fredito13
JF-Expert Member
- Sep 3, 2012
- 213
- 145
Wakuu,
Nina miaka karibia 10 ya utumishi kwenye sekta binafsi. Nimefanya kwenye makampuni na NGO's kadhaa hapa nchini na kikubwa ambacho ninakiona ni Watanzania kutojua haki zetu maofisini na sheria za kazi!
Kwa kiasi kikubwa, sisi Watanzania ambao tunaajiriwa sekta binafsi, wengi ni wahanga wa kukosa elimu ya wajibu na haki zetu kama wafanyakazi!
Wawekezaji wengi wanawatumia ndugu zetu wa Kitanzania kupora haki zetu za msingi katika ajira. Kwa sababu ya ufahamu mdogo, wengi huwa tunaishia kuwa wanyonge na kukubali matakwa ya waajiri hata pale tunapoumia! Mikataba mingi huandaliwa na upande mmoja na wengine husaini bila kujua kilichoandikwa (isipokua mshahara na JD tu). Mara nyingi waajiri wanavunja mikataba yetu na kutuendesha wanavyotaka, lakini kwa sababu ya uelewa mdogo na hofu ya kukosa ajira basi tunakwenda tu.
Kuna watu wako kwenye ajira mwaka wa 2 mfululizo lakini bado wanaambiwa wao ni vibarua. Kuna watu hawapati michango yao ya Pensheni (NSSF), kuna watu wanalipwa mshahara tarehe anayoamua mwajiri na kuna wenzetu wanakubali mpaka 'kuwambwa' makofi na mabosi kwa sababu ya ajira.
Ifike wakati sasa serikali kupitia TCU, Wizara ya Elimu na taasisi zingine zinazohusika wafikirie kuifanya kozi ya Rasilimali watu (Human Resources) kuwa ni ya lazima kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu, hasa mwaka wa mwisho wa masomo yao. Kama tumeweza kuwa na Computer Course ya lazima kwa kila mwaka wa kwanza chuoni, tuifanye HR lazima kwa wanaoandaliwa kuingia soko la ajira.
Kwa kuwepo course hii, Watanzania wengi wataifahamu sheria ya Kazi na Mahusiano kazini ambayo hutoa mwongozo wa haki na wajibu wa mwajiri na mwajiriwa. Sheria hii itatusaidia kupunguza manyanyaso ofisini ambayo yanatekelezwa na waajiri kupitia 'Watanzania wenzetu'. Pia, itatusaidia kujenga uwezo wa kusimamia na kusimamiwa pasipo kupimana nguvu maofisini!
Kuna mengi yanakosekana kwenye mfumo wetu wa elimu. Lakini hili rahisi linawezekana na litatusaidia hata kwenye mapato ya serikali!
Sent using Jamii Forums mobile app