Serikali haina mpango wa kufunga Maduka ya dawa ya watu binafsi

Serikali haina mpango wa kufunga Maduka ya dawa ya watu binafsi

Wasiwasi waniniii..

Tulieni na muwe watulivu watu wamejipanga na wanaendelea kujipanga, wapeni muda MSD, Huu utawala si ule dhaifu..
hapa kaziiTu..

Jana kuna jamaa yangu alienda kununua dozi pale ya Bi mkubwa wake. Imagine dawa iliyokuwa inauzwa nje elfu 46 ndani duka la msd linauza kwa sh elfu 12. Sielewi watu kwa nini hawaappreciate vitu kama hivi.
 
Huu mradi hautoendelea,haya maduka si baada ya muda yatauza "Hamna dawa" na watu watalazimika kurudi kununua dawa katika maduka ya private. Hili suala lilitakiwa kufanyiwa utafiti wa kitaalamu, kujua vipi mradi huu utekelezwa ili utoe huduma wakati wote, huku ukihakikisha halikosi dawa muda wote na utoe huduma nchi nzima, sasa kuanzisha kuamua kuutekeleza mradi mkubwa kama huu katika muda wa wiki mbili, ambao sidhani kama umefanywa utafiti wa kutosha kuna wasiwasi kama utaweza toa huduma nzuri.

Utafiti wa kitaalam, mchakato, upembuzi yakinifu, bado kuna changamoto ya blah blah blah. Acha watu watatue kero za wananchi hakuna jema mtalofanyiwa mridhike labda kuzungusha mikono.
 
Inatia kichefufu mbona serikali haieleweki
 
Umeonaa eeh.. iv km msd wanaweza kusupply kwenye hayo maduka.kwa nn isifanye hvy kweny hzo hospital? badala vduka
 
Mimi jana tarehe 2 nilikuwa na kijana wangu mgonjwa. alitibiwa Muhimbili Private (Fast Track). Nilipoandikiwa dawa nilikwenda kununua kwenye duka la MSD ambalo lipo pale Muhimbili opposite na ile garden iliyo karibu na MOI private. Nilishangaa bei zao. Kuna dawa mtaani inauzwa 5000/= na kuendelea, lakini pale nimenunua kwa shilingi 500/= tu. Sikuamini kwani ilibidi nimuulize muuzaji asije akawa amekosea. Akaniambia hajakosea ndiyo bei zao. Nawashauri muyatumie hayo maduka kwa kweli yanasaidia sana. La Muhimbili limefunguliwa tangu juzi tarehe 1. Asante sana Magufuli Mungu akubariki na kukulinda.
 
Back
Top Bottom