Mkuu mimi siwezi nikakupinga mawazo yako lakini kwa muda huu tulionao na kama unafuatilia siasa za zanzibar na tanganyika nahisi kwa hayo maneno uliyoyasema hutanipinga iwapo nikwambia umezungumza mumbo jumbo or nonesense.labda nikukumbushe tu labda umesahau.jee umesikia mtanganyika kuelezea kero za muungano?kama wapo ni wachache lakini unapomwambia mtanganyika akuwekee angalau kero tatu,atakwambia zanzibar tunawapa umeme,tunawapelekea chakula,tunawaajiri etc.hizo ndo kero kuu za watanganyika.kama mtu anafikira na mawazo yajuu kabisa,atajiuliza hawa wazanzibar tunawapa huduma hizi kwanini,mwisho utagundua kupata huduma na nafasi ni haki yao kwasababu hakuna nchi tanganyika bali iliopo ni jmt na zanzibar imo ndani ya jmt.lakini ndugu zetu wazanzibar unapo muuliza kero za muungano kwa haraka haraka atakupa kumi na tano na nizamsingi kabisa.kwa hiyo mdogo wangu kuifanya nchi moja kwa wazanzibaq ni sawa na kuput all eggs into one basket so haiwezekani.na ukikomaa kutaka nchi ndo wazanzibar watakuja juu mara mbili zaidi na kupinga serikali moja.kwa mfumo wa serikali tatu nawapongeza chadema na cuf,hapo kila nchi itajitegemea.je wewe hupendi kila nchi ijitegemee?kama hupendi unataka serikali moja malumbano mengine yataibuka.wapo ambao watasema zanzibar wanatengwa kimaendelea kwasababu ni mkoa wa kusini,ama waislamu ni wengi,ama waarabu,ama uamsho,wazanzibar kwao na watanganyika kwao.
Mandi, kwanza nakushauri ukajifunze jinsi ya kuandika!
Kama mimi kupendekeza serikali moja, nchi moja, Rais mmoja ni nonsense, Je wewe ambaye kila uchaguzi unaipigia kura CCM ambayo sera (SIC) yake ni serikali mbili kuelekea SERIKALI MOJA, halafu baada ya kuichagua CCM unalalamika "ZNZ TUACHENI TUPUMUE" sijui tukuiteje?
Watanganyika tunazo KERO nyingi za Muungano lakini tofauti na nyinyi Wazanzibari hatulii lii kama Mademu! Mojawapo ya KERO za Muungano ni
1. Wazanzibari kuongoza wizara zisizo za Muungano
2. Watanganyika kutoruhusiwa kumilika ardhi ZNZ wakati ZNZ ni sehemu ya JMT
3. ZNZ kuchangia ZERO shilings katika kuendesha serikali ya muungano
4. Wabunge kutoka ZNZ kushiriki na kutoa maamuzi bungeni kwenye wizara ambazo sio za Muungano
5. Kuchoma makanisa yetu na kupiga risasi mapadri wetu huko Zanzibar
6. Wazanzibari kulipishwa bei/bill ndogo ya umeme wakati umeme unazalishwa Tanganyika.
8. Pamoja na kulipishwa bei ndogo ya umeme bado wazanzibari wanashindwa kulipa ankara zao hence Watanganyika tunabeba mzigo kwa kuwafutia madeni yenu ya umeme.
9. Kupeperusha bendera ya JMT kwenye meli za Iran ambayo imewekewe vikwazo na UN
10. ZNZ kuwa uchochoro wa kukwepa kulipa kodi, halafu baadae bidhaa hizo kuingizwa kimagendo Tanganyika.
11. Watangayika kwenda ZNZ kwa passport wakati wazanzibari wanakuja Tanganyika bila passport
12. Tume ya katiba mpya kuwa na wajumbe sawa kutoka Tanganyika na Zanzibar, wakati ka-Zanzibar ni sawa na mkoa kama Tanga. Ratio ya 43,000,000:1,300,00 Usawa uko wapi hapa?
13. Mbunge mmoja wa Zanzibar anachaguliwa na idadi ya watu ambayo ni sawa idadi inayomchagua diwani 1 wa Tanganyika. MBUNGE 1 ZNZ = DIWANI 1 TANGANYIKA. Halafu eti wabunge wa Tanganyika na Zanzibar wote ni sawa ndani ya bunge la JMT.
Kero ni nyingi wengine wataongezea