Choga Cosmasy
Member
- Feb 8, 2017
- 18
- 32
Nashangaa wakati huu timu ya taifa vijana imefuzu michuano ya afcon kila mtu yupo kimya na hakuna anayeona mafanikio ya Malinzi.
Kwa hiki kilichofanyika isitoshe kuona Jamal si mtu sahihi katika maendeleo ya soka.
Nimeshangaa kuona hakuna taarifa nyingi za timu yetu kufuzu afcon ya vijana katika vyombo vya habari,lakini taarifa nyingi za kukosea kwa TFF ndizo zinazosikika.
Kauli hizo zilitolewa na Eliud Mvela katika uchaguzi huko Kilimanjaro, baada ya kusoma tu iliniduwaza sana mimi Choga nabaki najiuliza hivi ni nani aliyemwambia Mvela zuri moja linafuta maovu yote?
Hivi ni nani aliyemwambia ukifeli somo moja na kufaulu matatu basi hupaswi kusemwa?, Mvela nikwambie tu kufuzu kwa Serengeti boys sio kwamba ndio Tanzania imefanikiwa kisoka.
Aliyeiloga Tanzania kafa hapa ndipo tunapotea zaidi,ukweli ni kwamba mchawi wa soka letu ni uvivu wa kufikiri na sio mwingine.
Kwanza inawezekana vipi mtu mmoja awepo kwenye chaguzi zaidi ya mbili tena katika mikoa tofauti? ,hainiingii akili kabisa katika hili.
Ni kweli Serengeti boys imefuzu lakini unabaki unajiuliza tu hayo aliyoyasema tena katika uchaguzi yanamantiki ipi zaidi ya kampeni tu ya uchaguzi mkuu?, tunataka kuuaminisha umma wa wanamichezo kuwa tumefaulu wakati si kweli.
TUTAFAKARI UPYA.