Mwandishi:George Maziku
Kuna harakati kubwa zinaendelea nchini kote kuwachochea wananchi wa imani ya Kiislamu kuwachukia wananchi wenzao wa imani ya kikristo.
Wanaoendesha harakati hizi ni baadhi ya viongozi wa kiislam ambao wanatembea huku na kule nchini kueneza taarifa za uongo dhidi ya wakristo.
Watu hawa wamekuwa wakihutubia misikitini, katika makongamano yao, na kutumia vyombo vyao vya habari, wakieneza madai ya uongo na uzushi kwamba nchi yetu inaongozwa na "mfumo Kristo".
Kwamba serikali ya Tanzania tangu zama za utawala wa awamu ya kwanza wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, imekuwa ikiwapendelea Wakristo katika nyanja mbalimbali za kimaisha huku ikiwabagua Waislamu.
Viongozi hao wa Kiislamu wamekuwa wakitangaza kuwa serikali imekuwa ikifanya upendeleo kwa wakristo na kuwabagua waislam katika utoaji wa huduma za elimu, uteuzi wa viongozi serikalini na taasisi za umma na ajira, ambapo wanadai kuwa nafasi nyingi hupewa Wakristo.
Wanawashambulia na kuwashutumu vikali hayati Mwalimu Nyerere na viongozi wa makanisa ya Kikristo hususan viongozi wa Kanisa Katoliki nchini, kuwa ndio waasisi wa ‘dhuluma' hii dhidi ya Waislam.
Wanazungumza maneno mengi ambayo wanadai kuwa ndio ushahidi wa tuhuma zao dhidi ya serikali na makanisa, na wanahitimisha kwa kuwataka Waislamu kuamka na kupambana kudai haki zao kwa njia na gharama yoyote.
Watu hawa wamekwenda mbali zaidi hata kufikia kuhamasisha machafuko nchini kote, wanasema kuwa kama Wakristo wamemwaga ugali, basi nao wako tayari kumwaga mboga, wakimaanisha kuwa ni bora kusiwe na amani nchini ili tukose wote, yaani asiwepo mtu au kundi la watu wanaofaidi nchi peke yao wakati wengine wakibaguliwa.
Wachochezi hawa wanazunguka kila kona ya nchi yetu wakieneza sumu hii, wanafanya hivyo bila kificho kana kwamba nchi hii haina serikali, naamini viongozi wa ngazi zote wameyasikia matamshi ya watu hawa lakini cha kushangaza hakuna kiongozi yeyote aliyetoa kauli kuwakemea wahusika, sijui wanawaogopa au wanatenda hayo kwa baraka za viongozi wa serikali yetu!
Matokeo ya kauli hizi za uchochezi ni mabaya sana kwa sasa kwani kumeibuka chuki ya kutisha miongoni mwa waislam dhidi ya wakristo hususan katika mikoa ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi hususan Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara
na Morogoro.
Jambo la hatari zaidi ni kwamba propaganda hizi chafu na hatari zimepenyezwa kwenye siasa, Waislamu wengi wa ukanda wa pwani sasa wameshikamana na Chama cha Mapinduzi (CCM) eti kwa sababu kiongozi wake Rais Jakaya Kikwete ni Mwislamu.
Waislamu hawa sasa wananadi kuwa hizi ni zama za Waislamu kutawala nchi, wanauchukulia uongozi wa rais Kikwete kama utawala wa Waislamu, wanamsifia kuwa ameleta uwiano mzuri wa mgawanyo wa fursa za uongozi, ajira na nafasi za elimu kati ya Wakristo na Waislamu.
Waislam wengi sasa wamegeuka walinzi na watetezi wa serikali ya Rais Kikwete, wanaamini kuwa wote wanaompinga na kumkosoa ni Wakristo ambao wanaona kawakatia mirija yao ya kuendelea kuwakandamiza na kuwanyanyasa Waislamu.
Waislamu hawa wa ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi wengi wanaamini kuwa upinzani mkali dhidi ya serikali ya Rais Kikwete unaoendeshwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni njama za viongozi wa makanisa hususan Kanisa Katoliki ambao hawampendi Rais Kikwete kutokana na uongozi wake unaojali haki za Waislamu.
Kwa msingi huo, Waislamu wameihukumu CHADEMA kuwa ni chama cha Kikristo, kwamba ni chama cha Wakatoliki, wameshiba propaganda za uongo na uzushi za CCM zilizoanza mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.
Kwa hakika huu si mwelekeo mzuri kwa taifa letu, tunajenga mazingira hatari yatakayoiangamiza nchi yetu katika siku za usoni, tunaichimbia kaburi amani ya nchi yetu, tunaandaa vita ya kidini ambayo itasababisha mauaji ya kiholela ya wenyewe kwa wenyewe.
Athari za chuki kati ya Waislamu na Wakristo tayari zimeanza kuonekana wazi, tumesikia mapigano kati ya Waislamu na Wakristo yaliyotokea wiki iliyopita huko Mto wa Mbu, mkoani Arusha, yaliyosababishwa na mihadhara ya kashfa ya kidini ambayo imekuwa ikiendeshwa na makundi ya Waislamu na Wakristo ambayo tumehadharisha kwa muda mrefu kuwa ni hatari na sumu kwa amani ya nchi yetu.
Uhasama huu wa kidini hauwezi kumnufaisha yeyote, si Waislamu wala Wakristo watakaofaidika na hali hii, wote tutapata hasara, na bahati mbaya uhasama huu utawakumba hata wasiokuwa wafuasi au waumini wa dini hizi na hata wasiokuwa na dini, wote tutapata hasara kubwa.
Pia napenda kuionya serikali na chama tawala - CCM kwamba hamtabaki madarakani milele kwa kuchochea mitengano na machafuko baina ya wananchi, njia pekee ya kurudisha imani ya wananchi kwenu na hivyo kuendelea kutawala ni kuwahudumia watu kwa uaminifu na uadilifu, kuondoa kero zao za kila siku, kuboresha maisha yao, na kuwawezesha kuishi maisha yenye hadhi ya binadamu, huo ndio ‘uchawi mtakatifu' wa kisiasa. Mwenye masikio na asikie.
KUNA harakati kubwa zinaendelea nchini kote kuwachochea wananchi wa imani ya Kiislamu kuwachukia wananchi wenzao wa imani ya kikristo.

Source: Tanzania Daima
Kwa mwendo huu hatutafika, serikali kimya inasubiri CDM waandamane ndio waanze kuongea na kukemea, lakini hawa wenzangu wanachofanya sio sahihi kabisa labda ni sahihi kwa JK peke yake.