Uchaguzi 2020 Sera ya kutopeleka maendeleo Majimbo ya Upinzani inahalalisha Sera ya Majimbo!

tathmini

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
318
250
Sera mojawapo ya CHADEMA ni majimbo. Maana yake halisi ni kuwa watu wenyewe kwenye maeneo yao, yawe mikoa au wilaya, ndio wawe wanachagua au kuwateua viongozi wao, kama wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri.

Pia maeneo hayo, pamoja na Bunge, viongezewe madaraka ya kuamua badala ya Rais pekee. Bahati mbaya au nzuri Rais wa sasa ndiye anathibitisha umuhimu wa maeneo hayo kuongezewa madaraka, kwa kuwa amekuwa anasisitiza kuwa hawezi kupeleka maendeleo kwenye maeneo walikochagua wawakilishi kutoka upinzani.

Tena kwenye kampeni anathibitisha kutekeleza ubaguzi huo kwa kubeza majimbo 'pinzani'. Mfano kwa hasira kabisa alirudia mara mbili kuwa Bunda (CHADEMA) wamenyimwa taa za umeme barabarani na lami wakati kijiji cha Lamadi, Busega (CCM) kimepewa.

Akasema yanayofanana na hayo kuhusu Kaliua (CHADEMA) na Urambo (CCM). Lakini maeneo walikoshinda wapinzani, si wote walichagua upinzani, na wananchi wote wanalipa kodi zinazotumika kupeleka maendeleo. Kwa hiyo ni uonevu kwa maeneo hayo kubaguliwa, na ni kwa sababu tu Rais ana mamlaka na maamuzi karibu yote ya maendeleo.

Kama mikoa, wilaya na halmashauri vingekuwa na maamuzi hata nusu tu, ubaguzi huu usingekuwapo. Hizi ndizo sababu zinazohalalisha sera ya majimbo ya CHADEMA.

Kadri Rais anavyoendeleza ubaguzi huu wa maendeleo, ndivyo kilio cha kubaguliwa kinavyoongezeka, na jinsi sera ya majimbo itakavyoanza kukubalika
 
Lissu akomelee hii kwa kutoa mifano ya mgombea wa CCM anavyopiga mkwara kwa wananchi kuwa kama watachagua wapinzani hawatapelekewa maendeleo
 
Back
Top Bottom