Serikali iachane na kesi za Wapinzani

kinachoendelea kwa sasa hapa nchini sio haki kamwe.mbaya zaidi vyombo vinavyopaswa kutoa haki vinatumika kukandamiza wengine kisa tu ya tofauti ya kiitikadi. rais akumbuke kwamba mtawala wa leo ni mpinzani wa kesho. uongozi wa awmu ya tano kumbukeni kiapo chenu kinasemaje....
 
Nakumbuka ya Arusha... Nassari kapeleka ushahidi uliorekodiwa lakini mwisho wa siku Ni kimya, ukifuatilia utaona Luna watu WA serikali walihusishwa, haki IPO wapi?
 
Kinachoonekana kwa sasa ni huu Utawala wa Rais Magufuli kujikita kwenye siasa za chuki dhidi ya Wapinzani. Karibu Wabunge na Viongozi wote wa Upinzani kwa sasa wana aidha kesi 1,2 au 3 hadi 8 kama Mhe. Tundu Lissu zinaendelea Mahakamani na wengine wako Mahabusu. Kesi zote zinahusu UCHOCHEZI na hakuna kesi ya UFISADI, WIZI au KUGHUSHI NYARAKA zozote...!!

Nitarejea kesi mbili muhimu zinazowahusu Wabunge machachari wa CHADEMA. Kuna Mhe Godbless Lema(MB-Jiji la Arusha) na Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu(MB-Jiji la Mbeya). Kesi zote zina dhamana kulingana na Haki,Sheria na Katibaya nchi lakini kwa maksudi Mhe. Lema alikaa mahabusu miezi 4 pamoja na juhudi zote za kumpigania atoke kwa dhamana. Jambo lilelile lilofanyika Arusha kwa sasa linajirudia Mbeya mjini kwa Mhe. Sugu na kwa mazingira yaleyale ya madai ya kumkosoa Rais Magufuli hivo kufunguliwa kesi ya Uchochezi na kunyimwa dhamana.

Tayari kuna kila dalili ya kumfanya Mhe. Sugu aendelee kusota remande kwa kesi ya Uchochezi kwa wiki, miezi au hata mwaka huku ushahidi wa upande wa Serikali ikiwa ni kanda iliyorekodiwa tarehe 30/12/2017 katika mkutano wa Mbunge wa Mbeya akiwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu ikionyesha kuwa alimkosoa Rais au kumkashfu....!!!Upande wa Serikali wanang'ang'ania kuwa Mhe. Mbilinyi na Mhe.Emmanuel Masonga-Katibu CHADEMA Nyanda za Juu Kusini kuwa hawawezi kupewa dhamana maana itahatarisha usalama wao...!!!Sijui ni kwa vipi na kwa namna gani. Kwamba watuhumiwa walitoa lugha sijui chafu au ya kumkosoa Rais iwapo wakipewa dhamana watahatarisha usalama wao..!!!Kivipi??Haingii akilini.

Kama Rais Magufuli juzi kwenye sherehe za Uhuru waJMT aliweza kuwaachia HURU watu waliokuwa wamefungwa JELA MAISHA au HUKUMU YA KIFO kwa kesi za MAUAJI na KUBAKA WATOTO WACHANGA, inakuwaje Waheshimiwa Wabunge wa UPINZANI ambao ni Viongozi wa Wananchi kwa kuchaguliwa tena kwa kura nyingi sana kwenye majimbo yao wanang'ang'aniwa kwa kesi za kutengeneza kwa kisingizio cha Uchochezi??? Naomba Mahakama Kuu ya Tanzania iingilie kati na itoe TAFSIRI au ufafanuzi wa neno UCHOCHEZI na ni wakti gani mtu au raia anaangukia kwenye makosa ya UCHOCHEZI.

Haiwezekani mtu aliyaua, aliyebaka au kulawiti, aliyeiba au kufisidi leo anapewa msamaha wa Rais Magufuli huyuhuyu ambaye hataki Mbunge wa Upinzani apewe dhamana kwa kutumia haki yake ya Kikatiba kama Raia wa Tanzania na Mbunge kuikosoa Serikali yake anawekwa Mahabusu na kufunguliwa kesi za Uchochezi na ikibidi afungwe miezi au Miaka kadhaa...!!!Tumeona kwa Mhe. Peter Lijualikali(MB)-Kilombero kwa kufungwa jela miezi 6 kwa kosa la kubambikiwa tu...kisa ni Mbunge wa Upinzani. Lakini Babu Seya na kijana wake waliobaka watoto wetu leo wako huru na walishakaribishwa Ikulu na Rais Magufuli kama Wafalme!!!Hii ni kitu haiingii akilini asilani!!!!.

Nina hakika Dunia inaposoma na kusikiliza Habari za Tanzania inajiuliza mara 2 hii nchi inaongozwa na watu wa aina gani. Si ajabu M-7 amempongeza Rais Trump wa Marekani kwa kuwapa vidonge vyao viongozi wa Afrika akiwemo na M-7 mwenyewe kwa namna wanavyo lidhalilisha Bara la AFRIKA!! Heshima ya Afrika imeondoka na kina Nyerere,Mandela, Nkrumah na Kaunda kwa kuwataja wachache...!

Wasalaam.
Tunajua umetumwa na hao mbumbu na Nyumbu na Makarai ya Chadema.
 
Dhana potofu kabisa ni kudhani kuwa kwa kuwakandamiza na kuwadhalilisha viongozi wa upinzani wa serikali hii. Kwamba hiyo itasaidia CCM na viongozi wake kupendwa na kukubalika!!! Si kweli CCM na viongozi waandamizi wanachukiwa zaidi ya 2015. Na kama mtu anabisha uwepo uchaguzi huru na wa haki

Cairo's
 
Ndom madhara ya kuwapa Nchi watu tusiowafahamu vizuri kazazi hadi kizazi mwisho wa siku unampa mtu umjui anatokea wapi ukiona mtu anasema sana mimi mtanzania anarudia mara kwa mara kwa kutumia Nguvu Tafakari ni sawa na mtu kujifanya mzalendo kuzindi wenzio
 
Tunajua umetumwa na hao mbumbu na Nyumbu na Makarai ya Chadema.

Makusudically,
Wewe ni chizi perce...!!!Kwa taarifa yako hakuna aliyenituma isipokuwa nafsi yangu kama mtu ninayejitambua...!!!
Mimi naongelea nchi yetu ya Tanzania jinsi HAKI ZA MSINGI ZA KIKATIBA,UHURU WA KUTOA MAWAZO na UZALENDO NA UTU wa Watanzania wenzetu unavyodhalilishwa kwa sababu tu ya tofauti za kisiasa......!!!
Sijali wewe ni CCM kindakidanki,KADA , UVFCCM, LUMUMBA street, MTU ASIYEJULIKANA or whatsoever...!!Swala hapa ni kwanini KATIBA INAKIUKWA ILI KUWAKANDAMIZA WATANZANIA WENZETU KWASABABU TU HAWAKO CCM....???Try to think big man....Acha ujinga. Leo CCM iko madarakani kesho haitakuwepo....utakimbilia wapi???!
Baba wa Taifa Mwl. Nyerere(rip) pamoja na busara, hikma, maarifa na kipawa alichokuwa nacho aliwahi kusema, "......CCM SIYO MAMA YAKE" What says you about that?? Nasema tena acha ujuha...!!!
 
inamaana unataka kuipangia serikali vipaumbele vyake?
Swali lako lina dhihirisha ujinga ulio nao...!!!Serikali ni nani???
If you can answer me that simple question, then you have an answer for your silly question...!!!
 
Mbunge anatimiza wajibu kwa kutukana matusi??

Amemtukana nani?Hivi wale waliohamasisha UVCCM wawapige wapinzani akina BAshe na Masha wamefanywa nini kitu gani mpaka sasa?Double Standard au ?Hakuna matusi wala nini ni Chuki ya wapinzani tu.Mnaiaibisha nchi
 
Kinacho endelea sasa ni " ukinipiga unanionea, ukiniacha unaniogopa". Kesi zinazoendelea ni za kumtukana mtu na kumzushia uongo SIO kukosoa serikali.
 
Amini amini nawaambia yule mwovu muda wote usiku na mchana huzunguka kila eneo kutafuta mawindo yake kwa lengo la kuangamiza 'wanadamu', salini na mkiomba ili Baba yenu wa Mbinguni apate kuwaokoa ktk mikono ya 'shetani' huyu.
 
Back
Top Bottom