Serikali iimulike halmashauri ya Ulanga, inanyanyasa wafanyakazi

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862
Nafikisha malalamiko yangu rasmi wakuu wa serikali.

Kuanzia tarehe 04/06/2016 watendaji wengi wakiwa waalimu wa shule za msingi na sekondari walitumiwa message kuwa wakatishe likizo zao kwa ajili ya uhakiki utakaofanyika katika halmashauri kuanzia 08/06/2016, jambo hili liliwakwaza sana watendaji ambao wengi walikuwa wamesafili kwa ajili ya mapumziko baada ya kufungwa kwa shule, bila hiyana tarehe husika watendaji wengi walifanikiwa kusafili hadi Ulanga kuitikia wito na kuogopa kuitwa "wafanyakazi hewa", kituko kikawa siku ya uhakiki watendaji wa halmashauri wanadai zoezi limesogezwa hadi siku zijazo, kuuliza sababu ya kusogezwa hakuna jibu ila wanaambiwa kuwa wasiondoke, wawe karibu karibu.......

Jamani hii mbona kama kuna kutafutana, kuviziana? Naomba mamlaka husika iwasaidie hawa watendaji kwa kuwa ni haki yao kupumzika.

Kumbuka hii halmashauri ndio inayoongoza kwa kuwa na shule zinazoshika mkia, sababu kubwa ni walimu wengi wazuri kutimka kutokana na kuwepo watendaji wabovu halmashauri.

Ni hayo tu

Tume ya katiba
 
Back
Top Bottom