Waziri TAMISEMI: Hakuna sheria Inayompa mamlaka RC kumchapa mwanafunzi; Rais Magufuli: Nampongeza RC Mbeya kuwachapa wanafunzi

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo amesema hakuna kanuni/sheria inayompa mamlaka RC kumchapa mwanafunzi yoyote yule viboko kwani mwongozo wa uendeshaji wa elimu umetoa utaratibu wa adhabu kwa wanafunzi. Jafo amesema bado anasubiri taarifa ya RC wa Mbeya kuhusu tukio hilo.

Rais Magufuli
Nilikuwa nazungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, nikamwambia ulitakiwa uwatandike viboko kwelikweli na uwafukuze shule, na natangaza hapa kuwa wale wanafunzi wote wamefukuzwa Shule na bodi ile imevunjwa kwasababu ni uzembe wa bodi mpaka mambo yale yametokea.

Nampongeza RC Mbeya, ila kwa wale watoto waliotimuliwa shuleni lazima wazazi wao walipe, nasema haya sio kwa sababu sina huruma nimeshawahi kuwa mwalimu, nawaomba wazazi nafikiri kuna mahali tumekosea ni sheria kuhusu viboko.

Je, tumfuate nani?
1. Wateule?
2. Rais?
3. Katiba/Sheria?
 
Jafo kasema lini hayo? Je ni baada ya Mh. Rais kuongea au kabla? Uwe makini unapoleta taarifa kama hii, time is the biggest factor hapa, kuna sheria ndio, ila Mh. Rais ana uwezo wa kupindua sheria fulani kwa tukio fulani na mazingira husika.. Je Jaffo alisema baada au kabla ya Mh. Rais kusema?
 
Kama mukulu kasema basis tumemaliza
Wadogo tushawatimua skuli,hakuna namna,olle wake MTU apinge kauli ya mukulu
 
Tumeshalalamika humu. Awe huyo waziri amesema kweli au ni taarifa ya uongo, bado tunasimamia pale pale; nchi inatakiwa iendeshwe kwa mujibu wa sheria, katiba na taratibu zilizowekwa.

Haiwezekani kila jambo kuamuliwa na mamlaka kutoka juu! Sasa hawa waliopewa mamlaka ya ngazi za chini watafanya kazi gani? Awamu hii wateule wanajitahidi kutafuta kiki hata kwa kuingilia majukumu ya watu wengine.
 
Jambo likitokea ni bora wasubirie kauli ya mkuu wa nchi tu

Ova
 
Jafo kasema lini hayo? Je ni baada ya Mh. Rais kuongea au kabla? Uwe makini unapoleta taarifa kama hii, time is the biggest factor hapa, kuna sheria ndio, ila Mh. Rais ana uwezo wa kupindua sheria fulani kwa tukio fulani na mazingira husika.. Je Jaffo alisema baada au kabla ya Mh. Rais kusema?
Swala ni sheria inasema nini na si habari ya Magu kasema nini kwani yeye kama Raisi ndio anapaswa kuwa mfano wa kuheshimu utawala wa sheria na si vinginevyo.

Magu hatoshi kwa nafasi aliyoshikilia na hatufai.
 
Jafo kasema lini hayo? Je ni baada ya Mh. Rais kuongea au kabla? Uwe makini unapoleta taarifa kama hii, time is the biggest factor hapa, kuna sheria ndio, ila Mh. Rais ana uwezo wa kupindua sheria fulani kwa tukio fulani na mazingira husika.. Je Jaffo alisema baada au kabla ya Mh. Rais kusema?
Rais hana mamlaka ya kupindua sheria jukwaani. Anaweza kuipindua baada ya kutengeneza muswaada ukapelekwa bungeni.
Nyie ndio mnapoteza huyo msukuma mpaka anajihisi ni Mungu
 
Mh. Waziri, Jafo na yeye atupe sheria inayomkataza Mkuu wa mkoa kucharaza wanafunzi viboko, ukizingatia tukio lililofanywa na wanafunzi linahusisha usalama wa watu na mali na Mkuu wa Mkoa ndiye Mwenyekiti wa 'kamati' ya usalama ya mkoa.
 
Ingekuwa ulaya jafo alipaswa kujiuzulu Mara moja, kapishana na bossi wake hadharani.
 
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo amesema hakuna kanuni/sheria inayompa mamlaka RC kumchapa mwanafunzi yoyote yule viboko kwani mwongozo wa uendeshaji wa elimu umetoa utaratibu wa adhabu kwa wanafunzi. Jafo amesema bado anasubiri taarifa ya RC wa Mbeya kuhusu tukio hilo.

Rais Magufuli
Nilikuwa nazungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, nikamwambia ulitakiwa uwatandike viboko kwelikweli na uwafukuze shule, na natangaza hapa kuwa wale wanafunzi wote wamefukuzwa Shule na bodi ile imevunjwa kwasababu ni uzembe wa bodi mpaka mambo yale yametokea.

Nampongeza RC Mbeya, ila kwa wale watoto waliotimuliwa shuleni lazima wazazi wao walipe, nasema haya sio kwa sababu sina huruma nimeshawahi kuwa mwalimu, nawaomba wazazi nafikiri kuna mahali tumekosea ni sheria kuhusu viboko.

Je, tumfuate nani?
1. Wateule?
2. Rais?
3. Katiba/Sheria?
Kwa ukubwa wa kosa lenyewe lazima hawa watoto walichapwa na wazazi wao majumbani mwao mara walipofika rasmi makwao kama raia huru.
 
Back
Top Bottom