Serikali: Hatujaapisha viongozi Migombani

Serikali: Hatujaapisha viongozi Migombani

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,699
Reaction score
9,591
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ilala amepinga vikali kuapishwa kwa mwenyekiti wa mtaa wa segera-Migombani kulikofanywa na wakili binafsi, akisema kuwa ni ubabaishaji na kitendo ambacho hakikubaliki kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Kauli hii imekuja Siku moja baada ya wananchi wa mtaa huo wa Migombani jijini Dar es Salaam kuchukua dhamana ya kumuapisha mwenyekiti wao kwa kutumia wakili binafsi.

Wakati Mkurugenzi huyo wa Ilala akitoa kauli hiyo, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Segerea, Gango Filemon Kidera amebainisha kuwa wananchi wataendelea kupata huduma za kiserikali kutoka ofisi hiyo kama inavyotakiwa kwani kilichofanywa kilikuwa wazi na kilizingatia sheria za nchi na si batili kama inavyozaniwa.

"Tunasubiri tuone mkurugenzi anataka kumuweka nani badala ya kiongozi ambaye wananchi wamemchagua. Sababu za kutowaapisha viongozi waliochaguliwa hazijitoshelezi ndiyo maana wananchi wameshinikiza zoezi hilo lifanywe na wakili wa kujitegemea na sheria zinaruhusu kwakuwa zinataka mtu anayefanya hivyo ama awe hakimu au kamishna wa viapo," alisema Kidera na kuongeza kuwa:

"Endapo kutakuwa na utata wowote utakaojitokeza baada ya mwenyekiti na wajumbe wake kuanza kutekeleza majukumu yao basi nguvu ya umma itatumika kuamua hatma ya hali hiyo…tutaandamana na wananchi wanasubiri kuona hilo linatokea."
 
Hawa wakurugenzi ni chanzo cha machafuko, wao wakubali tu pale anaposhinda yeyote
 
Huyo Mkurugenzi mbambaishaji kwisha habari yake.CCM ina kauli ya kusema kama mtu haridhiki aende mahakamani, kwa hiyo kama mkurugenzi huyo anaona sheria zimekiukwa si aende mahakamani.
 
Chama cha majambazi bhana!Wana hujuma aisee yaani hadi aliyechaguliwa na wananchi wanataka wampige chini dah!
 
Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.
 
kama.kule simanjiro hadi wakamuua yule aliyeshida kisa chama hakimtaki ila wananchi wamempenda
 
huyo nitabia ya maharage kurukaruka kwenye chungu pindi tu moto ukiwa unakolea.lakini yanasahau kuwa kurukaruka kwao ndio kuiva...!!
 
Sasa huyo Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala kama alijua ni kinyume cha utaratibu walichokifanya Wananchi wa mtaa wa Migombani alikuwa anasubiri nini muda wote asishughulikie kasoro hiyo!? Au ni rushwa aliyokula anawaza ni kwa namna gani atairudisha kwa mwenyewe baada ya zoezi la kuchakachua Wananchi kukwama!? Hawa Wakurugenzi wa Halmashauri wa Mikoa+Wilaya ni makada wa CCM, na ndiyo watakaoanzisha vurugu October2015!
 
Nilivosikia no mtaa wa Migombani nilijua ni kule Regent Estate, karibu na Uporoto nyumbani kwa JK! Kumbe ni Tabata.
 
Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.
Ndugu yangu MUSSALLAN, ukitaka hali kama hiyo isitokee (machafuko) washauri hao wanaosababisha hali ya namna hiyo kutokea waache mara moja. Mkurugenzi wa Ilala hana sababu ya kutowaapisha viongozi toka upinzani na sababu zake hazina mashiko.
 
Sasa kama wao wanaotaka kuongozwa wameshagua mtu wao halafu wao wasioongozwa hawamtaki, tatizo liko wapi? si wawaache na kiongozi wao?
 
Serikali ya kibabaishaji na viongozi wake ni wababaishaji.

Na huu ubabaishaji sio tu kwa hao wakurugenzi bali unaanzia ofisi ya Waziri Mkuu.

THE BIG question is ni kwanini huyo Mkurugenzi hajawaapisha viongozi wa Migombani?

Tutamulaumu bure tu huyu Mkurugenzi, lakini huu uhuni unaratibiwa na una baraka zote za Pinda!
 
Back
Top Bottom