Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Suala lako ni hypothetical na unajiuliza kama kweli ulifanya uchunguzi huo kweli au ulitaka tu kutimiza wajibu wako wa kila siku wa kumsifia Mwalimu na wakati huo huo kuendeleza programu yako ya chuku dhidi ya mtawala wa leo. Umekuwa ukisikia kila siku kwamba kuna mahindi huko Rombo na hata huko Rukwa yakivushwa kwenda nje kwa sababu kuna ziada katika sehemu hizo. Tunajua pia kwamba SGR ina chakula cha kutosha na sasa kinatolewa kupunguza nakisi katika maeneo ambayo hayakuwa na mavuno mazuri. Hali unayozungumzia wewe si ya Tanzania (labda kwa sababu mwenzetu uko nje) ya leo. Sasa kujaribu kuonyesha kwamba 70% ya watanzania wanakabiliwa na njaa ni upotoshaji wa hali ya juu na hata inakinzana na maelezo yako mwenyewe kwa kusema kwamba nusu ya wilaya zote zinakabiliwa na njaa. That is not 70%.
Lakini mimi sitashangaa kusikia hii scare inatolewa na mtu ambaye inawezekana ana zaidi ya muongo mmoja hajaja nchini na anategemea kusoma magazeti online. Halafu kusifia njaa tuliyokuwa nayo wakati wa mwalimu sijui kuna mantiki gani maana hata kama ilitokea wakati wa mwalimu, hakikuwa kitu cha kujivunia hata kidogo.
Sasa kujaribu kuonyesha kwamba 70% ya watanzania wanakabiliwa na njaa ni upotoshaji wa hali ya juu na hata inakinzana na maelezo yako mwenyewe kwa kusema kwamba nusu ya wilaya zote zinakabiliwa na njaa. That is not 70%.
Nalo Gazeti la Nipashe la Jana linadokeza hivi (kama ni uongo serikali inaweza kutoa ufafanuzi):
Mikoa 16 (sawa na asilimia 76) ya nchi inakabiliwa na njaa na inahitaji msaada wa chakula cha dharura. Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe, aliliambia Bunge jana kwamba, kutokana na hali hiyo, serikali imefuta vibali vyote vya kusafirisha mazao ya chakula nje ya nchi kuanzia Julai mosi, mwaka huu.
Maghembe alisema serikali pia imepiga marufuku uuzaji wa mazao ya chakula nje ya nchi kwa kipindi cha miezi sita, kuanzia Julai Mosi hadi Desemba 31, mwaka huu.
"Madhumuni ya hatua hizi ni pamoja na kuipa serikali nafasi ya kufuatilia mwenendo mzima wa upatikanaji wa chakula nchini kwa lengo la kujihakikishia usalama wetu wa chakula katika kipindi hicho na baada ya hapo," alisema.
Alifafanua kwamba pamoja na tatizo la njaa linaloikabili sehemu kubwa ya nchi, baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakiwarubuni wakulima na kununua mazao yao moja kwa moja yakiwa shambani, jambo linalowanyonya wakulima.
Alisema ili kukomesha unyonyaji huo, serikali inakusudia kujenga masoko na maghala ya chakula katika maeneo mengi ili kuwawezesha wakulima kutumia utaratibu wa stakabadhi ghalani kuuza mazao yao.
Maghembe alikiri kwamba lipo tatizo la mazao ya chakula kusafirishwa kwa njia za magendo kwenda nje ya nchi, lakini alisema biashara hiyo inafanywa kwa vibali vya kughushi.
Aiitaja mikoa inayokabiliwa na njaa na idadi ya wilaya zake kwenye mabano kuwa ni Arusha (7), Dar es Salaam (3), Dodoma (1), Iringa (2), Kagera (2), Kilimanjaro (5), Manyara (2), Mara (4), Mbeya (1), Mtwara (1), Mwanza (5) na Pwani (2).
Mngine ni Shinyanga (7), Singida (2), Tabora (3) na Tanga (1). Hata hivyo, alisema wilaya 56 zinakabiliwa na hali tete ya ukosefu wa chakula.
Alisema kutokana na hali hiyo, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), inahamisha tani 115,000 za chakula cha ziada kilichopo kwenye maghala yake ya Sumbawanga, Makambako na Songea kwenda kwenye maeneo yanayokabiliwa na njaa katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Shinyanga.
"Hatua hii itawezesha serikali kukabiliana na upungufu wa chakula na mahitaji mengine ya soko kwa haraka zaidi serikali inawahimiza wakulima wajiwekee akiba ya chakula katika msimu huu kwa ajili ya mahitaji ya kaya zao mpaka msimu ujao," alisema.
Waziri Maghembe alisema hali ya uzalishaji wa chakula nchini msimu wa mwaka 2010/11 haikuridhisha kwa kuwa kuna upungufu wa tani 413,740 za chakula.
Alisema chakula kinachovunwa sasa kinatazamiwa kuwa tani 6,786,600 wakati mahitaji ni tani 7,200,340.
CHANZO: NIPASHE
Mbopo,
Usijaribu kufanya swala la njaa kuwa la ki-Chama... Utakuwa unafanya DHAMBI kubwa sana! Ni ukweli usiofichika kuwa takribani asilimia 80 ya wananchi wa Tanzania wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula .. Siyo SIRI! Swala la msingi ni kwamba LAZIMA serikali ijipange vizuri kukabiliana na tatizo hili..
Hii attempt ya kuzuia nafaka kuuzwa nje ya nchi siyo suluhisho - Bali - Serikali inunue hizo nafaka kwa BEI ya SOKO!
Mkuu nakupinga kwa hili la kusema SGR wana chakula cha kutosha....katika kipindi kifupi kilichopita tulimsikia Rais katika hutuba yake akisema SGR ambayo sasa ni NFRA watatoa hifadhi yao sokoni ili kupunguza bei ya vyakula. Cha ajabu watendaji wake wakaanza kujigaia huku wakisikika katika vyombo vya habari kuwa ugawaji huo wa nafaka utahusisha wafanyabiashara wadogo tu. Cha ajabu wafanyabiashara wadogo hao walichonunua toka NFRA ni tani 600 huku karibu tani 20,000 wakijipatia wao kupitia kwa wafanyabiashara wakubwa na hayohayo mahindi waliojigawia ndiyo yaliyokamatwa Rombo na baadhi ya magunia yakiwa na chapa ya NFRA..sasa kwa hili huwezi sema eti Rombo kuna ziada ya chakula.Suala lako ni hypothetical na unajiuliza kama kweli ulifanya uchunguzi huo kweli au ulitaka tu kutimiza wajibu wako wa kila siku wa kumsifia Mwalimu na wakati huo huo kuendeleza programu yako ya chuku dhidi ya mtawala wa leo. Umekuwa ukisikia kila siku kwamba kuna mahindi huko Rombo na hata huko Rukwa yakivushwa kwenda nje kwa sababu kuna ziada katika sehemu hizo. Tunajua pia kwamba SGR ina chakula cha kutosha na sasa kinatolewa kupunguza nakisi katika maeneo ambayo hayakuwa na mavuno mazuri. Hali unayozungumzia wewe si ya Tanzania (labda kwa sababu mwenzetu uko nje) ya leo. Sasa kujaribu kuonyesha kwamba 70% ya watanzania wanakabiliwa na njaa ni upotoshaji wa hali ya juu na hata inakinzana na maelezo yako mwenyewe kwa kusema kwamba nusu ya wilaya zote zinakabiliwa na njaa. That is not 70%.
Lakini mimi sitashangaa kusikia hii scare inatolewa na mtu ambaye inawezekana ana zaidi ya muongo mmoja hajaja nchini na anategemea kusoma magazeti online. Halafu kusifia njaa tuliyokuwa nayo wakati wa mwalimu sijui kuna mantiki gani maana hata kama ilitokea wakati wa mwalimu, hakikuwa kitu cha kujivunia hata kidogo.
Mkuu SGR unayoitaja je unajua kwa sasa wana akiba kiasi gani?? fatilia hilo kwanza ndipo uanze kufikiria hayo unayoyasema.Sijui unamaanisha chama gani maana mimi si mwanachama wa CCM na wala sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Tunachokubaliana wote hapa ni kwamba tatizo la upungufu wa chakula ni la kweli na lina ukubwa wake. Serikali imekiri hilo, sanjari na kueleza mikakati ya namna ya kukabiliana na tatizo hilo, mojawapo ikiwa ni kuachia shehena kutoka SGR kwenda kwenye maeneo yenye matatizo. lakini ni lazima tukubali pia kwamba tukiachia watu waendelee na kasi hii ya kuhamisha chakula, watu hawa watamaliza hata akiba zao na baadae kulalamika na kuomba msaada. Sasa suala la serikali kununua ziada yote nalo ni gumu kwa sababu za kibajeti na za kimahitaji. Hata hivyo, wakati tunakubali kwamba hali hii ni mbaya, tusiwe na negativity iliyopitiliza kiasi cha kutoa insinuations za kwamba kutakuwa na mgawo wa chakula na pale utakapotokea basi serikali haitatenda haki!
Swala la njaa ni la kila mtu,iweje ianze Dar?