Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,492
- 92,962
Hiyo ni hoja ya CCM kupitia kwa acting Secretary wao Mtatiro A.K.A Julius mwenye Sigida.
Si aingize hayo kwenye katiba mpya inayokuja maana kwa mujibu wa katiba ya sasa mbunge akifa unafanyika uchaguzi wa kutafuta mbunge mpya na hiyo ndiyo Demokrasia "Poti kumbuka mambo mazuri gharama" so kwakuwa tumetaka demokrasia na tuwe tayari kubeba gharama zake piaNaibu Katibu mkuu wa CUF Julius Mtatiro ameitaka serikali kuachana mara moja na chaguzi ndogo kwani ni kutapanya hela za walipa kodi bure.
Mtatiro amesema serikali inapaswa kupitisha sheria kwamba anapokufa mbunge sharti arithiwe kutoka chama kile kile bila kufanya uchaguzi upya.
Akizungumzia uchaguzi wa Arumeru alisema CCM ilipaswa kumteua mrithi bila kufanyika uchaguzi.
Mtatiro alitoa mfano wa nchi za Msumbiji na Ghana kwamba zinafuata mfumo huo.
Source: MWANANCHI
Kama umesoma mawazo yangu. Huu ni wivu tu kwa kuwa wanaumizwa na mafanikio ya CDM.ingeshinda ccm wangesema hayo?
Demokrasia ina gharama zake brother. Sasa huyo wa kuteuliwa atakuwa na tofauti gani ni kina Vicky Kamata?
Labda tuwe tunachagua kama raisi na makamu wake, at least tunajua tunachagua mtu na atakayemrithi kama kutakuwa na tatizo. Kuteuana, hell no.
Maoni mazuri kabisa mkuu! Gharama za kuhudumia wabunge wa viti maalumu ni kubwa sana,na wengi wao hawana tija. Pili majimbo ya uchaguzi huko Zanzibar yagawanywe upya. Watu Milioni moja na nusu wabunge 70!! Tatu liingizwe sharti muhimu,wagombea wote kupimwa Afya zao kabla ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.Uchaguzi uliomalizika juzi Arumeru Mashariki unatoa soma MOJA, kwamba watanzania wanachagua MTU na sio CHAMA. Ucahguzi wa 2010 Waarumeru walimchagua Jeremiah Sumari (CCM), Lakini juzi tu baada ya miaka 2 Waarumeru hao hao wamemchagua Joshua Nassari wa (CDM).
Hivyo kushauri kwamba mbunge anapofariki basi CHAMA kimuchague mwingine ni kawanyima wananchi haki ya kuongozwa na mtu wanayemtaka.
Ndiyo hizi chaguzi ndogo zinatumia pesa nyingi na ni kutapanya our meagre limited resources. Lakini mimi ningependekeza njia mojawapo ya kupunguza matumizi ya kuwapata na kuwagharamikia wabunge ni KUONDOKANA NA WABUNGE WA VITI MAALUMU. Just imagine tukiondokana na hawa wabunge tutakuwa tume save pesa kiasi gani zinazotumika kuwahudumia hawa wabunge wa VITI MAALUMU.
Democracy ina gharama zake, hivyo tusitafute short cut.
Mkuu hii ni hatari watu watauana kisa ubunge ni heri tu tuseme wanachama wa chama kilichoshinda ubunge kwenye jimbo wachague mbunge wao kwa gharama za chamaDemokrasia ina gharama zake brother. Sasa huyo wa kuteuliwa atakuwa na tofauti gani ni kina Vicky Kamata?
Labda tuwe tunachagua kama raisi na makamu wake, at least tunajua tunachagua mtu na atakayemrithi kama kutakuwa na tatizo. Kuteuana, hell no.
Nakubaliana na hoja kwamba serikali inaingia gharama kubwa kushughurikia chaguzi ndogo, wazo langu ni achukuliwe aliyekuwa mshindi wa pili bila kujali chama alichotoka maana anakuwa alipigiwa kura na wananchi wote. Kumchukuwa mtu kutoka chamani mmmh!?
Naibu Katibu mkuu wa CUF Julius Mtatiro ameitaka serikali kuachana mara moja na chaguzi ndogo kwani ni kutapanya hela za walipa kodi bure.
Mtatiro amesema serikali inapaswa kupitisha sheria kwamba anapokufa mbunge sharti arithiwe kutoka chama kile kile bila kufanya uchaguzi upya.
Akizungumzia uchaguzi wa Arumeru alisema CCM ilipaswa kumteua mrithi bila kufanyika uchaguzi.
Mtatiro alitoa mfano wa nchi za Msumbiji na Ghana kwamba zinafuata mfumo huo.
Source: MWANANCHI
Wengine wanasema, 'aliyekuwa mshindi wa pili ndio akabidhiwe jukumu'. Mimi nasema yote ni mawazo mazuri, lakin inabidi yatekelezwe kwa tahadhari. Ni mpaka tutakapokuwa na Tume Huru ya uchaguzi, uchaguzi huru na wa haki, sheria nzuri za uchaguzi na katiba bora, ndio mambo haya yatakuwa na mashiko zaidi.
Nadhan itakuwa busara kama tutayaangalia mambo haya kwenye mchakato wa katiba MPYA. Na lazima tutayaangalia tu