masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,171
NEMC , National Enviromental Management Council, ni chombo kinachohusika na kuangalia masuala yote yanayohusiana na mazingira nchini.
Tunajua NEMC ina husika na masuala mengine mengi lakini katika hili la mito(rivers) hasa inayokatiza jiji la Dar es saaam, maamuzi yao hayajakuwa na tija na kwa ujumla yamelitia Taifa hasara kubwa.
Tukisema Baraza hili la Mazingira lina neno "Management" ndani yake, basi hatujaona management yenye maana yoyote Zaidi ya kufukuza wachimba michanga mabondeni.
Tungetegemea NEMC ingekuja na utaratibu maalum wa jinsi , mosi, kuweka sera endelevu za upandaji miti kando kando ya mito pamoja na protection ya kingo za mito.
Pili, ya kuondoa mchanga katika mito, mchanga ambao umesababisha kina cha mito mingi kupungua sana na kusababisha madaraja kukatika na mito kujaa sana.
Sitaliongelea la mto Msimbazi, maana huo ni mfupa ambao ka sasa hata NEMC hawana ubavu wa kulifikiria utatuzi wake.
Tumeshuhudia mto Mpiji kukata kingo za daraja la Mpiji, na barabara kutopitika karibu siku tano.
Tumeona daraja la Kawe( maarufu kwa Malecela) likikatika kabisa na kuhitaji matengenezo makubwa.
Laiti michanga ingeondolewa kwa utaratibu unaoeleweka kama hatua zilivyochukuliwa na vyombo vingine hivi sasa, hasara kubwa tulizo shuhudia zingeweza kuepukika.
(daraja la Kawe mchanga ukitolewa sasa kuongeza kina cha mto)