Serikali Haitaki Kuvunja Mkataba na IPTL!- LEAT

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Wiki iliyopita sikufanikiwa kutazama kipindi cha PAMBANUA ambacho hurusha na TV ya Channel TEN.

Jana nilipata bahati ya kuangalia marudio ya kipindi hicho ambapo Mtangazaji wa Channel TEN alikuwa akizungumza na Wanaharakati watatu mmoja wao akiwa Ndg. Lugemeleza Nshala, Mwanasheria na Mwanaharakati machachari wa Mazingira wa Legal and Enviroment Association of Tanzania (LEAT). Walikuwa wakizungumzia Mikataba ya Kifisadi ambayo Serikali yetu imeingia na Wateketezaji (Wawekezaji?) na walielezea namna ambavyo nchi imeingizwa kwenye mikataba hatari inayomkamua ng'ombe wetu aliyekonda (Tanzania). Walielezea kuhusu Mkataba wa Biwater na DAWASCO na jinsi wao (LEAT) kama wanaharakati walivyoishinikiza serikali na kusaidia kuvunjwa kwa mkataba huo.

Katika moja ya maeloezo yake alielezea jinsi anavyoshangazwa na Serikali ya Tanzania kutotaka kuvunja Mkataba huo wa Kifisadi wakati katika mkatba hu ambao wao (LEAT) wanao, kuna kipengele kinasema kuwa Serikali ya Tanzania itakuwa na haki ya kuuvunja mkataba huo iwapo itatokea pande mgogoro kati ya Wana-hisa wa IPTL ambao mmoja wao atampeleka mwenzake Mahakamani.

Ndg. Nshala alisema anashangazwa kuwa Serikali haitaki kuuvunja Mkataba huo wa Kifisadi (Tukumbuke kuwa Serikali inataka kuinunua IPTL) kwa kutumia kifungu hicho kilichopo kwenye Mkataba huku ikifahamika wazi kuwa mmoja wa Wanahisa yaani VIP Ltd (kampuni ya KiTanzania iliyoingia ubia na Wamalaysia) wamewafikisha Wabia wenzao (Malaysia) Mahakamani. LEAT wanashangaa kwanini serikali haitaki kutumia kipengele hicho kuuvunja Mkataba huo na IPTL (LEAT wana nakala ya Mkataba huo kwa mujibu wa Nshala). Na wako tayari kusaidia ili mkataba huo uvunjwe.

My Take:
Wadau, au kuna mkono wa mtu ambaye bado Watz hawajamfahamu kwenye Mkataba huo? Maana Mkataba na Dowans umevunjwa labda ni kwa kuwa tumeshamfahamu Dowans ni nani. KULIKONI Serikali yetu?

"WATANZANIA SI MABWEGE TENA" Dk. Mwakyembe (Mb)
 
Wanasheria wa serikali hawafanyi kitu hata kama kinawezekana unless kama kuna kickbacks(kitu kidogo). Sio kwamba hawawezi kuuvunja mkataba huo bali ni nani anafaidika wakiuvunja. Uzaendo ndugu yangu haupo.

Hawa jamaa wa LEAT(Lawyer's Environmental Action Team na sio Legal and Environment Association of tanzania) ni wanaharakati wazuri tena wana data za kutosha. Mimi nawaamnini lakini je, serikali itawaamini? na je, hata ikiwaamini watakubali? Sio rahisi, labda wabunge wawape kibano bungeni
 
Serikali iliyokuwepo haifai kuwepo madarakani hata dakika mbili ,hii ni serikali ya kufanyiwa maandamano nchi nzima ili ijiuzulu ,sababu zipo kabakaba.

Ole wao bado demokrasia Tanzania inahesabika ni changa ,lakini kwa makosa yaliotokea ya Raisi aliekuwepo madarakani kutubadilishia Mawaziri kila baada ya wizi shutuma kutuhumiwa ,huku ni kukosa muelekeo na dira kwa Serikali iliyopo madarakani ,sasa imekuwa nchi inaendeshwa kwa kubahatisha au na raisi wetu imekuwa ni mtu anaecheza au kuchezesha bahati nasibu.

Alimuradi anamaliza miaka yake kumi kupata au kukosa ndilo linaloonekana kutumainiwa na Raisi wetu,na sio utekelezaji ambao aliwaahidi waTanzania ambao wengi walinunulika kwake kwa bei poa kwa lambalamba ambazo alikuwa akizinadi pia naweza kusema WaTanzania wengi waliweka matumaini makubwa sana na kuamini kabisa kwamba Mh.Kikwete ameelekea kumaliza tatizo japo kwa asilimia 50 ya shida za waTanzania.

Naweza kusema hata uchaguzi huu kama ungeendeshwa kwa haki na usawa basi upande wa kura za Uraisi Kikwete angewawacha wapinzani wake kwa mbali hili sina mbadala nalo kwani naamini kabisa WaTanzania wengi walikuwa wanampenda huyu jamaa kama anavyopendwa Seif Sharif na WaZanzibari,ila kwa upande wa Kikwete mambo yamekwenda yasivyotegemewa imani naupendo umeanza kutoweka na kuyoyomea kusiko julikana ,wananchi wameanza kukata tamaa na kauli yake ya mwisho ilisema kuwa watu wajifunge mikanda ndio iliyowaporomosha na kuwaweka raia chini na mikono wameshika tama, wananchi wanaona wamekatishwa tamaa waliyokuwa nayo kwa asilimia 79 ,na iliyobaki ndio bahati nasibu ya Raisi tulie nae.
 
Back
Top Bottom