Sensa ya watu na makazi

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
854
Bado tuna jamii ambazo zinaweza kukataa kuhesabiwa au kukwamisha zoezi la kuhesabiwa kwa sababu zozote zile?

Tafakari kutoka tamthiliya ya Ngoswe,Penzi kitovu cha uzembe (Edwin Semzaba)

Edwin Semzaba ktk tamthiliya yake alibainisha changamoto za uadidi wa watu ktk kijiji cha akina Ngengemkeni Mitomingi. Changamoto hizo ni k.v.

1.umbali wa makazi ya familia moja na nyingine. Ni changamoto mojawapo kwa wahesabuji kulifanya zoezi la uhesabuji kwa ufanisi.

2. ujinga,yaani wakazi kutojua umri wao na hawajui kusoma na kuandika.

3. Uhesabuji kuhusishwa na ushirikina, yaani wanaohesabu watu ni wachawi. Wanahesabu ili wapate wa kuwaroga.

4.ukosefu wa uadilifu kwa wahesabuji wenyewe(mapenzi kazini na ulevi) na hivyo kusababisha zoezi kuharibika kwa sbb karatasi za takwimu zinaungu(zw)a.
Ngoswe anamtongoza binti Mazoea, binti wa Balozi Mitomingi ambaye ni mwenyeji wake.

5.Ukosefu wa ushirikiano kati ya mhesabuji watu na viongozi wa mahali husika. Hawakutwi majumbani mwao licha ya kuwa na taarifa. Au hawaonyeshi ushirikiano ktk zoezi hili na hivyo kuwa kikwazo cha kufanikisha kazi.
nk nk.

Matokeo yake;

1. Huduma za jamii k.v. shule zinakosekana jirani na maeneo ya wakazi husika. Hivyo ujinga unazidi kutamalaki. Imani za kishirikina zinashika hatamu kwa kila tatizo.Watoto wa kijiji kile hawasomi kwa sbb shule ziko mbali.

2.Huduma za afya zinakosekana. Watu wanaendelea kuumwa na kufa kwa magonjwa yanayozuilika. Mme wa mama wawili wajane anafariki kwa kuwa hakupelekwa hospitalini kwa sbb huduma hiyo iko mbali na walipo. Aidha wakeze wanaamini kuwa alirogwa. Hata angepelekwa hospitalini asingepona. Matokeo yake anafariki na kuwaacha wakiwa na watoto wadogo,mwingine ni mchanga kabisa.

3. Barabara zinaendelea kuwa mbovu. Wakati Ngoswe anafika kijijini anashangaa kuuona udongo mwekundu kama udongo wa suriama.Hali ya barabara ni mbaya.

4. Huduma ya maji zinaendelea kuwa mbali au hazipo kabisa. Maji ya kijiji cha akina Ngengemkeni Mitomingi ni ya mto.Haya si safi na salama kwa matumizi ya binadamu lakini ndio yanatumiwa na wakazi wa kijiji hicho.
Mazoea,binti wa Ngengemkeni Mitomingi anakwenda mtoni kuteka maji. Ni mbali kidogo na nyumbani kwao. Na huko ndiko Ngoswe alimfuata na kuanza kumtongoza huku akimshikashika. Hapa tunapata mojawapo ya matokeo yawakutao mabinti na/au akina mama waendapo kuteka maji mbali na nyumbani.

Tumefanya nini ili kufanikisha zoezi la sensa?
1. Elimu kwa umma imetolewa juu ya umuhimu wa sensa. Na inaonekana tumeelewa na tuko tayari kuhesabiwa.

Maswali ya tafakari:

1.Je,tutakuwa tunahamasishwa kuhesabiwa kila sensa ikikaribia?
Naona kuna nguvu kubwa ya kuhamasisha watu kuhesabiwa. Najiuliza kuna nini nyuma ya hamasa hizi?

2.Je,haiwezekani serikali ikaja na mfumo mwingine mpya wa kupata takwimu za watu pamoja na taarifa zinazowahusu hao badala ya huu wa sasa?
-Hospitali kuwepo taarifa za watoto wanaozaliwa na kupelekwa kliniki pamoja na za wazazi wao.
- Shule ziwe na taarifa za watoto pamoja na za wazazi/walezi wao.
-Na maeneo mengine yanayokusanya watu wa makundi mbalimbali.
 
Swali moja la msingi:
Hivi kweli hawa watu wa Sensa, tutawatanbuaje siku ya sensa yenyewe? Watakuwa wanapita majumbani mwetu wakiwa wameambatana na wenyeviti wa Serikali za mitaa au? Maana mtu kitambulisho peke yake hakitoshi kumtambulisha kwa mtu wasiyefahamiana
 
Back
Top Bottom