Sera ya Chadema ya "Utawala wa Majimbo" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera ya Chadema ya "Utawala wa Majimbo"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kindafu, Apr 25, 2012.

 1. k

  kindafu JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Chadema ina uhakika mkubwa wa kushika Dola katika uchaguzi ujao kama utakuwa kweli huru na wa haki. Naunga mkono Sera yao ya „Utawala wa Majimbo", na ningependekeza kwamba waiweke hadharani tangu mapema ili iweze kufanyiwa „Pannel beating" kwenye „Vijiwe", „Media", „Mitandao" na „Forums" mbali mbali. Wakati mwafaka ukifika wataunda tu kamati maalum kuchambua maoni yatakayokuwa yametolewa na wadau na kutoa kitu kilicho bora - kinachokubalika na kinachowezekana! Ningetamani kwa sasa waainishe bayana yafuatayo:
  i. Ni jinsi gani wataigawa Tanzania ki-Majimbo i.e. Majimbo mangapi na mipaka yake ki-Jiografia.
  ii. Mfumo wa Utawala utakavyokuwa – ngazi ya Taifa na ngazi ya Jimbo.
  iii. Mfumo wa uchaguzi utakaotumika kuwapata viongozi ya Kitaifa na wa Majimbo.
  iv. Mipaka ya Utawala/Maamuzi – Kitaifa na katika Majimbo.
  v. Mfumo wa Utawala wa Fedha – Kitaifa na katika Majimbo.
  vi. Nk, nk, nk,….. – waweza kuongeza vipengele kadiri ya upeo wako!

  My Take:
  i. Hili litapunguza muda na gharama za „Uelimishaji Umma" wakati utakapofika.
  ii. Itawezesha wanachama wengi zaidi kuifahamu vema sera ya Chama chao na kuweza kuinadi katika ngazi na nafasi zao.
  iii. Itawezesha wanachama wanaotamani kuwania nafasi mbali mbali za Uongozi kuanza kujipanga mapema kwa nafasi za Kitaifa na katika Majimbo.
  iv. Nk, nk, nk……… Waweza kuongeza!
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Mtoa mada, naweza ipata wapi hiyo sera ili niisome kwanza niielewe ndio nije nitoe mchango.

  Hata kama ni nzuri kiasi gani lazima wananchi tuelimishwe, isije kuwa another sera maslah.

  Mikoa mimngine haina hata ulanga sijui itakuwaje.
   
 3. H

  Hute JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,047
  Likes Received: 3,920
  Trophy Points: 280
  hii ni safi sana, maendeleo yataspeed up zaidi kama kutakuwa na majimbo, accountability ya viongozi pia itakuwa kubwa zaidi kwasababu hao wakuu wa majimbo na wengine wengi watakuwa wanachaguliwa kwa kura.

  Sera za ccm za kuteuana ili mtu awe loyal kwa serikali ya sisiemu yanaleta umasikini na ufisadi tz...watu wanalindana ili waje wateuliwe tena, watu wanafagiliana hata kama kuna uchafu ili kusafisha njia asijetemwa term ijayo..
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,924
  Trophy Points: 280
  Kongosho

  Kuna ulazima wa kila mkoa kuwa na ulanga ili sera ya majimbo iweze kufanikiwa?
   
 5. m

  muislamsafi Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ya nimeipenda. Ila wailete mapema ili iwe chachu nyingine ya ushindi 2015
  watu wajipange kuwa watawala katika nafasi mbalimbali jimboni
  watu wafikirie kuhusu maendeleo ndani yamajimbo, majimbo yashindane kimaendeleo
  namwisho kuitoa nchi kwenyehili shimo la motoni
   
 6. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  waanzilishi wa sera hii sio chadema tu. Chifu Fundikira na chama chake wakati vuguvugu la upinzani linaanza walikuwa na hili hata wakashutumiwa kutaka kuigawa nchi vipande. Hii ni short sightedness. Naunga mkono sera ya majimbo - hii nchi kubwa sana na idadi ya watu si ajabu ikafikia milioni 80 hivi punde - maendeleo ya nchi na watu huenda yakadumaa na nchi ikawa haitawaliki toka dar au dodoma. Tujifunze kwa wamarekani jamani
   
 7. H

  Hute JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,047
  Likes Received: 3,920
  Trophy Points: 280
  kufanya ufisadi kwenye single controlled state kama tz kwa ujumla ni rahisi kuliko kufanya ufisadi kwenye majimbo......hata kama ukiangalia kwa mbali unaweza fikiri labda unataka kuigawa nchi vipande vipande, ukiangalia vizuri utakuwa hii sera ni bora sana na watz kwa sasa hatuwezi kugawanyika, labda kwa uzanzibari na ubara...lakini sio utanganyika hata kama tungemega vipi..
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Sio lazima sana, ila najaribu kuangalia rasilimali.
  Anyway, nitakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuchangia nikisoma na kuelewa huo mgawanyo wa majimbo utafanyaje kazi.

   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hii itasaidia kuondoa red tapes in the administration processes.
   
 10. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hapa sasa sana wasioipenda hii sera watakuja na 'nyimbo' zao zilizoshindwa za ukabila, ujimbo nk lakini kwa nchi kama tz, hii ni sera nzuri.

  Uzuri wake unatokana na ukweli kuwa nchi ya Tanzania ni kubwa na kuigawa katika managable areas itasaidia watu zaidi kushiriki katika maamuzi na msaada kutoka central government inaweza kuwa kwa mambo makubwa tu. Suala la majina tunaweza kutumia haya haya tuliyonayo na hata majimbo haya haya kuepusha confusions. Mfano, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Kusini, Kanda ya Mashariki nk.

  Chukulia, mkuu wa wilaya, mkoa, mkrugenzi pamoja na maofisa wengine wa maeneo wanachaguliwa na mtu mmoja aliyeko Magogoni na wanakuwa answerable kwake. Sehemu nyingine huyu anayewachagua hata hazijui na hajawahi kufika. Pia tukumbuke ukisema jimbo (mfano) Nyanda za Juu Kusini haina maana kuwa Wahaya, Wachaga, Wasukuma wote wahame warudi kwao kama wengine wanavyowaaminisha baadhi yetu.

  Pia hii itasaidia kuwa na 'realistic plans' badala ya hizi za sasa ambapo mtumishi wa ofisi ya umma anayehitaji kutumia Toyota Rav4 ya mil 45m kufanyia kazi analazimishwa kuwa na gari ya +250m.

  Lakini kikubwa kabisa ni ushahidi kuwa form ya utawala kwa sasa imeshindwa

   
 11. MAHENDEKA

  MAHENDEKA JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Jaribu kupekua threads zilizopita hoja hii ishajadiliwa kwa kirefu siku nyingi
   
 12. kinyoba

  kinyoba JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 1,238
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mi naona hii itapunguza sana wizi na ufisadi maana nionavyo Mimi hakuna eneo Tanzania ambalo halina raslimali za kuendeleza eneo husika!! Maendeleo yata speed up sana kwakua vinavyozalishwa vitabaki hapo hapo jimboni na kupunguza upotevu unaofanywa kwa mkusudi na viongozi wenye nia mbaya.
   
 13. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nchi wageni wanaingia bila mpangilio kama shamba la bibi. chukulia kagera kama ingekuwa full fledged jimbo thubutu ya hao wanaoingia na kuhonga wateule waishi kinyemela kama wangeweza fanya hivyo
   
 14. P

  Pax JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkuu hii sera ni bomba sana, nchi nyingi duniani zinaitumia. Jimbo linatoa kiongozi mmoja wa juu tumwite Senetor ambaye anakuwa amechaguliwa na wananchi wa jimbo husika, huyu zaidi ya kuwa ni kiongozi mkuu wa jimbo pia ni muwakilishi wa jimbo kwenye bunge la nchi, kama ilivyo sasa, sema jimbo linakuwa kubwa zaidi mfano unganisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuwa jimbo tuliite Serengeti. Hii ina maanisha kutakuwa hakuna wakuu wa mikoa wala wa wilaya, ila wakurungezi wa manispaa na madiwani ambao wote wanachaguliwa.

  Mapato: Majimbo yanatoa asilimia fulani ya pato lake central government ambayo ina jukumu sasa la kusawazisha kwa kuyapa fungu la hela zaidi majimbo yasiyo na uzalishaji mkubwa. Raisi anabaki kuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi na majukumu mengine yote. Kunakuwa na baraza la mawaziri lakini dogo sana. Mfano lazima kuwe na waziri wa ulinzi maana majimbo hayawezi kuwa na jeshi lake. Waziri mkuu ndio kama Hilary Clinton vile. Unaweza kuwa na mawaziri wengine lakini wanakuwa hawana kazi sana za kiutendaji maana majimbo yanajiendesha yenyewe na uchumi wa nchi katika mda mfupi unakuwa unapaa

  Chama chenye dola ndicho kinaamua sera kuu za nchi na policy za kufuata. Mfano serikali kuu ikisema afya ni bure na bunge likaridhia then kila jimbo halina budi kufuata. Kiufupi inaamuliwa sera zipi ziwe centralized na zipi majimbo yanaweza kujiamulia.

  Sera hii inaondoa bureaucracy sana inayotokana na viongozi wa kuteuliwa na mlolongo mkubwa wa mambo usio na tija. Formula zikishawekwa tayari kila jimbo linakuwa na ofisi kubwa na ndogo za TRA na hapa ufanisi unakuwa mkubwa sana maana ofisi hizi zinakuwa na mamlaka
   
 15. k

  kindafu JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu, ila naomba msaada wako kama kuna "Official Document". ya Chadema inayojibu japo baadhi ya maswali hapo juu utuwekee hapa Jamvini ili tuweze kutembea pamoja!
   
 16. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Hivi mnadhani hata Chadema ikichukua Dola 2015 itatawala milele? kama kila chama kitakuja na mfumo wake wa ugawaji wa Nchi tutafika kweli?

  Hiyo Sera ya majibu ni mzuri lakini ni lazima iwe ni sera inayokubalika na kwamba iingizwe kwenye katiba. kama kweli CDM wanaifagilia hiyo sera basi waifanyie kazi ili iingie kwenye katiba na kuwa mfumo rasmi ambao chama chochote kitachochukua dola hakitaweza kuubadili kirahisi tu. Unatakiwa uwe ni mfumo kama tunaotaka wa kuwa na idadi flani za wizara, mawaziri etc; rais anaechaguliwa anateua tu watendaji na si kupanga pangua ma wizara.

  Kama CDM wakichukua dola na kutaka kuuleta huo mfumo wa majimbo nakuhakikishia katiba yote itabidi iandikwe upya kabisa. Maeneo mengi sana yataathirika kuanzia serikali kuu hadi za mitaani, na kubwa kuliko zote Muungano.

  Haitokuwa rahisi kivile. Kwa wale mliowahi kufanya project za System changeover mtakubaliana na mimi, kwa mfumo huu wa uchaguzi kila baada ya miaka 5; muda utaisha system itakuwa haijakaa inavyotakikana, wasioitaka hiyo system watapata vya kuongea CDM 2020 itaangushwa atakaeingia nae atataka ku restore old system so it 'll be 10 years za vurugu za kimfumo.

  So kimsingi mfumo wa majimbo ni mzuri maana unasaidia sana katika kukuza maendeleo maana serikali kuu itakuwa inakusanya kutoka serikali za majimbo na jimbo lenye kuchangia zaidi ndilo litakuwa na nguvu zaidi kwenye kura za urais wa Serikali kuu. kiuwajibikaji kama serikali kuu itakuwa haiwajibiki then serikali za majimbo zitazuia fund zao mpaka wahusika wawajibike. Utawala wa majimbo kimsingi unapunguza sana nguvu ya serikali kuu na rais kwa ujumla.

  Mfano tulionao kwa hapa Tanzania ni Serikali ya zanzibar ndo ingekuwa serikali ya jimbo la Zanzibar, Huku bara napo tunakuwa na Serikali ya Jimbo la kaskazini, jimbo la Mashariki etc.

  Tatizo kuu la utawala wa majimbo:

  Kwa nchi zetu za kiafrika ni rahisi sana jimbo kujitenga. kwa sababu za kidini au kikabila. kwa hapa TZ kidini zaidi.
  Pia sababu za kiuchumi; jimbo likijiona linalea sana majimbo mengine kupitia serikali kuu basi laweza kujitenga na kuwa nchi huru.

  Kuna kila haja ya kuinyanyambua hiyo sera kwa undani wake kabla ya kuichukua. vinginevyo itatugharimu.
   
 17. M

  Miruko Senior Member

  #17
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  [TABLE="width: 582"]
  [TR]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 2, bgcolor: #FE0000"][/TD]
  [TD="width: 578, bgcolor: #B20000, colspan: 3"][/TD]
  [TD="width: 2, bgcolor: #FE0000"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF, colspan: 3"] [TABLE="width: 578"]
  [TR]
  [TD]
  MANENO “JIMBO” NA “MKOA”

  Maneno “Jimbo” na “Mkoa” kimsingi yana maana moja. Yote yana maana ya “eneo” katika mgawanyo wa nchi kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Serikali/utawala. Maneno haya yanatumika kwa kubadilishana (Interchangeably).

  Katika lugha ya kiingereza neno “Jimbo” lina tafsiri ya “Province” na neno “Mkoa” lina tafsiri ya “Region” lakini kiutawala yote yana maana ya aina moja ile ile ya eneo la kiutawala. Wakati Tanganyika (Tanzania Bara) inapata uhuru, neno “Jimbo” ndilo lilikuwa linatumika na Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika majimbo nane. Neno “Jimbo” lilibadilishwa baada ya uhuru na neno “Mkoa”. Huenda kubadilisha matumizi ya neno “Jimbo” kuwa “Mkoa” ulikuwa uamuzi wa kisiasa tu ili kuondoa fikra za “utawala” wa kikoloni. Kwa bahati mbaya kubadili neno “Jimbo” kuwa “Mkoa” hakukuenenda na mabadiliko ya misingi ya utawala wenyewe, yaani misingi ya mamlaka juu ya jamii chini ya mtu mmoja. Hiyo mtu anaweza kutumia “Tawala za Mikoa” au “Tawala za Majimbo” kwa maana moja ile ile.

  Mengi zaidi utayapata hapa (zipo kurasa 12). Sera ya Majimbo

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Sera ya Utawala wa Majimbo na Mchanganuo wa maana
   
 18. p

  popobaawa Member

  #18
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 19, 2007
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Utawala wa majimbo ndio nini?
   
 19. k

  kindafu JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu, na ndo maana nikaomba iwekwe hadharani mapema iweze kufanyiwa "Panel beating" ya kutosha wakati huu tunapojiandaa kutoa mawazo ya kutengeneza Katiba mpya!
   
 20. Jp Omuga

  Jp Omuga JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 2,671
  Likes Received: 822
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni nchi tajiri kwa rasilimali tulizozawadiwa na MUNGU....Watawala wameshindwa kutumia rasilimali hizi alijaribu Marehemu Nyerere tu kwenye historia yetu!

  Kwa nchi kubwa kama hii uwajibikaji unapokosekana laana zake ndo kama hizi hapa...

  Tunaambiwa kuna mgawanyo wa madaraka eti serikali kuu na serikali na serikali za mitaa lakini miongozo yote inatoka DAR es SALAAM kwa stahili ya REMOTE CONTROL.....hata uchimbaji wa madini kule NYAMONGO viongozi na wananchi wa maeneo husika hawana sauti kuhusu rasilimali zao....Mifano ni mingi sana!
  Wananchi Mtwara na Lindi wananufaika vipi na mradi wa kufua umeme wa gesi asilia kule???
  Wananchi wa Arusha kule Mererani wananufaika vipi na Tanzanite??

  Vidole havilingani ilhali vipo kwenye mwili mmoja....Nategemea kuwa maeneo ya nchi yetu pia yatatofautiana kwa wingi wa rasilimali...Lakini mbona hata maeneo yenye rasilimali nyingi nchini bado hali ni ngumu...

  Kwa nini viongozi tu na wafuasi wao ndo wanehemeke kupitia rasili mali za taifa huku wananchi walitunza rasilimali husika wakizidi kudhohofika na kutokomea kwenye umaskini wa kulazimishwa!!

  Eti uchumi wa dunia ndo unachangia wa kwetu nao udhohofu ni sawa lakini tunafanya nini kuhakikisha uchumi wetu unakuwa kupitia rasilimali zetu....Kwa nini wanyama tena hai watoroshewe nje ya nchi....je hii ni sera ya wizara husika...
  Pesa zinazopatikana zinawafikia wananchi kweli....

  Taratibu nyingine kichekesho kitupu...eti wanaoingia mikataba kwa niaba ya nchi yetu na wananchi (Mfano mradi wa Buzwagi) wanapewa 10%....hivi hawa si wanalipwa mishahara na posho....10% tena za nini kwao? Nchi yetu imefikia hapa kweli....Mtu anakaa ofisini DAR es SALAAM mkataba unasainiwa SHINYANGA anapewa 10% alafu wananchi wa eneo husika wanatimuliwa kama mbwa wezi!!! Kweli...........

  IPO HAJA YA KUBADILI MIFUMO YETU.....hivi hivi hatutafika huko tunapolenga tufike tukiwa kama taifa moja...Msije shangaa mkoa fulani ukijitangazia uhuru wake....REJEA YA MOMBASA KENYA, SUDAN KUSINI na KASKAZINI!!!
   
Loading...