Sera ya Tanzania ya Mafuta ikoje/iweje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera ya Tanzania ya Mafuta ikoje/iweje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 1, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280
  Kuna uwezekano mkubwa muda si mrefu ujao tutatangaziwa rasmi upatikanaji wa mafuta ya kiasi cha kutosha tu kuweza kufanya biashara ya kimataifa. Labda kuanzia kwenye Ziwa Tanganyika na hadi maeneo ya ndani zaidi ya Tanzania na hata kwenye pwani yetu. Kwa vile tumeshajua matatizo mengi ambayo tumeyaona kwenye madini ni vizuri kujua sera yetu ya mafuta ikoje? Na kwa vile tumeshaona mambo ya Angola, Chad na hata Guinea linapokuja suala la mafuta je Tanzania tumejiandaa vipi kusimamia sekta hiyo nyeti sana?

  Je vyama vyetu vikubwa vya kisiasa vinazo sera za mafuta au wote tunasubiri mafuta yapatikane ndio tuanze mjadala wa sera?
   
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika mpaka jana Mume mwenye Mke anamimba yapata miezi tisa ,ajanunua japo beseni la kuogeshea na mafuta ya nazi,au pini ya kubania nepi ya mtoto mtalajiwa na leo usiku kampeleka mkewe labour [Hospital].

  Eeehh Mkuu kama ni vulugu mechi kiwanjani referee kalala ndani ya uwanja ni hii ya mafuta.Siunatujua kuwa maono [Vison] kwetu si jambo la msingi.Cha msingi tumejua tunayo mafuta basi tunaingia kwenye uchimbaji na maisha yanaendelea ila naona tutatumia kanuni ya mbugani au polini survival of the fittest.Kwani kuna umuhimu gani wa kuwa na sera [Policy] ya mafuta itatusaidia nini?

  Kama wiki mbili zilizopita mtafiti mmoja wa maswala ya nishati , kwa jina la Bwana Dennis Malingo [Mwanasheia Kitaaluma] alikuwa anafanya mahojiano kwenye moja ya kipindi cha Luninga asubuhi,mada ilikuwa UTAFUTAJI WA MAFUTA NA UCHIMBAJI WA GESi.

  Ila paliponifurahisha sana ni hapa ulipogusia SERA YA MAFUTA,Kwa watu waelevu [Intellectual] kitendo cha kuanza kuwa na udadisi kuwa uenda nchi yako ikawa na uwezekano wa kuwa na mafuta basi waelevu wanaofikilia kwa niaba ya Watanzania wanapaswa kuwa tayari na vifaa kwa maana ya sera ya kukabili ujio wa changamoto hiyo mpya ili kukabiliana nayo tayari wakiwa wakamilifu kila idala eneo hilo la mafuta na gasi.

  Mtafiti huyo Bwana Dennis Malingo, anasema ALISHANGAZWA katika moja ya KONGAMANO LA WADAU WA UTAFITI WA MAFUTA NA GASI KWA BAADHI YA NCHI ZA AFRIKA, LILILOFANYIKA KILIMANJARO KEMPINSKY pale mmoja wa maafisa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira aliyehudhuria mwaliko huo wa kombano alioupewa ALIPOULIZWA na wanakongamano kama kuna MPANGO WOWOTE KULINDA MAZINGIRA NA MAENDELEO YA MAFUTA NA GASI.Kusudio la Wanakongamano autoe ili watu waupitie kama Wanakongomano KICHEKESHO Muungwana huyo mwakilishi wa wananchi hakua na sera [Policy] hiyo mkononi na zaidi alibaki kujiumauama kuwa upo kaacha ofisini.Lakini hapo hapo Mwakilishi wa Taifa la Kenya alipoulizwa yeye wa kwake akasema anao na akautoa na kuutetea.

  Mtafiti huyo anasema alijisikia AIBU yaani kosa la Mwakilishi huyo,wote waliokuwepo hapo waliondoka na tafsiri kuwa HAKUNA KITU KAMA HICHO [SERA YA TAIFA] .Na mbaya kuwa kongamano ni swala ambalo unatumiwa taarifa muda mlefu juu ya ujio huo.Na kwa kuwa unakuwa unajua MADA ya kujadiliwa nini basi unafanya matayarisho.Iweje Mwakilishi wa Kenya aje na SERA YA TAIFA LAKE MKONONI lakini HUYU MWAKILISHI WA WATANZANIA ASIENDE NAO WAKE MKONONI.Picha ua vijana wa sasa wanasema movie ni kuwa HAKUNA SERA HIYO.

  Tupotupo hata kwenye mambo ya msingi.Du inauuuuma,natamani kama Serikali ipate kiongozi dikiteta mwenye maono ya kuwaondoa Watanzania kwenye umaskini na uvivu wa kufikilia na kutenda na kuwa na moyo wa uthubutu.Hakika Mwakilishi huyo angetafuta pa kupitia yeye na kitengo chake husika.Alifuata nini kama hana data.Aibu saaaana,Mtafiti yule anasema mwishoni mwa kongamano kwa kila siku walikuwa wanachukua posho ya dola hamsini. Naam Mwakilishi wetu huyu naona alifuata dola hamsini kama shilingi elfu themanini kwa kiwango cha dola kwa wakati ule.
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Unachokisema kina ukweli kabisa, mimi nadhani Vyama vya upinzani vianze kulifanyia kazi hilo swala, kwani Serikali ya CCM kwasasa sidhani kama wana huo mda, kwasasa wao wanafanya kazi kama zima Moto, Rais yupo busy na kukinusuru chama kisife Wizara husika yaani Nishati na madini kwasasa wapo Busy na kujisafisha na tatizo la Umeme na tuhuma za Rushwa wanazokabiliwa nazo. Au ungetusaidia kwa kutoa proposal ya sera ya mafuta kwasababu Serikali yetu ni Sikivu ita edit na kui-document
   
 4. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwaka jana wakati ndugu zetu wazanzibari walivyoshupalia hoj ya kulitoa suala la mafuta kwenye mambo ya muungano, mkuu wa kaya, akisubiriwa kwa hamu amalize utata huu, baada ya kila mtu kuwa ameongea lake......"akalimaliza" in his trade mark style...." kwanini tuanze kulumbana sasa hivi kuhusu mtoto ambaye hata hajazaliwa bado?" ...wanahabari wakaripoti hivyohivyo..."yakaisha".
  Nakupenda kwa moyo wote Tanzania.....
   
Loading...