Sergio Busquets atangaza kustafu soka mwishoni mwa msimu

Sergio Busquets atangaza kustafu soka mwishoni mwa msimu

Meja Jenerali Isamuhyo

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
3,680
Reaction score
10,846
Hatimae kiungo bora mkabaji wa muda wote, Segio Busquets ametangaza kustaafu soka kufikia mwisho wa msimu.

Busquets ambaye huwa anacheza kiungo mkabaji, amefikia uamuzi huo katika umri wa miaka 37.

Ni mshindi wa Kombe la Dunia la mwaka 2010 akiwa na Timu ya Taifa ya Spain katika fainali zilizofanyika South Africa.

Ametwaa mataji 36 katika career yake ya soka.

Shukrani kwa kocha Pep Guardiola aliyemuibua kutoka team za vijana na kumpa nafasi kwenye kikosi cha wakubwa. Anakumbukwa kwa kuunda muunganiko wa yeye, Xavi na Iniesta katika eneo la kiungo cha Barcelona na Spain kuzitesa team nyingi sana.

Busquets alileta mapinduzi ya namna ya kucheza namba 6 bila ya matumizi ya nguvu kamaa ilivyokuwa imezoeleka awali.

Huyu ndio role model wa akina Rodri na viungo wa kariba hiyo.

Aliyekuwa kocha wake wa Spain, Vicente Del Bosque aliwahi kunukuliwa, “ ukitazama mechi huwezi kumuona Busquets ila ukimtazama Busquets utaona mtiririko mzima wa mechi”.

Pengine dunia haitokuja kumpata Sergio Busquets mwingine. Hakika ulikuwa wasaa mzuri sana kumshuhudia Busquets akicheza.
 
Back
Top Bottom