CHADEMA haijajiandaa kuunda serikali
Baada ya serikali ya CCM kupoteza imani kwa wananchi Chadema kimeonekana kuwa kimbilio la mwisho kwa wanyonge na wasio wanyonge. Kwa sababu hiyo lazima CDM kitapata wanachama wapya wengi, lakini pamoja na hayo sioni kama CDM kimejiandaa au kinajiandaa kwa ujio huo.
Najua CCM kwa vile wana serikali ina vitengo vingi na uwezo mkubwa hata wa kuwaahidi wanachama wake u-DC nk kitu ambacho CDM hawana. Lakini tunajua CDM ina taasisi yenye muundo wa serikali (serikali ya majimbo), ina vitengo vyake na idara zake kuanzia wilayani, majimboni, mikoani, hadi taifa, kwa hiyo kwa vyovyote vile haiwezi kushidwa kuwa accomodate wageni hasa wanaokuja tayari na CV zao mkononi kama kina Millya.
Lakini cha kujiuliza, CDM kama taasisi, viongozi wa wilaya wako wapi, viongozi wa mikoa ni akina nani, je, sera ya majimbo inaongozwa kwa organs na structure zipi mbona hazijulikani? Chama kama taasisi hakiwezi kukamilika kama hivi vyombo viko dormant vikisubiri ujio wa mtu mmoja (Slaa) kufanya mkutano wa hadhara na kuondoka. Hivi leo nikienda Masasi kwa mfano nimuulize m/kiti wa tawi anaweza kumjua kiongozi wake wa jimbo ni nani? Kama hamjui je CDM wanatekelezaje kwa vitendo sera yao ya serikali za majimbo, au iko vitabuni tu?
What I'm trying to advocate here is that, CDM kipanue wigo wa utawala wake isijibane sana makao makuu, i-practice kwa vitendo sera yake ya majimbo wananchi waanze kuizoea. Hawa wanachama wapya wanaokuja waungane na viongozi wenyeji (of course baada ya kuwa-screened) wagawane hayo majimbo, wajitanabahishe huko kiasi kwamba tukisema jimbo la kanda ya Ziwa kwa mfano tujue nani atakuwa answerable kusimamia uhai wa chama kwa kuanzisha matawi, kuingiza wanachama, kuanzisha miradi n.k. Nafikiri huo ndio mfano mzuri kwa chama kinachojiandaa kushika dola.
Chama hakiongozwi kwa kutegemea head office (ikulu), head office inachotakiwa ni kutoa directives, highest decision-making na support lakini day-to-day activities zinafanywa na na organs zilizo chini yake, lakini kwa CDM the opposite is true, chama ni Mbowe, Slaa, Zitto basi, wanaonekana kana kwamba wao ndio wanaopokea directives na wao ndio wanafanya day-to-day activities.
Chama kinaonekana kama kimepwaya kipo makao makuu na kwa wananchi lakini hapa katikati hakuna kiungo kabisa, wanachama wanaelea elea tu hakuna wa kuwa handle kiasi kwamba siku yeyote wanaweza ku-deflect. Kama bado unapanda majukwaani kuomba watu wajiunge wakati hujajiandaa kuwa accomodate ni uzembe na upungufu wa strategies. Inauma sana chama kama kinapata nguvukazi na kushindwa kuitumia.
CDM wasiishie tu kumfanyia tafrija kubwa Millya na wengine watakaojiunga, wajiandande ni vipi wanatumia hizo nguvu mpya zinazoingia kuimarisha chama na kuandaa makada wake tayari kwa kuongoza serikali. Lakini kama chama kitaendelea kutegemea head office tutarudi kule kule kwa Pinda kutokuwa na uwezo wa maamuzi hadi amsubiri rais arudi toka ziarani.
Luteni.