Serikali ifanye uchunguzi wa kina kuhusu ujenzi wa uwanja wa mpira wa Remela wilayani Ngara

josias

Member
Jan 7, 2014
47
34
Wakati Serikali ikichukua hatua mbalimbali kupambana na vitendo vya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za Umma kumeendelea kuibuka malalamiko kutoka kona mbalimbali za Tanzania kuhusu uwepo wa matumizi mabaya ya fedha za Umma katika baadhi ya Halmashauri.

Hivi karibuni tulishuhudia hatua zilizochukuliwa na Serikali kumsimamisha kazi na kuagizwa kukamatwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga Mkoani Tabora Ndugu Athumani Msabila kutokana na tuhuma za ubadhirifu alioufanya wakati alipokuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Pamoja na hatua hizi za Serikali bado Wananci wameendelea kulalamikia uwepo wa matumizi mabovu ya Fedha za Serikali na ujenzi wa miradi chini ya Kiwango hali inayopelekea kutoonekana kwa thamani ya Pesa.

Suala kama hili linajitokeza katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ambapo wananchi wa Wilaya ya Ngara hususani Wanamichezo wameonyesha kutoridhishwa na Ujenzi wa Uwanja wa Mpira katika eneo la Chuo cha VETA kilichopo Remela wilayani Ngara uliogharimu zaidi ya Tsh. Milion 530.

Wananchi hawa wanaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyombo vya Ulinzi na Usalama hususani Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumtafuta kokote aliko aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndugu Aidan Bahama ili ahojiwe kuhusu tuhuma mbalimbali za ubadhirifu ikiwemo Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu chini ya Kiwango ambapo Ujenzi wa Uzio na Vyoo vya Uwanja huo umetumia Tofali za Kuchoma na Udongo badala ya Cement hali iliyopelekea Kubomoka kwa Miundombinu hiyo hata kabla haijaanza kufanya kazi.

Pia Wananchi wanaitaka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kuchunguza Matumizi ya Fedha Takribani Milion 530 kwa ajili ya Ujenzi wa Uwanja wa Mpira katika Eneo la Chuo cha Ufundi Remela.

Hatua hii inakuja baada ya Wananchi kuonyesha kutoridhishwa na ubora wa Uwanja pamoja na miundombinu yake kwani Vyoo vya Uwanja huu vilititia ardhini hata kabla ya kuanza kutumika.

Lakini pia TAKUKURU inapaswa kuchunguza mchakato wa Manunuzi uliotumika kwenye Ujenzi wa Uwanja huo uliogharimu Takribani Milion 530 kwani inasadikika kuwa kwa asilimia kubwa Mafundi na vibarua waliotumika walikuwa raia wa Nchi ya Burundi na hili likidhihirisha kuwa Uwanja huu ulijengwa Kienyeji mno kutokana na ukweli kuwa hakukuwa na Kampuni iliyosimamia zabuni ya Ujenzi wa Uwanja huo hali ambayo imetengeneza mwanya wa upotevu wa fedha za mradi huu na pia kusababisha mradi huu kujengwa chini ya Kiwango.

Pamoja na kuwa Uteuzi wa Ndugu Aidan Bahama kama Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ulitenguliwa miaka takribani miwili iliyopita lakini Serikali Ina kila sababu ya Kumhoji na Kuchukia hatua kutokana na kuacha Dosari katika miradi aliyoianzisha ikiwa ni pamoja na mradi wa Uwanja wa Mpira wa Remela.

Pamoja na hayo Serikali kupitia kwa Waziri wa TAMISEMI wanapaswa kutoa majibu ya kueleweka kuhusu mpango wa Serikali katika Kukamilisha Uwanja huo ili Wana Michezo wa Wilaya ya Ngara waweze kunifaika na Uwanja huo.

Hapa Chini ninaambatanisha Picha za Uzio wa Uwanja, Vyoo vilivyobomoka na Kutitia kwenye Uwanja huo hata kabla ya Kutumika pamoja na eneo la Kuchezea (Pitch) ya Uwanja huo ili wadau mbalimbali Waweze kujionea na Kupima thamani ya Fedha.
FB_IMG_1703748234464.jpg
FB_IMG_1703748236628.jpg
FB_IMG_1703748222704.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1703748219344.jpg
    FB_IMG_1703748219344.jpg
    105.1 KB · Views: 4
Back
Top Bottom