Serikali iachane na kesi za Wapinzani

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Kinachoonekana kwa sasa ni huu Utawala wa Rais Magufuli kujikita kwenye siasa za chuki dhidi ya Wapinzani. Karibu Wabunge na Viongozi wote wa Upinzani kwa sasa wana aidha kesi 1,2 au 3 hadi 8 kama Mhe. Tundu Lissu zinaendelea Mahakamani na wengine wako Mahabusu. Kesi zote zinahusu UCHOCHEZI na hakuna kesi ya UFISADI, WIZI au KUGHUSHI NYARAKA zozote...!!

Nitarejea kesi mbili muhimu zinazowahusu Wabunge machachari wa CHADEMA. Kuna Mhe Godbless Lema(MB-Jiji la Arusha) na Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu(MB-Jiji la Mbeya). Kesi zote zina dhamana kulingana na Haki,Sheria na Katibaya nchi lakini kwa maksudi Mhe. Lema alikaa mahabusu miezi 4 pamoja na juhudi zote za kumpigania atoke kwa dhamana. Jambo lilelile lilofanyika Arusha kwa sasa linajirudia Mbeya mjini kwa Mhe. Sugu na kwa mazingira yaleyale ya madai ya kumkosoa Rais Magufuli hivo kufunguliwa kesi ya Uchochezi na kunyimwa dhamana.

Tayari kuna kila dalili ya kumfanya Mhe. Sugu aendelee kusota remande kwa kesi ya Uchochezi kwa wiki, miezi au hata mwaka huku ushahidi wa upande wa Serikali ikiwa ni kanda iliyorekodiwa tarehe 30/12/2017 katika mkutano wa Mbunge wa Mbeya akiwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu ikionyesha kuwa alimkosoa Rais au kumkashfu....!!!Upande wa Serikali wanang'ang'ania kuwa Mhe. Mbilinyi na Mhe.Emmanuel Masonga-Katibu CHADEMA Nyanda za Juu Kusini kuwa hawawezi kupewa dhamana maana itahatarisha usalama wao...!!!Sijui ni kwa vipi na kwa namna gani. Kwamba watuhumiwa walitoa lugha sijui chafu au ya kumkosoa Rais iwapo wakipewa dhamana watahatarisha usalama wao..!!!Kivipi??Haingii akilini.

Kama Rais Magufuli juzi kwenye sherehe za Uhuru waJMT aliweza kuwaachia HURU watu waliokuwa wamefungwa JELA MAISHA au HUKUMU YA KIFO kwa kesi za MAUAJI na KUBAKA WATOTO WACHANGA, inakuwaje Waheshimiwa Wabunge wa UPINZANI ambao ni Viongozi wa Wananchi kwa kuchaguliwa tena kwa kura nyingi sana kwenye majimbo yao wanang'ang'aniwa kwa kesi za kutengeneza kwa kisingizio cha Uchochezi??? Naomba Mahakama Kuu ya Tanzania iingilie kati na itoe TAFSIRI au ufafanuzi wa neno UCHOCHEZI na ni wakti gani mtu au raia anaangukia kwenye makosa ya UCHOCHEZI.

Haiwezekani mtu aliyaua, aliyebaka au kulawiti, aliyeiba au kufisidi leo anapewa msamaha wa Rais Magufuli huyuhuyu ambaye hataki Mbunge wa Upinzani apewe dhamana kwa kutumia haki yake ya Kikatiba kama Raia wa Tanzania na Mbunge kuikosoa Serikali yake anawekwa Mahabusu na kufunguliwa kesi za Uchochezi na ikibidi afungwe miezi au Miaka kadhaa...!!!Tumeona kwa Mhe. Peter Lijualikali(MB)-Kilombero kwa kufungwa jela miezi 6 kwa kosa la kubambikiwa tu...kisa ni Mbunge wa Upinzani. Lakini Babu Seya na kijana wake waliobaka watoto wetu leo wako huru na walishakaribishwa Ikulu na Rais Magufuli kama Wafalme!!!Hii ni kitu haiingii akilini asilani!!!!.

Nina hakika Dunia inaposoma na kusikiliza Habari za Tanzania inajiuliza mara 2 hii nchi inaongozwa na watu wa aina gani. Si ajabu M-7 amempongeza Rais Trump wa Marekani kwa kuwapa vidonge vyao viongozi wa Afrika akiwemo na M-7 mwenyewe kwa namna wanavyo lidhalilisha Bara la AFRIKA!! Heshima ya Afrika imeondoka na kina Nyerere,Mandela, Nkrumah na Kaunda kwa kuwataja wachache...!

Wasalaam.
 
Hivi nyinyi bavicha huwa mna akili za kutosha hata kijiko?

Hamujui hata kwamba mahakama ni mhimili unaojitegemea??

Chadema ni janga

Hayo ni ya kwako na Uvccm yako. Mimi sihusiki na Bavicha, CCM wala Lumumba......!!!
Hapa naongea kama Mtanzania Mzalendo ambaye sifurahishwa na namna Wapinzani wanavyonyanyaswa na kukandamizwa pasi na sababu za msingi....!!!.

Tell me, ni akili gani ianyoweza KUSAMEHE WAUAJI, WAFIRAJI NA WABAKAJI lakini ikakamata Mbunge anayetimiza wajibu wake kwa kufanya mikutano na kukosoa serikali iliyoko madarakani(kwa mujibu wa siasa ya vyama vingi).....!!

Unamwachia huru mtu aiyehukumiwa kunyongwa lakini unamfunga Mbunge wa Upinzani kwa kosa la kukosoa...!!

Hii ndiyo tunayosoma kwenye Vitabu vya Dini Nabii Issa aliwaambia Mafarisayo Wanafiki waliokuwa wakichuja MBU lakini wakimeza NGAMIA...!!! It doesn't make any sense at all!!!! Huu ni wendawazimu na ni mambo ya hovyo na aibu...!!
 
Hayo ni ya kwako na Uvfccm yako. Mimi sihusiki na Bavicha, Wiziccm wala Lumumba......!!!
Hapa naongea kama Mtanzania Mzalendo ambaye sifurahishwa na namna Wapinzani wanavyonyanyaswa na kukandamizwa pasi na sababu za msingi....!!!.

Tell me, ni akili gani ianyoweza KUSAMEHE WAUAJI, WAFIRAJI NA WABAKAJI lakini ikakamata Mbunge anayetimiza wajibu wake kwa kufanya mikutano na kukosoa serikali iliyoko madarakani(kwa mujibu wa siasa ya vyama vingi).....!!
Unamwachia huru mtu aiyehukumiwa kunyongwa lakini unamfunga Mbunge wa Upinzani kwa kosa la kukosoa...!! Hii ndiyo tunayosoma kwenye Vitabu vya Dini Nabii Issa aliwaambia Mafarisayo Wanafiki waliokuwa wakichuja MBU lakini wakimeza NGAMIA...!!! It doesn't make any sense at all!!!! Huu ni wendawazimu na ni mambo ya hovyo na aibu...!!
Mbunge anatimiza wajibu kwa kutukana matusi??
 
Ndo siasa walizozichagua kwa sasa. Wafanye tuu maana wapo kwenye Mbereko.
 
Mbunge anatimiza wajibu kwa kutukana matusi??

Naona wewe ni kanjanja au kihiyo wa kisiasa na hujui hata maana na tofauti kati ya MATUSI na KUKOSOA!!!
Kukosoa au kukosolewa mbona ni jambo la Kawaida kabisa na ndo maana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere(RIP) aliwahi VIONGOZI LAZIMA WAKUBALI KUKOSOA NA KUKOSOLEWA because they're not Angels from heave...!!. Mwalimu alikuwa na hekima, busara na kipawa cha Uongozi na alijua maana na faida za kukosoa na kukosolewa. Ndo maana wakati anang'atuka aliomba MSAMAHA KWA WATANZANIA KWA MAKOSA ALIYOFANYA NA AKAMWOMBEA MSAMAHA hata Rashid Mfaume Kawawa=rip(MP)...!!!Hawa ndo walikuwa viongozi wa kweli siyo sasa hivi tuna makanjanja tu wanaojifanya miungu watu wasiokubali kukosolewa...!!Matokeo yake ndiyo haya!!
 
Mkosoe Mbowe akuchachawangwe.
 
Mkosoe Mbowe akuchachawangwe.
Hivi unajitambua kabisa kabisa wewe? Hoja hujibiwa na hoja na sio nondo za mahabusu!
Nakurudisha shule japo najua kuwa hukuhudhuria ipasavyo kuwa in any action there's reaction! Na ukweli haufunikiki kwa namna yoyote. Kwanini mkasirike mkiambiwa ukweli?
Nanunua ugomvi sasa. Mbowe unayemtaja hapa hana dola wala sio hayupo juu ya sheria. Kama unaweza kuthibitisha tuhuma za kuwaua wanaomkosoa na mamlaka ikajua na kumwacha afanye hivyo basi kosa sio lake bali ni la mamlaka na dola! Kwanini msimkamate na kumshtaki? Huu mpango wenu wa kuwasakama watu wenye ushawishi na wanaokubalika kwa jamii hautokaa ufanikiwe bali utazidi kumng'arisha mbele ya umma! Endelea kutumika wakati wenye uelewa wanachanja mbuga kuelekea mafanikio!
 
Kinachoonekana kwa sasa ni huu Utawala wa Rais Magufuli kujikita kwenye siasa za chuki dhidi ya Wapinzani. Karibu Wabunge na Viongozi wote wa Upinzani kwa sasa wana aidha kesi 1,2 au 3 hadi 8 kama Mhe. Tundu Lissu zinaendelea Mahakamani na wengine wako Mahabusu. Kesi zote zinahusu UCHOCHEZI na hakuna kesi ya UFISADI, WIZI au KUGHUSHI NYARAKA zozote...!!

Nitarejea kesi mbili muhimu zinazowahusu Wabunge machachari wa CHADEMA. Kuna Mhe Godbless Lema(MB-Jiji la Arusha) na Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu(MB-Jiji la Mbeya). Kesi zote zina dhamana kulingana na Haki,Sheria na Katibaya nchi lakini kwa maksudi Mhe. Lema alikaa mahabusu miezi 4 pamoja na juhudi zote za kumpigania atoke kwa dhamana. Jambo lilelile lilofanyika Arusha kwa sasa linajirudia Mbeya mjini kwa Mhe. Sugu na kwa mazingira yaleyale ya madai ya kumkosoa Rais Magufuli hivo kufunguliwa kesi ya Uchochezi na kunyimwa dhamana.

Tayari kuna kila dalili ya kumfanya Mhe. Sugu aendelee kusota remande kwa kesi ya Uchochezi kwa wiki, miezi au hata mwaka huku ushahidi wa upande wa Serikali ikiwa ni kanda iliyorekodiwa tarehe 30/12/2017 katika mkutano wa Mbunge wa Mbeya akiwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu ikionyesha kuwa alimkosoa Rais au kumkashfu....!!!Upande wa Serikali wanang'ang'ania kuwa Mhe. Mbilinyi na Mhe.Emmanuel Masonga-Katibu CHADEMA Nyanda za Juu Kusini kuwa hawawezi kupewa dhamana maana itahatarisha usalama wao...!!!Sijui ni kwa vipi na kwa namna gani. Kwamba watuhumiwa walitoa lugha sijui chafu au ya kumkosoa Rais iwapo wakipewa dhamana watahatarisha usalama wao..!!!Kivipi??Haingii akilini.

Kama Rais Magufuli juzi kwenye sherehe za Uhuru waJMT aliweza kuwaachia HURU watu waliokuwa wamefungwa JELA MAISHA au HUKUMU YA KIFO kwa kesi za MAUAJI na KUBAKA WATOTO WACHANGA, inakuwaje Waheshimiwa Wabunge wa UPINZANI ambao ni Viongozi wa Wananchi kwa kuchaguliwa tena kwa kura nyingi sana kwenye majimbo yao wanang'ang'aniwa kwa kesi za kutengeneza kwa kisingizio cha Uchochezi??? Naomba Mahakama Kuu ya Tanzania iingilie kati na itoe TAFSIRI au ufafanuzi wa neno UCHOCHEZI na ni wakti gani mtu au raia anaangukia kwenye makosa ya UCHOCHEZI.

Haiwezekani mtu aliyaua, aliyebaka au kulawiti, aliyeiba au kufisidi leo anapewa msamaha wa Rais Magufuli huyuhuyu ambaye hataki Mbunge wa Upinzani apewe dhamana kwa kutumia haki yake ya Kikatiba kama Raia wa Tanzania na Mbunge kuikosoa Serikali yake anawekwa Mahabusu na kufunguliwa kesi za Uchochezi na ikibidi afungwe miezi au Miaka kadhaa...!!!Tumeona kwa Mhe. Peter Lijualikali(MB)-Kilombero kwa kufungwa jela miezi 6 kwa kosa la kubambikiwa tu...kisa ni Mbunge wa Upinzani. Lakini Babu Seya na kijana wake waliobaka watoto wetu leo wako huru na walishakaribishwa Ikulu na Rais Magufuli kama Wafalme!!!Hii ni kitu haiingii akilini asilani!!!!.

Nina hakika Dunia inaposoma na kusikiliza Habari za Tanzania inajiuliza mara 2 hii nchi inaongozwa na watu wa aina gani. Si ajabu M-7 amempongeza Rais Trump wa Marekani kwa kuwapa vidonge vyao viongozi wa Afrika akiwemo na M-7 mwenyewe kwa namna wanavyo lidhalilisha Bara la AFRIKA!! Heshima ya Afrika imeondoka na kina Nyerere,Mandela, Nkrumah na Kaunda kwa kuwataja wachache...!

Wasalaam.
Kampe wewe dhamana utukane makusudi utegemee dhamana,sasa ataenda kujielezea vizuri raisi alimuua nani?Break za mdomo hamna afu mnalia dhamana dhamana
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom