Kitchener
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 13,823
- 27,694
Leo mitandao ilpata shida sana, ila naamini watendaji wa serikali wanafanya kazi kwa hofu, mfano TCRA kama wasingechukua hatua, wangeshughulikiwa, wala siwalaumu, wangeulizwa kwa nini mliruhusu mitandao wakati polepole anaongea?
Maria sarungi na wanaharakati wengine walikuwa wanatumia twitter x, serikali ikafunga kwa kigezo kuwa inaleta maudhui ya ngono, ila ukienda kule kwa VPN unaona account za viongozi wetu zinafanya kazi. najiuliza, kwahiyo viongozi wetu wanaangalia porno kule twitter au vipi? Jibu ni kwamba, wameadhibu watanzania woote waliokuwa wanatumia twitter kwa kujipatia kipato au kupata information zinazowafanya wapate ugali kwa sababu tu ya hofu au dispute yao. hii ni collective punishment na ni uonevu.
Gwajima ametoa maoni yake, serikali imefunga makanisa zaidi ya 2000 nchini kote, watu hawafungishani ndoa, watu hawazikani, watu hawaabudu, ibada zote zimefutwa, kwa kosa la gwajima tu (kama lipo). hii ni collective punishment. wangedili na gwajima, sio kuwapa adhabu waumini. wana haki kuabudu, ni kikatiba kabisa.
Polepole ametoa maoni yake, na alijiuzulu kwa hiari yake, matokeo yake wao wameenda kuteka dada yake; amekosa nini sasa?
Ninaishauri Serikali, iache kuadhibu watu wasio na makosa au ambao hawana direct dispute nao, sio haki, ukifanya hivyo kinachotokea ni kwamba, watu wanabaki na vinyongo moyoni na wanakuchukia zaidi.

- watu wanajiuliza, kwa hiyo serikali haitaki watu watoe maoni?
- ukifunga mitandao hutaki watu wapate information wawe gizani?
- waliokuwa wanaingiza kipato kwa mitandao wasipate pesa?
- ajira zenyewe hamna na zile za binafsi kwa mtandao hamtaki?
- watu wana maduka ya mtandaoni, wanafilisika, ndio nia ya serikali?
- mnataka ninyi tu ndio muwasiliane na kujua yanayoendelea duniani ila wananchi wawe gizani?
- mnafikiri hawa wananchi ni mifugo mmeiweka kwenye cage muifanye mpendavyo?
- haitaki watu wakosoa? inataka iimbiwe nyimbo za sifa na kuabudiwa tuuu nchi hii yote iwe ya machawa?
- inataka watu waishi gizani wasijue kinachoendelea duniani kwa sababu wanafunga mianya ya information na maoni?
- inataka kutisha watu wakitoa tu maoni wanashughulikiwa hivyo watu wakae kimya?
- serikali haijui kama imewekwa madarakani na wananchi na siku wakichoka wanaweza kuiondoa pia?
- hawajifunzi kwa gadafi aliyetoa pesa na mtaji kwa raia wanaishi kwa kugharimiwa vitu vingi na serikali ila waliponyimwa uhuru waliona pesa na vyote hivyo ni takataka bora uhuru?
- hivi hii serikali inataka nini?
- wao ni wakubwa kuliko Mungu?
- Mungu mwenye ametupatia uhuru kuchagua kufuata njia njema au mbaya sembuse wewe rais wa dunia?