Hili ilitokea majuzi tarehe 20/2/2016 katika shule ya msingi chemchem iliyoko kata ya Igawilo jijini Mbeya baada ya mlinzi wa shule kudondoka ghafla na kufariki akiwa lindoni usiku kwa kufia kazini watu walipatwa na uchungu na kusema ni sawa na askari aliyefia vitani anapaswa kupewa heshima ndipo waliamua kuwaambia wanafunzi wakaombe mchango wa rambirambi ili kwenda kuhani msiba huo huku waalimu wakichangishana sh 3000@. Mwalimu mkuu wa shule hiyo alipinga wazo hili akidai anaogopa rungu la magufuli na kupoteza ajira yake na akaamua kupiga simu kwa afisa elimu jiji na afisa huyo akaagiza hakuna kuchangishana shuleni kama kuna watu wanataka kuchangishana juu ya msiba huo wawe waalimu wawe wanafunzi wawe nani? basi wakakutane nje na eneo la shule.Timbwili likaibuka wajumbe wa kamati ya shule wakasema hawaoni dhamani ya kufanya kazi shuleni hapo ikiwa hata wakifa hawatadhaminiwa na wanafunzi wao na jamii kwa ujumla kwa kisingio cha magufulism Tafadhali sana serikali itoe ufafanuzi hata misiba ni marufuku wanafunzi kwenda kuhani kwa kutoa chochote na je? tunawajenga vipi? watoto hawa kuna hatari wakiwa wakubwa hata misibani hawatakuwa wanaenda!