Serikali haina mpango wa kufunga Maduka ya dawa ya watu binafsi

Serikali haina mpango wa kufunga Maduka ya dawa ya watu binafsi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,930
Reaction score
63,673
Serikali imesema haitayafungia maduka ya dawa ya watu binafsi yaliyopo pembezon mwa Hospitali za Umma kwa kuwa maduka hayo yameanzishwa kisheria.

Ili kuhakikisha wagonjwa wanaofika kwenye hospitali za Umma hawaendi kununua dawa kwenye maduka binafsi, serikali imesema itaendelea na mkakati wake wa kuboresha maduka ya dawa yanayofunguliwa na Bohari ya Dawa MSD kwenye hospitali zake, na kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua duka la dawa linalomilikiwa na Bohari ya Dawa MSD, duka lililopo Ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa upande wake uongozi wa MSD umesema baada ya ufunguzi wa Duka hilo la dawa, mkakati uliopo kwa sasa ni kufungua maduka hayo kwenye hospitali za Rufaa za Kanda kwenye mikoa ya Mwanza na Arusha, huku hospitali nyingine za rufaa zilizo na maduka ya dawa zikiongezewa uwezo kwa kupewa dawa zaidi.

Duka la Dawa la MSD kwenye Hospital ya Muhimbili ni duka la pili kuzinduliwa na Bohari ya Dawa baada ya lile la Mbeya. Duka hilo la Muhimbili ambalo limeanza na kuuza aina 450 ya dawa tofauti, linatarajiwa kuongezewa uwezo hadi kufikia kuuza aina 2000 ya dawa za binadamu.

 
Last edited by a moderator:
Hatimaye serikali imesema kuwa haitofunga maduka ya dawa mbali na MSD kufungua maduka hayo kila hospitali kubwa nchini.

Hayo yamesemwa leo na katibu mkuu wizara ya afya wakati akizindua duka la dawa la serikali lililofunguliwa hospitali ya taifa Muhimbili.

My take
Tuliweka wazi jinsi mchakato wa upatikanaji dawa nchini ulivyo na tukaishauri serikali ni bora ikaingia kwenye ushindani huku ikianza mchakato wa kujitosheleza kwa kuanza kuzalisha dawa na kuingia ubia na baadhi ya viwanda. Pia ianzishe viwanda vyake na siyo kufunga maduka binafsi.

Tutaendelea kuishauri kwa kadiri tuwezavyo!
 
Alikuwa aendelee tu kulala huyu mwenyekiti, kufuli inakuja kufunga mlango
 
Huu katibu mkuu ni Kilaza. Nadhani Dr. Magufuri anawachora watu kama hawa kwani yeye ndiye alikurupuka kusema yanafungwa. Watu wasiojiamini utawajua tu.
 
Sijaelewa, ina maana ya watu binafsi yanabakia na hapo hapo ya MSD yanafunguliwa?
 
Kelele nyingii,Mwisho wa siku hakuna hata moja la maana alilofanya.makontena yamelipiwa kodi kumbe.
 
Ndo dunia ya utandawazi hiyo. Usimnyime mtu kufanya choice aitakayo. Kuna brands nyingi za dawa na serikali haitaweka zote ila maduka binafsi yanazo.
 
Sijaelewa, ina maana ya watu binafsi yanabakia na hapo hapo ya MSD yanafunguliwa?

Ndiyo maana yake.
Kwa sababu kuna dawa ambazo huwezi kuzipata kwenye bohari ya MSD.

Kama Serikali inarudi kufanya biashara kwa kiwango hicho na ikazuia Watu binafsi kufanya biashara ya dawa
pembezoni mwa Hospitali, tusubiri RTC mpya na ulanguzi. Lakini kwa uamuzi huu wa kuwaachia Watu binafsi kufanya biashara hapo angalau ni uamuzi wa busara.
 
Huu katibu mkuu ni Kilaza. Nadhani Dr. Magufuri anawachora watu kama hawa kwani yeye ndiye alikurupuka kusema yanafungwa. Watu wasiojiamini utawajua tu.

Huyu jamaa sijui kama hatamaliza miezi miwili maana miongoni mwa watu wanaokula 10% za manunuzi ya dawa na vifaa tiba kutoka msd, naona anajichanganya ili asikumbwe na hili panga
 
Serikali imesema haina Mpango wa kuyafunga maduka ya dawa ya watu binafsi yaliyo Karibu na Hospitali kwani yapo Kisheria.

Imesema itaendelea na Mkakati wake wa Kuboresha maduka ya dawa yaliyofunguliwa na MSD kuhakikisha watu wanapata madawa kwa bei nafuu. Hadi sasa yameshafunguliwa Maduka mawili ambayo ni Muhimbili na Mbeya. MSD wamesema watafungua Maduka ya Dawa Kikata kwenye Hospitali za Rufaa na hadi january watakua wamemaliza

Prof.Idrisa Mtula Mwenyekiti wa Bodi ya MSD.
Huu mradi hautoendelea,haya maduka si baada ya muda yatauza "Hamna dawa" na watu watalazimika kurudi kununua dawa katika maduka ya private. Hili suala lilitakiwa kufanyiwa utafiti wa kitaalamu, kujua vipi mradi huu utekelezwa ili utoe huduma wakati wote, huku ukihakikisha halikosi dawa muda wote na utoe huduma nchi nzima, sasa kuanzisha kuamua kuutekeleza mradi mkubwa kama huu katika muda wa wiki mbili, ambao sidhani kama umefanywa utafiti wa kutosha kuna wasiwasi kama utaweza toa huduma nzuri.
 
Ndiyo maana yake.
Kwa sababu kuna dawa ambazo huwezi kuzipata kwenye bohari ya MSD.

Kama Serikali inarudi kufanya biashara kwa kiwango hicho na ikazuia Watu binafsi kufanya biashara ya dawa
pembezoni mwa Hospitali, tusubiri RTC mpya na ulanguzi. Lakini kwa uamuzi huu wa kuwaachia Watu binafsi kufanya biashara hapo angalau ni uamuzi wa busara.

Kibiashara na kiuchumi ni uamuzi mzuri, ila kwa nia ya kutatua zile kero za madawa na kupigwa bei za kufa mtu, bado kutakuwa pale pale, tuko hapa tutapashana mrejesho
 
Hapo jambo la kuwa nalo makini ni hujuma maana itakuwa ndio zile "panadol zimeisha lakini nenda paleee kwa mkinga utapata" . Dawa zitakazobaki MSD itakuwa ni hamna, zimeisha, hizo sina, pamoja na zimebaki nusu dozi!
 
hata ingekuwa wanataka kuyafunga hawana hata chembe ya nguvu kisheria , tumewashauri wasome sheria ya famasi ya 2003 ( pharmacy act - 2003 ) nadhani wamechungulia wameona moto kudadeki ! mtafungwa !
 
Hapo jambo la kuwa nalo makini ni hujuma maana itakuwa ndio zile "panadol zimeisha lakini nenda paleee kwa mkinga utapata" . Dawa zitakazobaki MSD itakuwa ni hamna, zimeisha, hizo sina, pamoja na zimebaki nusu dozi!

ni hivi , msd haina uwezo wa kuwa na paracetamol ya aina nyingine zaidi ya sheladol , ukiwaambia wakupe calpol mara zote watakuambia hawana , unategemea nini ?
 
Wasiwasi waniniii..

Tulieni na muwe watulivu watu wamejipanga na wanaendelea kujipanga, wapeni muda MSD, Huu utawala si ule dhaifu..
hapa kaziiTu..
 
Safiiiii Sanaa sasa duka langu lililopo amana litaendelea kuwepo
 
Back
Top Bottom