Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,403
- 31,379
Kuna mambo manne nayaona. Kwanza ni kweli kabisa kuna mbadiliko ya hali ya dunia na ukame unakuwa ni janga. Bahati nzuri katika nchi yetu tuna mito mikubwa ambayo inaathirika kutokana na tributaries kukauka lakini haikauki kabisa. Kwa wenzetu wenye irrigation scheme huweka reservoir kukabiliana na hali kama hiyo, sisi hatujafikiria hilo kama waziri mkuu Pinda alivyokiri mbele ya ugeni wa India. Si sahihi kufikiri mkulima au wakulima wanauwezo wa kujenga reservoir hasa wa kilimo chetu cha mkono.
Pili, ni kweli pia wananchi wanatakiwa wabuni mbinu za umwagiliaji. Mimi nimezaliwa katika maeneo ambayo kilimo cha umwagiliaji kilianza miaka 150 iliyopita na kina jina la asili,mifereji hiyo ipo na mingine imwekewa miiko(kulinda). Utashangaa siku hizi watu wamebomoa mifereji hiyo na eneo letu linaathirika kama maeneo mengine.
Yapo maeneo yasiyohitaji pump bali utaratibu wa mifereji kwani maji yaliyopo yanatiririka. Ukienda maeneo hayo utamaduni umetoweka, vijana wenye nguvu wametimkia mjini na wazee waliopo wanaishi ili siku ipite. Kilimo cha namna hii hakiwezi kukabiliana na njaa.
Tatu, serikali ina mkono pia kwasababu mkulima wa nyanya pale kipera na mlali morogoro anauza tenga lake kwa sh 2500. Sasa huyu mtu mpaka akusanye 300,000 za kununua pump sijui maisha yanamsubiri huku kukiwa na mlo, ada n.k. Endapo angepata bei nzuri nina hakika angeongeza uzalishaji na kwa njia hiyo uzalishaji wa mazao muhimu kama yanafaka ungezalisha ziada na kukidhi mahitaji ya nchi. Kuna atakayesema aende bank, lakini je kuna bank itampa mtu mkopo asiye na hata akaunti? Serikali inatakiwa ijenge mazingira ya kumwezesha mkulima kwa bei na upatikanaji wa mitaji. Ulaya na marekani wanafanya hivyo ndio maana mkulima ana insurance, nikimaanisha serikali zao hazikuwaacha tu bali ziawajengea mazingira mazuri. Ireland ilipiga marufuku uingizaji wa mayai ili kumjengea mkulima mazingira mazuri ya bei.
Nne, mwaka jana december kuna mbunge amelalamika kuwa watu wa sumbawanga waruhusiwe kuuza mazao nje. Ni sawa kwasababu wanamahijtaji kama watu wengine. Kama serikali ingenunua chakula kile na kukihifadhi badala ya kuachia kiende nje, huenda leo tungekuwa na ziada ya kuuza kwa bei nzuri Kenya na Somalia. Sioni mantiki ya kuacha chakula kiuzwe nje halafu tuagize kwa pesa za kigeni. Sijui kama SGR yetu ina ukubwa wa kiasi gani kitaifa lakini upo umuhimu wa kuangalia suala la hifadhi. Wakati wa miaka ya 1980.... tuliwahi kuletewa mchele kutoka Japan na Korea. Ulikuwa sio mzuri na maelezo yalikuwa ni chakula cha msaada kwani wanasafisha maghala na mchele huo ulikuwa wa miaka 10.
Sisi tunashindwaje kuhifadhi chakula hata kama hali ya hewa ni nzuri miaka 2 tu?
Taarifa za mashirika ya kimataifa zinaonyesha kuna balaa la njaa East Africa hasa Kenya na Somalia. Historia inaonyesha kuwa kunapokuwa na matatizo kama hayo kwa jirani zetu sisi huwa ni waathirika kutokana na mahitaji yanayochochewa na bei. Kwa vile tuna upungufu katika mikoa mingi ukichanganya na ukosefu kwa majirani sina uhakika tupo salama.
Kama alivosema mmoja wetu, je 'stress test' inatupa jibu gani? Tutakapobaini kuna tatizo na kuanza kusubiri meli zitoke Japan au Korea, tunaweza kupoteza watu. Na historia ni shahidi wa kweli kuwa hatujaweza kuwa tayari kukabiliana na majanga.
Kenya na Uganda mambo si mazuri, tuna uhakika tupo salama!!!! endapo tupo salama tumshukuru mwenyezi, vinginevyo tunapaswa kujiandaa.