Serikali harakisheni mfumo wa Bima ya Afya kwa wote watu wanakufa huku

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
230
547
Nchi zetu za kiafrika uzalendo uko chini sana na hasa hasa kwetu Tanzania

Nieleweke neno uzalendo hapa namaanisha ile hali ya mtu kuwa commited kutekeleza majukumu yake kikamilifu kutoka ndani ya moyo wake pasipo kulazimishwa au kushurutishwa na wakubwa wa kazi

Watumishi wengi hasa sekta ya afya hii commitiment hawana kabisa kabisa kabisa hasa hasa hawa vijana wadogo ambao tulitegemea wawe chachu kazini kwasababu ya morali na ari ya kutaka kujiimarisha zaidi kwenye field zao

Kwanini nahusianisha na Bima ya Afya kwa wote?

Kumekuwa hakuna mwongozo sahihi wa gharama za matibabu na kumbuka mgonjwa hana namna ya kuhoji gharama atakayotajiwa

Baadhi ya vituo vya afya (zingatia neno "Baadhi") hasa vya serikali unaanza kuhudumiwa kwa kuangaliwa usoni! Kama mwonekano wako sio wa hela hela utakufa wakati wahudumu wanacheza na simu zao na vicheko juu

Hakuna anayejali kuhusu afya yako kama hauna hela. Ukiandikiwa gharama zilizojuu ya uwezo wako hakuna atakayekusikiliza zaidi ya kukupa maneno ya dhihaka

Endapo mfumo wa Bima ya Afya kwa wote ukiwekwa vizuri hiki kichaka cha kutohudumia watu kwasababu ya kukosa hela hakitakuwepo hivyo vitabaki vichaka vichache ambavyo ni rahisi kuwadhibiti hawa watoa huduma za afya

Mgonjwa akirudishwa nyumbani bila kuhudumiwa au akifia hospitali kwa kukosa huduma sababu ya ukosefu wa hela, mtoa huduma anayo room ya kujitetea kuhusu sheria inayomtaka mgonjwa kulipia matibabu
 
Kaa kimachaleee Tanzania yakuendeshwa na matukio vinginevyo mtaendelea kufaa.

Ile pesa inayopotea kila CAG anaposoma yale mapoteo ile BIMA ingeanzishwa mda sana🙏🙏✍
 
Back
Top Bottom