa kasi sana na resource zako zinakuwa zimekulipa vyema ahata wakizimalizamo, utakuwa umebaki na sustainable market.

Mkuu this is an excellent idea. Maana hata kodi hatupati kwa hizo rasilimali zetu. Tungeingia nao mikataba ya aina hii kweli nchi ingefika mbali sana kimaendeleo.
 
Tatizo la Serikali ya Tanzania kwa Reli ya kati ni kubwa sana hakuna Kiongozi katika Serikali hii mwenye dhamira ya kweli ya kufanya Reli hii ifanye kazi maana karibu viongozi wote wana Kampuni zao za Usafirishaji wa Mizigo kwenda nje ya Nchi.

Kama mtakumbuka vizuri aliekuwa Waziri wa Maliasili Ndugu Ezekieli Maige,katika utetezi wake aliokuwa anautoa alipokuwa anahojiwa kuhusu mali na malori aliyokuwa ameyapata kinyume na utaratibu alisema kuwa mali zake zote alizozipata zinatokana na Biashara ya Malori ambayo huwa yanampatia Tshs 20 Mil kwa mwezi,sasa kama biashara ya malori kiasi kidogo hicho alichokuwa nacho yanampatia fedha nyingi kiasi hicho sidhani kama angekuwa na dhamira ya kweli ya kuisaidia Reli ya Kati ifanye kazi kwa ufanisi. Huo ni mfano mdogo wa Waziri mmoja je Mawaziri wengine hatujui wanamiliki Malori kiasi gani? Mimi sioni dhamira ya dhati hata kama tutachangia fedha ni kazi bure!
 
Kwa michango niliyoiona hapa kuhusu hii thread inaonesha kumbe wengi wetu ni wazalendo.....kwanini Mwakyembe asichukue proposal hii?
 
Mawazo ya walevi wanaofaidi mfumo wabkifisadi kwa jinsi wasivyokuwa na tabia y ya kurudisha mrejesho hata sent hawapati , tena wazo la kilevi kabisa hili. Upuuzi wafanye wao mie nichangie
 
Kwa michango niliyoiona hapa kuhusu hii thread inaonesha kumbe wengi wetu ni wazalendo.....kwanini Mwakyembe asichukue proposal hii?
Mwakyembe hana maamuzi binafsi, mpaka apige simu Bagamoyo ndio achukuwe hatua rejea sakata la bodi ya tpa vs mngt ya tpa na sasa maamuzi ya sumatra
 
Mkuu this is an excellent idea. Maana hata kodi hatupati kwa hizo rasilimali zetu. Tungeingia nao mikataba ya aina hii kweli nchi ingefika mbali sana kimaendeleo.

Mkuu
Mie naona ndo njia rahisi ya kuharakisha maendeleo, na kutengeneza ajira za kusaza. Maana hapo utakuwa umevuka vikwazo vya rushwa, tatizo la kuwaambia watoe kodi ya pesa kuna watu hawazi ona pesa inapitia kwake na asiibe, yani ni ugonjwa asipoiba anajisikia vibaya mno. Njia nzuri ni kuwa bypass kwa kuuza commodity-to-commodity.

Harafu hapo unakuwa na mass market, ambayo ndo kodi utapata indirectly kuzidi hata ile ambayo wangekupa directly. Yani unakuwa umeuua ndege wawili miundo mbinu unayo na bado pesa unapata.
 
Mkuu hii makitu ya wawekezaji tuachane nayo, nchi itajengwa na wananchi wenyewe. Shirika letu la reli liwe public Company ambapo wananchi wote wawe na uwezo wa kuwekeza na wahimizwe kuwekeza kama njia ya kuisaidia nchi yao.

Wazo zuri sana wawekezaji hatutaki, mimi naunga mkono hoja. Naomba mods waombe appointment kwa mkuru wapeleke hayo mawazo. Mimi nitatoa sh laki moja
 
Hao jamaa unawaacha wanaenda mpaka wanafika mwisho, wakifika mwisho we unaishusha gharama karibu nusu ya Mombasa tuone watafika wapi.
 
Hao jamaa unawaacha wanaenda mpaka wanafika mwisho, wakifika mwisho we unaishusha gharama karibu nusu ya Mombasa tuone watafika wapi.

Kagame atawaingiza mkenge sana watu wake kwa ugomvi usiokuwa na maslahi kwa taifa
 
Wazo zuri. Financing reli yote yenye urefu takribani km 2,000 (kumbuka reli inazunguka sana) tunaweza hitaji kama tillioni 15 hivi (Railway Finance). It is say 4 years project...
Tunaweza kugawana hivi:
  1. 40% -Government (each year 10%)
  2. 20% - International institutions/countries (EU, IMF, nchi zingine wapenda maendeleo)
  3. 15% - Organizations and companies in the country (mining, communication, banking, institutions, business entities etc)
  4. 25%- wananchi wote kwa hiari yao

mawazo mazuri kama haya ndo tunayoyataka hapa jf. Kwa namna hii tunaweza kuendelea kama yatafanyiwa kazi.
 
Wazo zuli sana mwenye namba ya mwakyembe mwambie asome maoni yetu mimi 20000 nitatoa hongera mtoa wazo umebuni ukweli ni kwamba kuna watu tunamaslahi ya nchi yetu selikali haijui tu
 
Back
Top Bottom