Serikali: Hatufufui TRL mpaka uongozi ubadilishwe................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali: Hatufufui TRL mpaka uongozi ubadilishwe.................

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 6, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Serikali: Hatufufui TRL mpaka uongozi ubadilishwe


  na Betty Kangonga


  [​IMG] WAZIRI wa Uchukuzi Omary Nundu amesema kuwa serikali haitaweza kutoa fedha za kuendesha na kufufua Kampuni ya Reli Nchini (TRL) hadi pale uongozi utakapobadilishwa.
  Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uchukuzi ilisema kuwa Nundu alitoa kauli hiyo katika ziara ya siku moja mkoani Morogoro akiwa ameambatana na Naibu wake Athman Mfutakamba.
  Ilisema kuwa ni lazima uongozi ubadilishwe na kuwekwa mwingine madhubuti ndipo fedha hizo zitolewe na kuwa zoezi hilo linahitajika kutekelezwa mapema.
  “Mwenendo ninaouona haunipi matumaini katika kuliendesha shirika…yapo mambo mengi nayaona ya kiutawala zaidi na sio mtaji pekee hata wakipewa fedha katika hali hii hakuna kitakachobadilika,” ilisisitiza.
  Kwa mujibu wa taarifa ya meneja wa ufundi wa karakana Ngosomwile ilisema kuwa watahakikisha wanafanya jitihada ili karakana kubwa ya matengenezo ya reli iweze kupatiwa mahitaji yake muhimu na kurudisha uwezo wa kutoa huduma kama ilivyokuwa awali.
  Ilieleza kuwa karakana hiyo inakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa fedha hatua inayosababisha kushindwa kuendelea na uwezo wa kutengeneza vichwa vya treni.
  Hata hivyo ilisema kutokana na matatizo yanayoikabili karakana hiyo kuna wakati ulazimika kutoa vifaa katika injini moja na kuweka kwenye injini nyingine kama sehemu ya kufufua angalau injini chache.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Uongozi amdhubuti wanajua hata namna ya kuupata kama wangelikuwa wanajua mbona nchi hii kila mahali mambo ni shaghala baghala?
   
 3. m

  mzambia JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Siyo kauli ya kutolewa na kiongozi wa juu ka yeye. Damn nundu damn
   
Loading...