Serikali iache kuzifunga benki za kijamii kwa masharti yasiyoeleweka,iziache zikue na izilee

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Naona Benki Kuu wanazunguka huku na kule kuzifunga Benki za Kijamii(Community Banks)

Mhanga wa hivi karibuni ni Mbinga Community Bank,sababu kubwa wanayotoa eti wamepandisha kiwango cha mtaji kwa mabenki na kwamba hiyo benki haina mtaji huo.

Mimi nadhani BOT waangalie upya hili la kufunga Benki za Kijamii,hizi benki ziko karibu mno na wananchi kuliko hizi benki kubwa kubwa,na pia benki hizi ni juhudi za wananchi wenyewe na mitaji yao kuzianzisha.Kwa nini unaifunga?

Yaani wasomi waliokaa hapo benki kuu wamefundishwa kufunga mabenki tu na hawana alternative ideas ?

Benki Kuu kama regulator anatakiwa awe mlezi na pia mshauri na afanye hayo kwa malengo ya kuhakikisha Taasisi anazosimamia zinaendelea kuwepo,sio kuzinyonga.

Tuwaachie wananchi wa vijijini benki zao wakopeshane,nyie mnaokaa mjini endeleeni na benki zenu zenye masharti magumu kwa mwananchi wa kawaida,

Benki Kuu izipe jicho tofauti Benki hizi zinazozunguka mashambani kukopesha wananchi ambao benki nyingine ziligoma kuwakopesha
 
hahahaha....mku umenichekesha eti ziko karibu na wananchi..Kwani wananchi wanapewa hela ya bure? My friend community bank is just a business like any other business.

Na hela za wananchi zikipotea..utakuja hapa kusema wananchi wanyonge wanadhulumiwa? serikali iingilie kati? Get real my friend.
 
Kweli kabisa
Hao wanaozifunga hizi benki zinazokopesha wakulima,mama lishe,machinga na wafugaji,wote unakuta wana akaunti Standard Chartered Bank,CITIBANK na mabenki mengine yenye makao makuu ulaya,marekani na Canada.

Wanaona nongwa wana jamii nao kukopeshana
 
hahahaha....mku umenichekesha eti ziko karibu na wananchi..Kwani wananchi wanapewa hela ya bure? My friend community bank is just a business like any other business.

Na hela za wananchi zikipotea..utakuja hapa kusema wananchi wanyonge wanadhulumiwa? serikali iingilie kati? Get real my friend.
Wananchi wanakopeshwa katika mazingira rafiki....huwezi kuipa masharti sawa NMB na Mbinga Community Bank
 
BOT kwa maelezo yao wanasimamia sheria ya mabenki Banking and financial institution act 2006 and its regulations.
Hii inazitaka benk mtaji wake usipungue Bil 15.
Nadhani wazo lako ulipaswa upeleke bungeni wabadilishe sheria mkuu.
 
Bilioni 15 ni kwa benki za kibiashara benki za kijamii ni bilioni 5
Hii ni moja ya sentesi
"If the bank will continue with the current capital It will be detrimental to the interests of its depositors, Something which will pose risk to stability of the entire financial system" Hii ni sehemu ya hiyo statement.
Kama ni kweli BOT wako sahihi. Nimesoma mahala wameandika hiyo 15Bil na statement hapo juu.
Nadhani wataalamu wetu waachiwe wafanye kazi zao. Sidhani kama BOT watakuwa na lengo la kunyayasa jamii ya watu wa huko. Yote yanafanyika kwa faida pana...
 
BOT kwa maelezo yao wanasimamia sheria ya mabenki Banking and financial institution act 2006 and its regulations.
Hii inazitaka benk mtaji wake usipungue Bil 15.
Nadhani wazo lako ulipaswa upeleke bungeni wabadilishe sheria mkuu.
Wazielimishe na kuzipa fursa ya kuzikopesha

Otherwise basi benki za wananchi zinazohudumia wavuja jasho vijijini zifikiriwe tofauti katika kupanga madaraja ya mabenki.....Mbinga Community Bank au Dar es Salaam Community Bank zinafanya biashara katika eneo dogo sana,mfano huko Mbinga,kuna nyingine iko mufindi tu,nyingine Dar es salaam tu(Dar es salaam community bank),hizi zina limited operational area,tofauti na NMB,CRDB,NBC,haya yako nchi nzima na ni giants,

Sasa kuweka sharti moja kwa benki yenye kufanya kazi katika kiwilaya na ile yenye coverage nchi nzima is unfair.

Ifanyike haraka hatua ya kuzipa tofauti benki,lengo hasa kugusa zile zilizoanzishwa vijijini,hizi zinahitaji special attention,sehemu nyingine ukisema mtaji bilioni 15,hakika zitaozea benki tu hizo bilioni nyingi,hao wakulima wa chai walau waambiwe mtaji bilioni 7-10
 
"If the bank will continue with the current capital It will be detrimental to the interests of its depositors, Something which will pose risk to stability of the entire financial system"

Ila kikibwa naungana na wewe juhudi zifanyike kusaidia hizi benk zinazodili na wananchi wa kipato cha chini zisife.
 
Hao wataalam wanaitumikia jamii,hawajitumikii,watoke maofisini watwambie wameona shida gani na hatari gani,na wamefanya utafiti upi, wanatuongoza kitaalam,sio kututawala kitaalam kwa matamko
 
hahahaha....mku umenichekesha eti ziko karibu na wananchi..Kwani wananchi wanapewa hela ya bure? My friend community bank is just a business like any other business.

Na hela za wananchi zikipotea..utakuja hapa kusema wananchi wanyonge wanadhulumiwa? serikali iingilie kati? Get real my friend.
Kweli kabisa mkuu itakuwa kama kwa vyama vya ushirika vya msingi na mamlaka za mazao zilizopewa dhamana ya kuwainua wakulima vilivyogeuka na kuwa vitega uchumi vya watu binafsi wenye kila aina ya dhuruma na utapeli kwa wakulima,vinasababisha umasikini tu kwa wakulima na badala yake kuwanufaisha watendaji ndani ya vyama, mkulima anakatwa mpaka kodi ya kulipia ununuzi wa ma land cruiser yasiyomnufaisha bali kumwongezea gharama tu,wanakopesha pembejeo feki, na na kila aina ya makato halafu eti serikali ikae kimya pembeni ikiangalia tu simply because vyama hivyo vimenzishwa na wananchi wenyewe.
 
Acha zifungwe!

Kwa sasa tuna Bank karibia 50 Tena Nje ya hizo community bank

Kwa level ya Uchumi wetu na uzalishaji wetu ( GDP) sio Afya kuwa n utitiri wa Banks

Mitaji ya kuanzisha Banks ilishushwa kipindi ha Nyuma ili kuchochea ongezeko la Banks na kwa kuwa zimeongezeka na kujiimarisha ni wakati muafaka sasa kuziacha zilizopo na Ilizzongeza Mtaji baada ya kuanzishwa kuimarika kwa kuzuia Entrance of new Financial Instituition ili zilizopo ziimarike zaid!
 
Bank za Tanzania hazijawahi kuwa rafiki wa mtanzania, acha zifungwe.
 
Standard za kibenki tunazozitumia ni za marekani na ulaya ambao wenyewe wameishamiliku uchumi unaoitaji standard za za hivyo, sisi inapaswa tujiweke kwenye standard tunazoendana nazo kutokana na uchumi wetu lakini pia uwezo wa wafanyabiashara wa chini na wakulima ili tuwawezeshe kuinuka kiuchumi , mfano mdogo tu, mimi nimesoma uganda. nilikua napita mpakani mwa tanzania na Uganda mutukula, sasa tunapoenda kubadilisha hela wale money changer wako upande wa Uganda Tanzania hawapo, sasa nikauliza kwanini kwetu Tanzania hawapo? wakaniambia kuwa, upande wa uganda unachotakiwa kuwa nacho ni mtaji tu kama milioni mbili au tatu ili ufanye hizo kazi, lakini Tanzania ni lazima uwe na mtaji wa milioni 40 ndio uweze kufanya hizo kazi. sasa wale vijana wa uganda wamejenga magorofa pale, wanapeleka mazao uganda masemi kibao na kulipa kodi uko wana hoteli kibao na wameajiri watu umo.
 
Hizo kweli ni dharau serikali haiwezi kuzifunga benki kama inafunga milango ya chooni.
 
Mmeshaambiwa benki haina ukwasi (haina pesa za kukimu mahitaji ya kibenki) sasa itakopesha nini? Kifupi ni kuwa benki haizalishi na watu wanaendelea kula mshahara wa bure tuu.
 
Back
Top Bottom