SALAMU
Binafsi nashukuru kwamba sensa sasa inafanyika/imefanyika na kwamba
TAKWIMU za kuotea kwenye mipango ya serikali tunaweza kupata jibu pamoja na mambo mengine mengi.
Lakini kila nilitokuwa nikisoma HABARI kuhusu sensa niliona makarani kama picha inavyoonyesha nikajiuliza maswali mengi
Kulikuwa na UMUHIMU wote kwa hao makarani kuvaa REFLECTORS {karani ayelikwenda IKULU kavaa, kwa makamu wa raisi pia, source picha kwenye magatezi}
Kwa jinsi ninavyoelewa REFLECTORS utumika ili watu wakuone kirahisi hasa kwenye maeneo yenye magari na machine zinazotembea, zinaweza kutumika kwenye matukio mbalimbali kama mpira au mikusanyiko mikubwa kwa ajili ya kuonyesha watoa HUDUMA.
Lakini kwenye zoezi kama la SENSA karani anakwenda kwa wahusika kwenye makazi yao au kwenye biashara zao, zena akiwa wameongozana na wenyeji wa eneo husika (mjumbe na mwenyekiti wa kijiji), sasa hivi reflector wanavaa za nini?
ni nani huyo aliyefanya LOBBYING office za TAKWIMU ili aweza kutumbua pesa yetu kwa kupitia huu mradi wake wa reflector?
Tunafanya sensa ya mabilion kwa matumizi yasiyo na umuhimu kama haya.
Mwisho
I STAND TO BE CORRECTED
Nimejaribu kuweka PICHA za mazingira TOFAUTI ili kuonyesha picha halisi