Pax,
..majimbo huwa na mamlaka fulani ktk mambo ya kodi, elimu,sheria etc etc.
..USA kuna majimbo yanayoruhusu hukumu ya kifo na kuna majimbo yanakataa hukumu hiyo.
..yalikuwepo majimbo USA ambayo yalikuwa yamehalalisha segregation na ndoa za weusi na weupe zilikuwa zimepigwa marufuku, ingawa federal government ilikuwa inaelekeza vingine.
..pia sasa hivi kuna majimbo yamekwenda mahakamani kupinga utaratibu wa Health Care aliopendekeza Obama.
..katika masuala ya kodi, USA yapo majimbo ambayo hayana sales tax na mengine yana sales tax.
..kwa mtizamo wangu bado demokrasia yetu haijakomaa kiasi cha kuweza kuhimili utawala wa majimbo.
..ninachoogopa mimi ni gharama kubwa zinazotokana na mfumo huo, pamoja na kutunishiana misuli kunakoweza kutokea baina ya majimbo, au baina ya majimbo vs serikali kuu.