Serikali: Idadi ya Wagonjwa wa COVID19 kwenye baadhi ya vituo yapungua

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe amesema idadi ya watu waliopata maambukizi ya Ugonjwa huo kwenye baadhi ya vituo vya matibabu imepungua na wengi wao wanaendelea vizuri

Ametaja idadi ya wagonjwa kwa siku ya leo kwa Mkoa wa Dar na Pwani katika Hospitali ya Amana kuna wagonjwa 12, Kisoka- Mloganzila 6 pamoja na Kituo cha Kibaha chenye wagonjwa 24

View attachment 1451311

Watu wanafia majumbani mwao

I will never ever believe these lunatics!
 
Mbona tuliotangaziwa sio wengi wa kutisha, hao wanaopungua kwa kasi ya kutisha wametokea wapi?
 
Jana nimemskia Katibu Mkuu Wizara ya Afya akitaja idadi ya chini kabisa ya wagonjwa katika vituo wanakotibiwa wagonjwa wa covid-19. Na alisema wote wanaendelea vizuri.

Ikiwa kama alichokuwa akikisema hakikuwa na msukumo wa kisiasa basi itoshe tu kusema kuwa kwa sasa hali ni shwari. Tumesha idhibiti corona na maisha yanaweza kurudi katika hali ya kawaida.

Nina shauri shule na vyuo vifunguliwe watoto wetu wasome. tunafahamu kuwa maradhi haya yameathiri sana nchi za Ulaya, Mashariki ya mbali na marekani. na pia tunafahamu huko ndiko wanakosoma watoto wa wanasiasa wengi.

Hao watoto wenu wanaweza tu kuendelea maisha yarudi kawaida huko uingereza au italia sisi wa kwetu hawa wanaosoma tosamaganga high school au st john university pale buguruni na mjimwema primary school kule kigamboni fanyeni utaratibu warudi shule.

Hatuoni tena sababu ya kuwa na hofu juu ya corona tena labda kama mnapiga siasa kuhusu taarifa mnazotoa kumfurahisha aliejificha.
 
Ummy Mwalimu nimemwelewa sana ktk janga hili. Hakuna waziri aliyekuwa mstari kutuongoza vema ktk mapambano haya Kama Ummy.

Hakulala kila wakati nilimwona akisaka wagonjwa au wenye dalili popote kusudi Ugonjwa usienee lkn kupitia hotuba za mabosi itakuwa aligundua kitu cha hatari sana.

Itakuwa alihisi anapambana na Corona na team ya watu wanaodhani wanapambana Ugonjwa wa Upele. Katulia kimyaaa anausoma mchezo kwa mbaaali huku akisubiri maagizo tu ya team Upele yatolewe atekeleze
 
Tuko vizuri,ingawa najua watu wengine bado watabeza...

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapo waliokua wamejipanga kulitumia hili janga kisiasa lakini wanafeli kadri siku zinavyozidi kwenda.

Nililojifunza kubwa kutoka kwa JPM kwenye hili ni kuwa na utulivu wa maamuzi kwenye kila situation no matter how bigger it may appear.
 
Mkuu deal done. Kama ambavyo Spanish influenza ilivyowakamata vilivyo ndugu zetu hata korona ni yao pia.. Malaria yetu, AIDS yetu, nasema hivi kila MTU ashinde mechi zake.
 
Ummy Mwalimu nimemwelewa sana ktk janga hili. Hakuna waziri aliyekuwa mstari kutuongoza vema ktk mapambano haya Kama Ummy. Hakulala kila wakati nilimwona akisaka wagonjwa au wenye dalili popote kusudi Ugonjwa usienee lkn kupitia hotuba za mabosi itakuwa aligundua kitu cha hatari sana. Itakuwa alihisi anapambana na Corona na team ya watu wanaodhani wanapambana Ugonjwa wa Upele. Katulia kimyaaa anausoma mchezo kwa mbaaali huku akisubiri maagizo tu ya team Upele yatolewe atekeleze
jana alisherehesha siku ya familia vizuri sana kwa hotuba nzuri. yupo vizuri kwenye ku deliver speech. anapiga sarufi hatari haruki mkato wala nukta.
 
Mimi nilishauri mwezi wa sita mwanzoni kwa tahadhari na mpangilio madarasa ya mitihani yahudhurie shule yaani darasa la nne, la saba, kidato cha pili NNE na sita kwanza na walimu woote washambulie kuwafundisha ili kupunguza msongamano! Baadae waliobaki wajiunge kadri maisha yatakavyokuwa yanarudi sawa.
 
Wazazi wengi watasita kupeleka watoto wao shule kwa wiki za karibuni hofu bado ipo MTAANI huko tz labda wiki hii waanze kutaja takwimu zinazoshuka ili kuwaandaa wazazi kisaikolojia kwamba kwasasa Mambo ni shwari.
 
jana alisherehesha siku ya familia vizuri sana kwa hotuba nzuri. yupo vizuri kwenye ku deliver speech. anapiga sarufi hatari haruki mkato wala nukta.
Sista anajua na tena hana Ile tabia ya kutajataja watu wanaodhani wanamiliki roho za watanzania. Yani Kuna majitu likipigiwa au likiiba kura linadhani limechaguliwa kuongoza roho za watu halafu lenyewe ndio Limungu lenye mbingu na enzi. Ummy hana hizo na anaheshima sana
 
Kauli Kama hizi wakati mashine ilipigwa stop. Hao waliopungua Ni wale waligundulika wiki mbili zilizopita ?
FB_IMG_15896022464411290.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nawaona vile WHO na AU namna walivyo vurugwa na hizi siasa zetu za kuto kutoa taarifa za wazi na zisizo na shaka kuhusu Corona! 😟

Hata hawajui cha kutufanya! Ila ni kweli, shule na vyuo vifunguliwe tu. Sasa kama hiyo Corona haipo, iweje mpaka leo hakuna hata taarifa za awali ni lini vijana wetu watarudi masomoni?
 
Back
Top Bottom