Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 524
Wiki iliyopita sikufanikiwa kutazama kipindi cha PAMBANUA ambacho hurusha na TV ya Channel TEN.
Jana nilipata bahati ya kuangalia marudio ya kipindi hicho ambapo Mtangazaji wa Channel TEN alikuwa akizungumza na Wanaharakati watatu mmoja wao akiwa Ndg. Lugemeleza Nshala, Mwanasheria na Mwanaharakati machachari wa Mazingira wa Legal and Enviroment Association of Tanzania (LEAT). Walikuwa wakizungumzia Mikataba ya Kifisadi ambayo Serikali yetu imeingia na Wateketezaji (Wawekezaji?) na walielezea namna ambavyo nchi imeingizwa kwenye mikataba hatari inayomkamua ng'ombe wetu aliyekonda (Tanzania). Walielezea kuhusu Mkataba wa Biwater na DAWASCO na jinsi wao (LEAT) kama wanaharakati walivyoishinikiza serikali na kusaidia kuvunjwa kwa mkataba huo.
Katika moja ya maeloezo yake alielezea jinsi anavyoshangazwa na Serikali ya Tanzania kutotaka kuvunja Mkataba huo wa Kifisadi wakati katika mkatba hu ambao wao (LEAT) wanao, kuna kipengele kinasema kuwa Serikali ya Tanzania itakuwa na haki ya kuuvunja mkataba huo iwapo itatokea pande mgogoro kati ya Wana-hisa wa IPTL ambao mmoja wao atampeleka mwenzake Mahakamani.
Ndg. Nshala alisema anashangazwa kuwa Serikali haitaki kuuvunja Mkataba huo wa Kifisadi (Tukumbuke kuwa Serikali inataka kuinunua IPTL) kwa kutumia kifungu hicho kilichopo kwenye Mkataba huku ikifahamika wazi kuwa mmoja wa Wanahisa yaani VIP Ltd (kampuni ya KiTanzania iliyoingia ubia na Wamalaysia) wamewafikisha Wabia wenzao (Malaysia) Mahakamani. LEAT wanashangaa kwanini serikali haitaki kutumia kipengele hicho kuuvunja Mkataba huo na IPTL (LEAT wana nakala ya Mkataba huo kwa mujibu wa Nshala). Na wako tayari kusaidia ili mkataba huo uvunjwe.
My Take:
Wadau, au kuna mkono wa mtu ambaye bado Watz hawajamfahamu kwenye Mkataba huo? Maana Mkataba na Dowans umevunjwa labda ni kwa kuwa tumeshamfahamu Dowans ni nani. KULIKONI Serikali yetu?
"WATANZANIA SI MABWEGE TENA" Dk. Mwakyembe (Mb)