Serikali ianze mpango wa Mgao wa Chakula na ianze na Dar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ianze mpango wa Mgao wa Chakula na ianze na Dar?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 8, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Robo tatu ya Tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula. Kuna watu wanakabiliwa na njaa katika nusu ya wilaya zote nchini na hali haionekani kutengemaa sasa hivi. Serikali inajitahidi kuhamisha nafaka kutoka sehemu mbalimbali zenye chakula kupeleka kwenye sehemu zenye upungufu wa chakula. Kwenye soko la dunia nchi nyingi zaidi zinazidi kugombea chakula kidogo kilichopo na kama kawaida mataifa makubwa yatakuwa na uwezo wa kupata vyakula vingi kuliko nchi maskini.

  Kwa vile chakula ni limited resources ni wazi kuwa itahitajika uamuzi wa makusudi wa kuanza kufikiria jinsi ya kuration chakula aidha kwa mikoa, wilaya na hata kwa kaya. Japo kuration chakula kwa kaya ni uamuzi wa mwisho kabisa wa hali ngumu ya njaa yawezekana kuanza kuration chakula kwenda kwenye miji mikubwa na hasa kupunguza vyakula vya anasa katika miji hiyo hasa vitu kama nyama, mchele na baadhi ya matunda. Hii yote ni katika kuhakikisha kuwa hakuna sehemu ya Tanzania ambayo inakabiliwa na uhaba kupita kiasi. Wasiwepo watu wanaoishi katika anasa ya kula na kusaza katika taifa la watu wengine ambao hawajui watakula nini.

  Kama ilivyokuwa wakati wa Mwalimu ambapo matajiri na maskini waligawana njaa ili kuhakikisha watu wote wanapata vyakula vya msingi yawezekana uamuzi kama huo tusipoangalia unaweza kuchkuliwa tena. Je, wale walioshiba watakuwa tayari kula pungufu ya wanavyokula sasa? Je, mashule ya boarding yanaweza kuhitaji kufungwa kwa ajili ya upungufu wa chakula (hii ikiwa ni pamoja na vyuo)? Je, italazimika kupiga marufuku baadhi ya sherehe na mikutano ambayo ambayo inatumia vyakula vingi kama starehe?

  Je suala hili la mgao lianze na Jiji la Dar mahali ambapo watu wachache hata wanajua kuwa sehemu nyingine Tanzania kuna uhaba wa njaa? Jibu langu ni ndio. Nimekuwa nikifuatilia suala hili kwa miaka mitatu na naweza kusema kwa uhakika mkubwa tu, hakuna kitu kinachoweza kusababisha migongano ya kisiasa na kijamii kama hili suala la chakula. Wakati wa Nyerere japo kulikuwa na nidhamu ya watu kujali kuwa sote tuko pamoja katika hili; je chini ya viongozi wetu hawa Watanzania watakuwa pamoja kukubali kushare kidogo au Ufisadi ndio utajionesha kustahili kwake zaidi kuliko watu wengine?

  nawaza tu.
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Suala lako ni hypothetical na unajiuliza kama kweli ulifanya uchunguzi huo kweli au ulitaka tu kutimiza wajibu wako wa kila siku wa kumsifia Mwalimu na wakati huo huo kuendeleza programu yako ya chuku dhidi ya mtawala wa leo. Umekuwa ukisikia kila siku kwamba kuna mahindi huko Rombo na hata huko Rukwa yakivushwa kwenda nje kwa sababu kuna ziada katika sehemu hizo. Tunajua pia kwamba SGR ina chakula cha kutosha na sasa kinatolewa kupunguza nakisi katika maeneo ambayo hayakuwa na mavuno mazuri. Hali unayozungumzia wewe si ya Tanzania (labda kwa sababu mwenzetu uko nje) ya leo. Sasa kujaribu kuonyesha kwamba 70% ya watanzania wanakabiliwa na njaa ni upotoshaji wa hali ya juu na hata inakinzana na maelezo yako mwenyewe kwa kusema kwamba nusu ya wilaya zote zinakabiliwa na njaa. That is not 70%.

  Lakini mimi sitashangaa kusikia hii scare inatolewa na mtu ambaye inawezekana ana zaidi ya muongo mmoja hajaja nchini na anategemea kusoma magazeti online. Halafu kusifia njaa tuliyokuwa nayo wakati wa mwalimu sijui kuna mantiki gani maana hata kama ilitokea wakati wa mwalimu, hakikuwa kitu cha kujivunia hata kidogo.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Aah nimekuelewa; kilichopo ni nakisi tu chakula so bada bing bada bong mnahamisha chakula toka upande huu na kwenda kule mambo yamekwisha? Hakuna tatizo la njaa, kuna tatizo tu la upungufu wa chakula hapa na pale ambao utaondolewa kwa kuhamisha chakula toka upande huu kwenda kule. Well if that is the case.. good. Wala usijali nilichosema kwani ni njozi tu na scare tactic.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Gazeti lenu la Serikali Habari Leo limeandika hivi katika Tahariri yake ya leo

  SERIKALI kupitia Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe, imetangaza upungufu wa chakula nchini na kutoa hadhari kwa wananchi kuhusu hali hiyo na pia kuzuia uuzaji nje wa chakula mara moja.

  Waziri alisema bungeni Dodoma juzi kwamba kuna upungufu wa tani 413,740 za chakula kinachotokana na nafaka na tayari wilaya 56 ziko hatarini kukumbwa na njaa kama hatua madhubuti hazitachukuliwa kuzinusuru.

  Ni jambo jema, kwamba Serikali imeliona hilo na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na hiyo ya kuzuia vibali vya kusafirisha chakula nje ya nchi ambavyo katika maeneo mengine vilikuwa vikitumiwa vibaya.

  Chakula kimekuwa kikisafirishwa nje ya mipaka ya nchi yetu hasa kwa kuzingatia kuwapo na hali ya ukame katika nchi za Pembe ya Afrika na hivyo kuhitaji chakula kwa wingi na kusababisha wakulima wetu kuvutwa na biashara hiyo ya chakula.

  Imekuwa ni kawaida kwa wakulima kuuza chakula na kusahau kujiwekea akiba kutokana na kuhitaji zaidi fedha ambazo siku hizi ndizo zimekuwa jibu la kila kitu si mijini tu bali hata vijijini.

  Pamoja na Serikali kuwahakikishia wananchi kwamba nchi ina akiba ya ziada ya mazao yasiyo nafaka kwa maana ya viazi, muhogo, ndizi na vinginevyo, kiasi cha tani milioni 1.7, lakini chakula kikuu cha Watanzania wengi ni nafaka.

  Licha ya kwamba marufuku ya kuuza chakula nje imeanzia Julai mosi na inatarajiwa kukoma Desemba 31, upo umuhimu wa agizo hili kutekelezwa kivitendo kwa dhati ili kuhakikisha kwamba hakuna Mtanzania anakufa kwa njaa.

  Tunasema hivyo kwa sababu tulishazoea kusikia maagizo, maonyo na hata marufuku kama hizi zikitolewa, lakini mambo yanajiendea kama kawaida kana kwamba hakuna mtu anayewajibika kuyasimamia.

  Safari hii Watanzania hatupaswi kucheza na hali ilivyo kuhusu chakula, kwa sababu katika baadhi ya nchi jirani, hali imeshakuwa mbaya na watu wanakabiliwa na utapiamlo mkali kutokana na njaa iliyosababishwa na ukame.

  Tusipokuwa makini na hili, tukaacha kuwasikiliza viongozi wetu, kwa kuingiza masuala ya siasa na itikadi, tutajikuta katika hali mbaya na siasa isitusaidie chochote, zaidi ya kuchekwa na watakaokuwa na chakula.

  Si siri kwamba wananchi wana njia na mbinu nyingi za kuvusha chakula na kukiuza nje ya nchi, lakini hapa tunapaswa kuelekeza nguvu zetu zote katika kuzuia biashara hiyo, tusije tukatumbukiwa nyongo.

  Hakuna asiyefahamu kuwa mtu mwenye njaa hana uwezo wa kufikiria chochote na hata wa kuzalisha chochote hivyo tukicheza muda huu, tutajikuta tunaangaliana na njaa yetu na hakuna atakayeweza kuzalisha mali na matokeo yake tutakufa njaa kama si kusubiri misaada ya kigeni ambayo haitatutosheleza.

  Hivyo basi watakaokaidi amri hii ya Serikali na kuendelea kutoa vibali haramu au kuvusha chakula nje ya mipaka, hatua kali ichukuliwe bila kuoneana aibu wala kuogopa lawama, kwani bora hiyo kuliko fedheha.

  My Take:
  Aidha hili gazeti linasema kweli au linasema uongo. Kwamba tatizo ni baya sana au ni kijitatizo kidogo tu ambako hakatishii maisha ya watu wetu. Tukikubali anachosema Mbopo ina maana suluhisho ni kuhamisha chakula huku na kule tu.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nalo Gazeti la Nipashe la Jana linadokeza hivi (kama ni uongo serikali inaweza kutoa ufafanuzi):

  Mikoa 16 (sawa na asilimia 76) ya nchi inakabiliwa na njaa na inahitaji msaada wa chakula cha dharura. Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe, aliliambia Bunge jana kwamba, kutokana na hali hiyo, serikali imefuta vibali vyote vya kusafirisha mazao ya chakula nje ya nchi kuanzia Julai mosi, mwaka huu.
  Maghembe alisema serikali pia imepiga marufuku uuzaji wa mazao ya chakula nje ya nchi kwa kipindi cha miezi sita, kuanzia Julai Mosi hadi Desemba 31, mwaka huu.
  "Madhumuni ya hatua hizi ni pamoja na kuipa serikali nafasi ya kufuatilia mwenendo mzima wa upatikanaji wa chakula nchini kwa lengo la kujihakikishia usalama wetu wa chakula katika kipindi hicho na baada ya hapo," alisema.
  Alifafanua kwamba pamoja na tatizo la njaa linaloikabili sehemu kubwa ya nchi, baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakiwarubuni wakulima na kununua mazao yao moja kwa moja yakiwa shambani, jambo linalowanyonya wakulima.
  Alisema ili kukomesha unyonyaji huo, serikali inakusudia kujenga masoko na maghala ya chakula katika maeneo mengi ili kuwawezesha wakulima kutumia utaratibu wa stakabadhi ghalani kuuza mazao yao.
  Maghembe alikiri kwamba lipo tatizo la mazao ya chakula kusafirishwa kwa njia za magendo kwenda nje ya nchi, lakini alisema biashara hiyo inafanywa kwa vibali vya kughushi.
  Aiitaja mikoa inayokabiliwa na njaa na idadi ya wilaya zake kwenye mabano kuwa ni Arusha (7), Dar es Salaam (3), Dodoma (1), Iringa (2), Kagera (2), Kilimanjaro (5), Manyara (2), Mara (4), Mbeya (1), Mtwara (1), Mwanza (5) na Pwani (2).
  Mngine ni Shinyanga (7), Singida (2), Tabora (3) na Tanga (1). Hata hivyo, alisema wilaya 56 zinakabiliwa na hali tete ya ukosefu wa chakula.
  Alisema kutokana na hali hiyo, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), inahamisha tani 115,000 za chakula cha ziada kilichopo kwenye maghala yake ya Sumbawanga, Makambako na Songea kwenda kwenye maeneo yanayokabiliwa na njaa katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Shinyanga.
  "Hatua hii itawezesha serikali kukabiliana na upungufu wa chakula na mahitaji mengine ya soko kwa haraka zaidi…serikali inawahimiza wakulima wajiwekee akiba ya chakula katika msimu huu kwa ajili ya mahitaji ya kaya zao mpaka msimu ujao," alisema.
  Waziri Maghembe alisema hali ya uzalishaji wa chakula nchini msimu wa mwaka 2010/11 haikuridhisha kwa kuwa kuna upungufu wa tani 413,740 za chakula.
  Alisema chakula kinachovunwa sasa kinatazamiwa kuwa tani 6,786,600 wakati mahitaji ni tani 7,200,340.
  CHANZO: NIPASHE
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mi naona kitu muhimu ni kurahisisha njia ya usafirishaji wa chakula kutoka mahali kilipo na kukipeleka sehemu ambayo wanashida ili kupunguza ulanguzi kama sasa hv ukienda magengeni unaambiwa pilipili moja tsh 50 yaan maeneo ya mjni hali ni mbya sana
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Swala la njaa ni la kila mtu,iweje ianze Dar?
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwenye red: Test results za hypothesis zinasemaje? Kuna njaa Tanzania? Asilimia ngapi iko within your description ya njaa?
   
 9. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,126
  Likes Received: 6,611
  Trophy Points: 280
  Mi naona dar walau watu wanaweza kuchakarika wakala, vijijini huko loo MUNGU wangu sijui hata niseme nini, ukisikia njaa ni njaa kweli kweli ati.
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mbopo,

  Usijaribu kufanya swala la njaa kuwa la ki-Chama... Utakuwa unafanya DHAMBI kubwa sana! Ni ukweli usiofichika kuwa takribani asilimia 80 ya wananchi wa Tanzania wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula .. Siyo SIRI! Swala la msingi ni kwamba LAZIMA serikali ijipange vizuri kukabiliana na tatizo hili..

  Hii attempt ya kuzuia nafaka kuuzwa nje ya nchi siyo suluhisho - Bali - Serikali inunue hizo nafaka kwa BEI ya SOKO!
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Nashukuru kwamba umekiri kwamba namna ulivyolieleza tatizo wewe (katika namna ya kutisha na kuogopesha) haikuwa sahihi kwa sababu upungufu wa chakula umekuwa ukijitokeza kila mara na hiyo ndiyo sababu ya kuwepo kwa SGR. Hali hii ni tofauti sana na nchi ambazo zinakabiliwa na tatizo hilo ambazo zimelazimika hata kuagiza GMO kutoka nje na hata kununua mahindi na nafaka nyingine kutoka nchi jirani. Kwa kuambua kwamba kilimo chetu bado kinategemea mvua na zana duni, na, kwa kutambua kwamba mvua zimekuwa zikinyesha kwa upungufu mkubwa, tatizo la upungufu wa chakula hasa kwa maeneo makame kama Shinyanga, Arusha, Manyara, Dodoma na baadhi ya maeneo ya Singida ni hali inayojitokeza kila mwaka, hata pale nchi inapokuwa imepata bumper harvest. Unapoitaja Dar es Salaam ambayo kwa kiasi kikubwa wananchi wake si wakulima, mimi inanipa shida kuielewa. Kwa kutaja mikoa 16 haimaanishi kwamba wilaya na maeneo yote wilayani humo au mkoani humo kuna njaa. Mimi nafikiri Serikali imetoa tahadhari hiyo kama namna moja wapo ya kulikabili tatizo hili ambalo limesababishwa na ukame uliopitiliza hasa katika pembe ya Afrika. Lakini waziri amethibitisha unachokikata kwamba kuna tishio hilo lakini siyo katika namna hiyo unayoieleza: kwamba kutakuwa na rationing kama ya wakati wa Mwalimu na kuonyesha kwamba sasa hivi hakutakuwa na mgawo wa haki! Sababu? Kikwete!!!!! Very unfortunate.
   
 12. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sijui unamaanisha chama gani maana mimi si mwanachama wa CCM na wala sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Tunachokubaliana wote hapa ni kwamba tatizo la upungufu wa chakula ni la kweli na lina ukubwa wake. Serikali imekiri hilo, sanjari na kueleza mikakati ya namna ya kukabiliana na tatizo hilo, mojawapo ikiwa ni kuachia shehena kutoka SGR kwenda kwenye maeneo yenye matatizo. lakini ni lazima tukubali pia kwamba tukiachia watu waendelee na kasi hii ya kuhamisha chakula, watu hawa watamaliza hata akiba zao na baadae kulalamika na kuomba msaada. Sasa suala la serikali kununua ziada yote nalo ni gumu kwa sababu za kibajeti na za kimahitaji. Hata hivyo, wakati tunakubali kwamba hali hii ni mbaya, tusiwe na negativity iliyopitiliza kiasi cha kutoa insinuations za kwamba kutakuwa na mgawo wa chakula na pale utakapotokea basi serikali haitatenda haki!
   
 13. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hehehehe! Habari uliyoandika na iliyoandikwa kwenye magazeti ni tofauti kabisa!! Sijui data zako umezitoa wapi...
   
 14. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,035
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakupinga kwa hili la kusema SGR wana chakula cha kutosha....katika kipindi kifupi kilichopita tulimsikia Rais katika hutuba yake akisema SGR ambayo sasa ni NFRA watatoa hifadhi yao sokoni ili kupunguza bei ya vyakula. Cha ajabu watendaji wake wakaanza kujigaia huku wakisikika katika vyombo vya habari kuwa ugawaji huo wa nafaka utahusisha wafanyabiashara wadogo tu. Cha ajabu wafanyabiashara wadogo hao walichonunua toka NFRA ni tani 600 huku karibu tani 20,000 wakijipatia wao kupitia kwa wafanyabiashara wakubwa na hayohayo mahindi waliojigawia ndiyo yaliyokamatwa Rombo na baadhi ya magunia yakiwa na chapa ya NFRA..sasa kwa hili huwezi sema eti Rombo kuna ziada ya chakula.

  Sasa ni kipindi ambacho serikali imekuwa ikifanya ununuzi wa nafaka kwa wakulima,katika kipindi kama hiki mara nyingi tumezoea kuona bei za nafaka zikishuka. Lakini Uliza sasa bei zinavyopanda kwa kasi...ni zaidi ya Sh. 500 kwa kilo ya mahindi.

  Kosa kubwa ambalo limefanya na hii serikali yetu nimekuwa nikisisitiza ni Msimu wa mavuno uliopita ambapo Serikali badala ya kuelekeza nguvu zao katika kununua nafaka za ziada mikononi mwa wakulima katika maeneo yaliyokuwa na mavuno mazuri, ikabaki ikihamisha nafaka hizo kutoka eneo moja kwenda lingine kwa nia madhubuti ya kupatiana tender za usafirishaji kwa makampuni ya usafirishaji yanayomilikiwa na Viongozi wetu huku tukiacha chakula cha ziada kikinunuliwa na nchi za Jirani kama kenya na Malawi, na sasa pamoja na kuwa hadi sasa nchi hizi hazijapata mavuno ya kutosha wana hifadhi kubwa ya nafaka kulioko sie ambao tuliongoza kwa mavuno katika msimu uliopita.

  My take kwenye hili ni usitishwaji wa ugawaji wa mahindi ya hifadhi ya Taifa kwa bei nafuu kwa hao wanaojiita ni wafanyabiashara kwa kisingizio eti cha kushusha bei ya vyakula huku wakiyasafirisha nje ya nchi kila kukicha na badala yake mahindi hayo yapelekwe kwenye maeneo yenye uhaba mkubwa wa chakula.
   
 15. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,035
  Trophy Points: 280
  Mkuu SGR unayoitaja je unajua kwa sasa wana akiba kiasi gani?? fatilia hilo kwanza ndipo uanze kufikiria hayo unayoyasema.
   
 16. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna hatari tukawa ama tunakuza swala la njaa ama tunadumaza ukubwa wake.
  Naomba kujua tatizo ni nini Tanzania.
  1. Hakuna chakula cha kutosha kulisha watanzania wote? ama
  2. Kuna sehemu za nchi hazina chakula cha kutosha na kuna sehemu kuna chakula cha kusaza?

  Natambua kwamba matatizo yote mawili yanasababisha njaa, lakini naamini kwamba
  yanatatuliwa kwa njia tofauti kabisa.

  1. Kama kuna tatizo la upungufu wa chakula kutulisha watanzania wote.
  Basi mfumo mzima wa kilimo nchini unatakiwa kufumuliwa na kusukwa upya kabisa.
  kuna mada ya kilimo kwenye thread nyingine, nimetoa maoni yangu huko.

  2. Kama matatizo ya chakula yako maeneo fulani fulani tu, basi hapa tatizo
  ni miundombinu ya uchukuzi na usafirishaji.

  Haya matatizo yote mawili yanauhusiano wa moja kwa moja na serikali
  iliyoko madarakani. Kama Mwanakijiji umegusia swala la njaa kipindi cha
  Mwalimu ukiandaa mazingira ya kuisontea kidole serikali iliyoko madarakani
  nakuunga mkono aslimia mia moja.

  Ntaweka nyama zaidi baadaye.
   
 17. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbopo
  Unaweza ukatuthibitishia vipi kwamba haiwezekani tukaingia kwenye food rationing kama
  kipindi cha mwalimu?

  Nchi hii inamatatizo mangapi ambayo sasa ni makubwa kuliko kipindi cha mwalimu?
  kwa nini hili lishindikane?

  Ukiamua kufanya risk assessment haiwezi kuepuka kufanya worse case scenerio analysis?
  Anachokifanya Mwanakijiji ni stress testing, kwamba, kama the worst happen now, what the
  impact will be? and how are we prepared to face it?

  Kama tayari tumeishajikuta kwenye several worse scenerios na serikali yetu imeshindwa
  kutukwamua salama na kwa haraka, kwa nini hauonekani kuwa na wasiwasi hili la chakula
  likitokea?

  Serikali yetu imeshindwa kutukwamua kutoka kwenye tatizo la umeme?
  Serikali yetu imeshindwa kutukwamua kutoka kwenye tatizo la rushwa?
  serikali yetu, ilipokutana na changamoto kubwa wakati wa uchaguzi imeshindwa kusimamia
  mabadiliko ya serikali kwa kufuata matakwa ya wananchi.
  Serikali yetu imesababisha mvua ionekane ni laana kwenye jamii yetu, ikija kwa wingi
  inatuua kwa mafuriko, leo unasema imekuja kidogo ndo maana tunanjaa, niambie
  wapi katika ardhi ya tanzania panaweza kuhimiri mvua inyayo kwa wingi?


  Nini kinakupa faraja kwambaserikali hii haitoweza kuruhusu njaa kutushambulia mpaka tukaingia
  kwenye food rationing?

  Hakika nakuambia, Kama likkitokea hili, Jakaya atasema yeye sio mbegu wala mbolea.
  Tumuombe Mungu acheleweshe jambo hili
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwakuwa hata MGao mkali UMEANZIA HAPA....MAMBO MEENGI HUANZIA HAPA.....
   
 19. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo la njaa ni la kujitakia.
   
 20. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  sijui ni ukame unachangia JANA NIMENUNU KIBIRITI TSH 100
   
Loading...