Sera za muungano za chama cha CHADEMA hizi hapa

Sera za muungano za chama cha CHADEMA hizi hapa

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
858
Reaction score
131
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF) vimewasilisha maoni kwa tume ya Mabadiliko ya Katiba vikitaka madaraka ya Rais yadhibitiwe pamoja na kutaka Muungano wa serikali tatu.

MAPENDEKEZO YA CHADEMA

Chadema jana kiliwasilisha mapendekezo kadhaa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba; mojawapo kikitaka kuwapo kwa mfumo wa shirikisho wa serikali tatu kwenye Katiba Mpya.

Katika mfumo huo, Chadema kinataka kuwapo kwa Serikali ya Tanganyika na Zanzibar, ambazo kila moja itakuwa na mamlaka kamili ya Rais, Bunge na Mahakama, na kuwapo pia kwa Serikali Ndogo ya Muungano.

Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Chadema iliyokutana na Tume hiyo jana, Tundu Lissu, alisema katika mapendekezo waliyoyawasilisha kwa Tume, wanataka Rais wa Serikali ya Muungano achaguliwe na wabunge wa Bunge la Tanganyika.

Pia achaguliwe na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, magavana, mameya na wenyeviti wa halmashauri za wilaya.

Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya sekretarieti yake kukutana na Tume hiyo jana.

Wajumbe wengine waliounda sekretarieti hiyo, ni Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai); Zitto Kabwe (Naibu Katibu Mkuu Chadema Tanzania Bara na Mbunge wa Kigoma Kaskazini) na John Mnyika (Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Chadema na Mbunge wa Ubungo).

Wengine ni Said Issa Mohammed (Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar); Hamad Mussa Yussuf (Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar); John Mrema (Mkurugenzi wa Halmashauri na Masuala ya Bunge Chadema) na Profesa Kulikoyela Kahigi (Mbunge wa Bukombe).

Lissu alisema katika mapendekezo yao, wanataka kuwapo kwa pande mbili za Muungano haki ya kujitoa kwenye Muungano kwa sharti kwamba, wanaotaka hivyo, wapige kura ya maoni.

Alisema pia wanataka yabaki mambo saba pekee, ikiwamo linalohusu ulinzi na usalama katika Serikali ya Muungano.

Lissu alisema wanataka Rais wa Muungano akae madarakani kwa miaka mitano ingawa anaweza kuongezewa muda, lakini kuwapo na utaratibu wa kupeana zamu za urais kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Alisema Rais huyo pia ndiye atakayekuwa na mamlaka ya kutangaza vita, lakini ataruhusiwa kufanya hivyo baada ya kupata kibali cha Bunge na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Katika mapendekezo yao mengine, alisema wanataka kinga ya mashtaka ya jinai dhidi ya Rais iondolewe, na pia kuwapo na udhibiti mkubwa wa mamlaka ya Rais.

Alisema wanataka kila atakayeteuliwa na Rais lazima aombe kazi husika kwenye tume huru za kitaalamu na athibitishwe na Bunge.

Lissu alisema pia wanataka serikali iwe na wizara zisizozidi 18 na zisizopungua 15 na pia Bunge liwe na wabunge 250 na liwapo Bunge la majimbo litakalokuwa na wabunge 50.

Pia alisema katika mapendekezo yao, wanataka kila raia aliyetimiza umri wa miaka 18 awe na haki kuchagua na kuchaguliwa, na kwamba, lile sharti la awali la kutaka anayetaka kugombea urais lazima atimize miaka 40, wanataka lisiwepo.

Alisema pia kuwapo na utaratibu wa kila raia mwenye haki ya kupiga kura apige kura awe ndani au nje ya nchi, au awe huru au amedhibitiwa na vyombo vya dola.

Lissu alisema pia wanataka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) isiteuliwe na Rais kama ilivyo sasa, badala yake wanataka iwe tume huru yenye wajumbe 25.

Alisema katika wajumbe wa tume, 15 wapendekezwe na vyama vyenye uwakilishi katika Bunge na kwamba, wajumbe wengine wa NEC watoke kwenye chama cha mawakili wa Tanganyika, taaluma, taasisi zisizokuwa za kiserikali, vyama siasa, visivyokuwa na uwakilishi bungeni.

Lissu alisema wajumbe hao wakipatikana, watatakiwa kupelekwa bungeni kuthibitishwa na Bunge na kwamba, Mwenyekiti na Makamu wake wa NEC watateuliwa na wajumbe wa tume.

Kuhusu umilikaji wa rasilimali, alisema wanataka Katiba Mpya itamke kwamba, maliasili ni mali ya wananchi na kwamba, kama wananchi hawatatoa ridhaa isichukuliwe.

Pia alisema pia wanataka malipo ya mrahaba yapelekwe kwenye maeneo yaliko madini ili wananchi wanaoishi katika maeneo hayo wapate asilimia 40 walipe kodi na asilimia 60 ibaki serikalini.

Alisema katika mfumo wa utawala, wamependekeza utaratibu wa kuwapo kwa mikoa na wilaya uliorithiwa kutoka kwa wakoloni uondolewe, kwa madai kwamba, mikoa na wilaya zimetengwa kwa misingi ya kabila.

Lissu alisema badala ya mfumo huo, kuwapo na mfumo wa majimbo yasiyopungua 10, ambayo alisema yataondoa ukabila.

Alisema katika mapendekezo yao, badala ya mkoa, wanataka kuwapo Jimbo la Nyanza Magharibi litakalohusisha mikoa ya Kagera, Geita na Shinyanga.

Jimbo lingine alisema liwe la Nyanza Mashariki, ambalo litahusisha mikoa ya Mara, Mwanza na Simiyu; Jimbo la Ziwa Tanganyika (Kigoma, Katavi na Rukwa); Jimbo la Kati (Tabora, Dodoma na Singida); Jimbo la Kaskazini (Kilimanjaro, Arusha na Manyara) na Jimbo la Pwani Kaskazini (Tanga, sehemu ya Pwani na sehemu ya Morogoro).

Jimbo lingine, alisema ni la Mji Mkuu wa Dar es Salaam; Jimbo la Pwani Kusini (Mtwara, Lindi, Mafia, Rufiji na Ulanga) na Jimbo la Nyanda za Juu Kusini (Njombe, Mbeya na Ruvuma).

"Ukigawanya nchi namna hiyo, hakuna jimbo litakuwa na rasilimali zake," alisema Lissu.
Alisema pia wamependekeza kwenye mfumo wa utawala, kusiwapo mtu atakayeshawishi kwa Rais ili ateuliwe.
Pia wamependekeza miji iongozwe na mameya wa kuchaguliwa na kwamba, Katiba Mpya itamke kwamba, Kiswahili ni lugha ya taifa na kitumike katika shughuli zote za kiserikali, na pia miswada na sheria zote viandikwe kwa Kiswahili.

MAPENDEKEZO YA CUF

Nacho CUF kimependekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania apunguziwe madaraka ya kuteua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kwamba kufanya hiyo kutaiwezesha kutekeleza majukumu yake bila kuingiliwa na mtu yoyote.

CUF kimependekeza kuwa mwenyekiti wa NEC pamoja na wajumbe wake wachaguliwe na vyama vya siasa pamoja na Asasi za Kiraia kwa niaba ya wanachi, na sio Rais kuteua mtu yoyote.

Kadhalika, chama hicho kimependekeza kuundwa kwa serikali tatu na kila moja iwe na Katiba yake ili kuondokana na malalamiko ya Muungano yaliyodumu kwa muda mrefu hapa nchini.

Pia CUF kimetaka mkataba uliounda muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar utafutwe popote ulipo ili wananchi wapate fursa ya kuujadili.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba muda mfupi baada ya chama chake kuwasilisha maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Profesa Lipumba alisema chama chake jana kiliwasilisha maoni yao kama walivyofanya wananchi wengine.
"Hili jambo la Tanganyika na Zanzibara kuwa nchi moja halikubaliki kwa sababu kunapotokea kuzungumzia matatizo ya muungano uwakilishi hautoshi," alisema Profesa Lipumba.

"Mapatano ya muungano yalikuwa kwamba kila serikali itakuwa na mamlaka kamil, lakini mambo yasiyo ya muungano na yale ya muungano yaliwekwa chini ya serikali ya Tanganyika," alisema Profesa Lipumba.

Mapendekezo mengine yaliyotolewa na CUF kwa tume hiyo ni pamoja na Katiba kutambua mgombea binafsi kwa kuanzia ngazi ya Diwani, Mbunge na Rais.

Aidha, CUF kilipendekeza kwamba ushindi wa kiti cha urais uanzie asilimia 50 na kwamba mgombea akipata kura chini ya asilimia hizo uchaguzi urudiwe asitangazwe kama mshindi.

Profesa Lipumba kwa niaba ya CUF alisema, wamependekeza kwa tume kusiwepo na uchaguzi mdogo endapo kutatokea tatizo lolote kwa mgombea aliyeshika nafasi hiyo kutenguliwa au kupoteza maisha badala yake nafasi hiyo ichukuliwe na mgombea aliyeshika nafasi ya pili.

Mapendekezo mengine waliyotolewa na CUF ni pamoja na kutaka haki za binadamu kuingizwa katika Katiba pamoja na raslimali za nchi zitambuliwe na kugawanywa kwa usawa.

Alisema wamependekeza kwamba vyama vya siasa viruhusiwe kuungana na kusimamisha mgombea mmoja pamoja watendaji wa ngazi mbalimbali wasiteuliwe na Rais na kushika madaraka mpaka Bunge liwathibitishe.

CUF kilitaja baadhi ya nafasi ambazo Bunge linatakiwa kuzithibitisha kuwa ni pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na, Majaji.

Waliokiwakilisha CUF ni Profesa Lipumba; Naibu Katibu Mkuu Bara, Julius Mtatiro; Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Masoud Hamad; Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa, Mbarala Maharagande; Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa CUF (Juvica), Katani Ahmed Katani na baadhi ya wabunge wa Viti maaalum.

CHANZO: NIPASHE
 
Well said Chadema, ila hoja juu ya umri wa miaka 18 kama sifa na kigezo (kikatiba) ya mtanzania - hasa haki ya kuchaguliwa nafasi ya Urais kidogo haijaeleweka vizuri, je ni kwa hoja kwamba if you are old enough to vote then you are old enough to run for any political office? Au hoja hii ipo based on median age in Tanzania? Au kwamba majority of Tanzanians are under the age of 30? Au kwa sababu nyingine zozote...?

Mtanzania husika anatarajiwa atakuwa amefikia kiwango gani cha elimu na anatakiwa awe na uzoefu kiasi gani katika masuala ya public leadership? In other words, je kuna requirements pia za minimum qualifications (experience ya uongozi) na pia minimum level of education? Is it degree ya kwanza? It is miaka kadhaa ya uzoefu fulani? At what age mtanzania husika anatarajiwa kupata hiyo degree au kukusanya the relevant experience? Au elimu na experience sio vigezo vya msingi?

Chadema needs to approach suala hili la umri na kugombea urais holistically, not in an atomistic manner; Otherwise the age of 35 is more ideal;
 
Naamini ktk muungano wa serikali moja tu! Umri wa urais nafikiri kuna makosa kwenye hili.

Itabidi tuanze kupiga debe umri wa kupiga kura iwe miaka 14 umri wa kumaliza elimu ya msingi ili nao wapate haki ya kuchagua na kuchaguliwa!
 
Mapendekezo ya CHADEMA yanaacha maswali mengi zaidi ya majibu huku mapendekezo ya CUF yakiwa kama yameandikwa na kikundi cha UAMSHO.

Vyama vimeonesha bado havijatambua Mtanzania wa sasa anataka nini na anategemea vyama vifanye nini.

Ama kweli, kama vyama mbadala ndiyo vinakuwa na mapendekezo kama haya, Tanzania bado tuko mbali sana katika demokrasia ya kweli na maendeleo.

Is this April foul's day or I'm just in dream.
 
Mchambuzi

Canada (waziri mkuu) na ufaransa (Rais) umri wa kuchaguliwa ni miaka 18! Sidhani kama wameshawahi kupata mwenye umri huo. Uingereza Waziri Mkuu kijana kabisa alikuwa na miaka 24.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu, naamini ni kutokana na mazingira ya sasa ndani ya nchi yetu kisiasa, kiuchumi na kijamii ndo iliyopelekea mapendekezo ya namna hii kutoka kwenye vyama vikuu vya upinzani. Kisiasa na kiuchumi inaonyesha nchi yetu inayumba sana na hakuna tena utashi wa usimamizi wa misingi ya muungano wetu. Kila mmoja amebaki na watu wake, rafiki zake, jamii yake na wafadhili wake kwa manufaa binafsi na si ya nchi kama tulivyoona waanzilishi wa muungano walivyofanya hapo awali.

Inasikitisha na inakatisha tamaa kwani ndo tulipofikishwa na wenzetu wenye dhamana ya uongozi wa taifa letu kwa pande zote 2 za muungano wa tanganyika na zanzibar.
 
Mapendekezo ya CHADEMA yanaacha maswali mengi zaidi ya majibu huku mapendekezo ya CUF yakiwa kama yameandikwa na kikundi cha UAMSHO.

Vyama vimeonesha bado havijatambua Mtanzania wa sasa anataka nini na anategemea vyama vifanye nini.

Ama kweli, kama vyama mbadala ndiyo vinakuwa na mapendekezo kama haya, Tanzania bado tuko mbali sana katika demokrasia ya kweli na maendeleo.

Is this April foul's day or I'm just in dream.

Pendekeza yako tuone acha kulalamika
 
Vyama vyote viwili vina mapendekezo ambayo ukiyachunguza vizuri yanafanana kwenye mambo ya msingi hasa muungano.madaraka ya Rais.Uteuzi wa viongozi.

Sera za mikoa na wizara at least kwa kuanzia kwa akili yangu yanaonyesha mwanga. Umri si tatizo vyama vitaona kama vinamtu mwenye uwezo wa miaka 18 kuongoza nchi sawa.

Muungano wenye nguvu ni wa nchi moja tu nchi mbili utaleta matatizo pia wa sasa ndo kabisa kila siku malumbano. serikari tatu utasaidia ila nao utakua na matatizo mawazo yangu
 
CDM wamepoteza golden opportunity kwenye suala la MUUNGANO. This is a BOLD TRUTH. CDM huko ZNZ hawana wafuasi wengi hili lazima walitambue. Majority ya wafuasi wa CDM wako Tanganyika. Baada ya kuweka facts hizi wazi, kwanini CDM wamepoteza golden opportunity??

Baada ya chokochoko za mda mrefu za Wazanzibari kuhusu Muungano, Watanganyika wengi wanaona dawa/suluhisho la malalamiko hayo ya Wazanzibari wakati wanachangia ZERO SHILINGI kwenye Muungano, ni kuwa na nchi moja, serikali moja, rais mmoja. Huu ndiyo ungepaswa kuwa msimamo wa CDM.

Kama CDM wangekuja na msimamo huu wange score points huku Tanganyika ambako ndiko base yao ilipo. Lakini pia msimamo huu ungewa udhi wazanzibari WOTE. Lakini CDM they have nothing to loose in Zanzibar. Lakini huo msimamo wa serikali tatu, halafu URAIS wa Muungano uwe wa kupokezana vijiti kati ya Tanganyika na Zanzibar, they have shoot themselves on their feet.
 
Achane ubinafsi,Kwa mara ya kwanza kama mzanzibar kindakindaki nayaunga mkono mapendekezo ya Chadema mia kwa mia
 
Kwa kweli big up vyama vyote vya CUF na CDM mmejaribu kugusa engo zote ambazo ndio zimetufikisha hapa tulipo, Mamlaka ya Raisi, Mfumo wa Serikali, Muungano, Nafasi ya Bunge nk BIG UP! Kazi yao tume sasa kuchambua kwa uzalendo wa hali ya juu. Ntashangaa sana kama maeneo makuu haya yanayopigiwa kelele hayatabadilika kwenye KATIBA! Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Tanganyika
 
Mchambuzi

Canada (waziri mkuu) na ufaransa (Rais) umri wa kuchaguliwa ni miaka 18! Sidhani kama wameshawahi kupata mwenye umri huo. Uingereza Waziri Mkuu kijana kabisa alikuwa na miaka 24.
Ndio maana nikauliza kigezo kwetu ni nini, je ni miongoni mwa vile nilivyotaja? au ni kwa sababu wengine wanafanya hayo kwa mfano ufaransa? Katika muktadha wetu, kigezo cha miaka 18 ni kipi hasa.
 
CDM wamepoteza golden opportunity kwenye suala la MUUNGANO. This is a BOLD TRUTH. CDM huko ZNZ hawana wafuasi wengi hili lazima walitambue. Majority ya wafuasi wa CDM wako Tanganyika. Baada ya kuweka facts hizi wazi, kwanini CDM wamepoteza golden opportunity??

Baada ya chokochoko za mda mrefu za Wazanzibari kuhusu Muungano, Watanganyika wengi wanaona dawa/suluhisho la malalamiko hayo ya Wazanzibari wakati wanachangia ZERO SHILINGI kwenye Muungano, ni kuwa na nchi moja, serikali moja, rais mmoja. Huu ndiyo ungepaswa kuwa msimamo wa CDM.

Kama CDM wangekuja na msimamo huu wange score points huku Tanganyika ambako ndiko base yao ilipo. Lakini pia msimamo huu ungewa udhi wazanzibari WOTE. Lakini CDM they have nothing to loose in Zanzibar. Lakini huo msimamo wa serikali tatu, halafu URAIS wa Muungano uwe wa kupokezana vijiti kati ya Tanganyika na Zanzibar, they have shoot themselves on their feet.

Mkuu hapa naona CDM wametumia busara ya hali ya juu mno, ukichukulia kwamba kwa sasa to be frank ni kwamba hakuna anayeutaka Muungano si Wazanzibar au Watanganyika wote tumechoka. Ila hakuna chama cha siasa kinachoweza kuongea hayo kiuwazi kabisa bila kuundiwa mizengwe ya kuwa eti wanaenda kinyume na BABA wa TAIFA na hawalitakii mema taifa letu! Nimepapenda hapo waliposema kuwa itabidi zipigwe kura za maoni ili kama unataka kujitoa ujitoe kwa kweli wamekata kilimilimi cha UAMSHO! wakipiga domo wataambiwa piga kura ya maoni afu mjitoe maana KATINA inaruhusu, then Tanganyika hao wanaendelea huku wakiwa hwajaadhirika na dhambi ya Uasi!
 
Well said Chadema, ila hoja juu ya umri wa miaka 18 kama sifa na kigezo (kikatiba) ya mtanzania - hasa haki ya kuchaguliwa nafasi ya Urais kidogo haijaeleweka vizuri, je ni kwa hoja kwamba if you are old enough to vote then you are old enough to run for any political office? Au hoja hii ipo based on median age in Tanzania? Au kwamba majority of Tanzanians are under the age of 30? Au kwa sababu nyingine zozote...?

Mtanzania husika anatarajiwa atakuwa amefikia kiwango gani cha elimu na anatakiwa awe na uzoefu kiasi gani katika masuala ya public leadership? In other words, je kuna requirements pia za minimum qualifications (experience ya uongozi) na pia minimum level of education? Is it degree ya kwanza? It is miaka kadhaa ya uzoefu fulani? At what age mtanzania husika anatarajiwa kupata hiyo degree au kukusanya the relevant experience? Au elimu na experience sio vigezo vya msingi?

Chadema needs to approach suala hili la umri na kugombea urais holistically, not in an atomistic manner; Otherwise the age of 35 is more ideal;......

Hata kusingekuwa na kigezo cha umri, mwisho wa siku ni uamuzi wa wananchi wenyewe! Kitu cha kuzingatia hapa ni aina ya demokrasia mnayofuata au ukomavu wa demokrasia inayofuatwa!
 
Kwani ni lazima Zanzibar waendelee kuwa na Baraza la Wawakilishi? Kwa nini na wao sasa wasiwe na bunge?
 
Chadema needs to approach suala hili la umri na kugombea urais holistically, not in an atomistic manner; Otherwise the age of 35 is more ideal;

Mimi sikubaliani kabisa kushusha umri wa mgombea urais, ningependa Rais asiwe chini ya miaka 50 ili awe amepitia sharuba za maisha na anajua uongozi na madaraka ni dhamana ya namna gani. Awe na elimu isyopungua shahada ya pili, utumishi wa umma ndani ya nchi usiopungua miaka 20, mwisho athibitike uraia wake hadi vizazi 4 nyuma.

Pamoja na kura za wote, apigiwe kura za majimbo na aibuke na majimbo asili mia 60.

Pamoja na yote hayo pawepo na high council ya wawakilishi 2 wa vyama vya siasi, wawakilishi 4 madhehebu ya dini, wawakilishi 2 umoja wa NGOs, wawakilishi 2 wa vyama vya wafanyakazi, wawakilishi 2 wa vyama vya wakulima, wawakilishi 2 wa viwanda na mali asili, na wawakilishi 2 Legal institution representation BILA chombo cha dola kuhusishwa. Wasizidi 20 Maazimio yao yawe check and balance ya kumsaidia Rais kwa manufaa ya kuwa kama atakuwa ametokea kutokana na mgombea binafsi apate forum ya maoni ya hao.

Madaraka ya mabunge ya majimbo yawe kamili kuhusiana na asili mia 80 ya maamuzi ya kisiasa na kiuchumi ya majimbo.

Ni nyongeza tu natafuta website ya kutuma maoni yangu sijapata maana sipati access.

Pamoja na kufurahia na uwasiliaji wa maoni sielewi kwa nini maoni hayo yasiwe yanakuwa published kila wiki ili kupata mrejesho.
 
Ndio maana nikauliza kigezo kwetu ni nini, je ni miongoni mwa vile nilivyotaja? au ni kwa sababu wengine wanafanya hayo kwa mfano ufaransa? Katika muktadha wetu, kigezo cha miaka 18 ni kipi hasa.

Mchambuzi hivi HUELEWI kwasababu hutaki kuelewa au kwasababu akili zako ni ndogo (No pan intended).

I'll try again for the last time, kama hutaelewa basi sina jinsi ya kukusaidia.

Kigezo cha miaka 18 kiko katika HAKI ya mtu kuchagua viongozi na kuchaguliwa kuwa kiongozi ambayo HAKI hiyo imeainishwa katika katiba yetu (hata Katiba hii mbovu tuliyo nayo sasa. Kwamba Kila mtanzania anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi).

Sisi Watanzania tuliamua kwamba mtu akishafika miaka 18 basi mtu huyo ni mtu mzima na ana akili timamu, hivyo anaweza KUPIGA KURA i.e kuchagua kiongozi. Kama basi mtanzania wa miaka 18 tumempataia HAKI ya kuchagua viongozi, kwanini basi Mtanzania huyo huyo tumunyime haki yake ya kikatiba ya kuchaguliwa kuwa kiongozi?

Kama tunafikiri miaka 18 bado watanzania wengi wanakuwa hawajakomaa kiakili (read kuchagua viongozi) basi tusogeze mbele umri wa kupiga kura eg 22 years. Lakini pindu Mtanzania huyo tukimpatia HAKI ya kuchagua viongozi pia tumpatie haki yake ya kikatiba ya kuchguliwa kuwa kiongozi kwa mujibu wa katiba yetu. Sio tunampatia HAKI mkono kulia (read kuchagua viongozi). Lakini tunamnyang'anya HAKI hiyo hiyo mkono wa kushoto (read HAKI ya kutochaguliwa kuwa kiongozi).

Ndiyo maana wengine wakasema kigezo cha umri ni kimojawapo katika ya vigezo vingi including Elimu etc vinavyotumika kumpima mgombea urais. Ndiyo maana wakakwambia pamoja na nchi kama za Ufaransa na Canada katiba zao kutoa HAKI hiyo ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi, haijatokea hata siku moja wakampata RAIS/PM mwenye umri wa miaka 18. Mgombea Urais anapimwa kwa vigezo vingi sio umri tu. Point hapa ni kwamba tusiwanyime Watanzania wenye umri wa miaka 18 HAKI yao ya kikatiba ya kuchaguliwa kuwa viongozi, kama ambavyo tunavyowapatia wazee wa miaka 100 HAKI yao ya kikatiba ya kuchaguliwa kuwa viongozi, lakini pamoja na kutoa haki hiyo Tanzania hatujawahi kumpata mgombea URAIS wa miaka 100, achilia mbali RAIS mwenye miaka 100. Usiniambie hapa Tanzania hakuna wazee wenye umri wa miaka 100.

Kama mpaka hapo hajaelewa basi pole sana.
 
Hongera CDM na CUF kwa maoni mazuri kuhusu Muungano. Kama kati ya waliotoa maoni kuhusu Muungano yatakuwa kama ifuatavyo (kwa kusaidia kutoa uamuzi); Serikali tatu 20%: serikali mbili 55% Serikali moja 25%: Kutokana na alama hizi, pamoja ya kuwa wengi wamesema serikali mbili (55%) kwa maana ya muundo wa sasa; busara itumike kama alivyotumia Hayati Nyerere enzi za vyama vingi vya siasa, tukubali serikali tatu. Sababu aliyoiona Nyerere wakati huo wa vyama vingi iko valid kwa suala la muungano kwa hivi sasa.
 
Mchambuzi hivi HUELEWI kwasababu hutaki kuelewa au kwasababu akili zako ni ndogo (No pan intended).

I'll try again for the last time, kama hutaelewa basi sina jinsi ya kukusaidia.

Kigezo cha miaka 18 kiko katika HAKI ya mtu kuchagua viongozi na kuchaguliwa kuwa kiongozi ambayo HAKI hiyo imeainishwa katika katiba yetu (hata Katiba hii mbovu tuliyo nayo sasa. Kwamba Kila mtanzania anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi).

Sisi Watanzania tuliamua kwamba mtu akishafika miaka 18 basi mtu huyo ni mtu mzima na ana akili timamu, hivyo anaweza KUPIGA KURA i.e kuchagua kiongozi. Kama basi mtanzania wa miaka 18 tumempataia HAKI ya kuchagua viongozi, kwanini basi Mtanzania huyo huyo tumunyime haki yake ya kikatiba ya kuchaguliwa kuwa kiongozi?

Kama tunafikiri miaka 18 bado watanzania wengi wanakuwa hawajakomaa kiakili (read kuchagua viongozi) basi tusogeze mbele umri wa kupiga kura eg 22 years. Lakini pindu Mtanzania huyo tukimpatia HAKI ya kuchagua viongozi pia tumpatie haki yake ya kikatiba ya kuchguliwa kuwa kiongozi kwa mujibu wa katiba yetu. Sio tunampatia HAKI mkono kulia (read kuchagua viongozi). Lakini tunamnyang'anya HAKI hiyo hiyo mkono wa kushoto (read HAKI ya kutochaguliwa kuwa kiongozi).

Ndiyo maana wengine wakasema kigezo cha umri ni kimojawapo katika ya vigezo vingi including Elimu etc vinavyotumika kumpima mgombea urais. Ndiyo maana wakakwambia pamoja na nchi kama za Ufaransa na Canada katiba zao kutoa HAKI hiyo ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi, haijatokea hata siku moja wakampata RAIS/PM mwenye umri wa miaka 18. Mgombea Urais anapimwa kwa vigezo vingi sio umri tu. Point hapa ni kwamba tusiwanyime Watanzania wenye umri wa miaka 18 HAKI yao ya kikatiba ya kuchaguliwa kuwa viongozi, kama ambavyo tunavyowapatia wazee wa miaka 100 HAKI yao ya kikatiba ya kuchaguliwa kuwa viongozi, lakini pamoja na kutoa haki hiyo Tanzania hatujawahi kumpata mgombea URAIS wa miaka 100, achilia mbali RAIS mwenye miaka 100. Usiniambie hapa Tanzania hakuna wazee wenye umri wa miaka 100.

Kama mpaka hapo hajaelewa basi pole sana.

Pengine akili zangu ni ndogo, kwani bado sioni mantiki ya kuweka kigezo cha kugombea urais kiwe miaka 18 hasa iwapo suala zima linaangaliwa holistically kwa maana ya kwamba vigezo vingine vitakuwa pia ni uzoefu wa muda fulani katika masuala fulani na kiwango cha chini cha elimu fulani; Vinginevyo kama nia ni kuwafurahisha watanzania na kutumia hoja hii kama mtaji wa kisiasa huku ikijulikana wazi kabisa kwamba holistically, practicalities hazitampa nafasi mtanzania wa miaka 18 kuwa rais wa nchi, basi mtaji huo wa kisiasa kwa chadema kama inaufatuta, upo; Vinginevyo i choose to remain kuwa na akili ndogo katika hili kama ulivyo ainisha hapo juu na asante kwa pole yako kwani pengine ninai hitaji;
 
Nitaandika katika sentensi moja, kama utashindwa kuona hiyo MANTIKI basi huwezi ku pass hata course ya LLB 101.

Mantiki yake iko kwenye HAKI ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi.

The Oparating word here is HAKI. I rest my case.
 
Back
Top Bottom