Sensa: CCM itavuna mbegu ya udini iliyopandikiza katika Taifa, it's pay back time!

ujinga huu wa udini ulipoanzishwa na rais na washirika wake wengi tulijua kwamba madhara yake kwa baadae yatakua makubwa, ni jambo la ajabu kwamba chama kinachojiita tawala CCM baada ya kubanwa na Chadema kwa jinsi kilivyoshindwa kuongoza wakaona propaganda pekee ya kuwasaidia ni udini kule Mtwara mwenyekiti wa uwt SOPHIA SIMBA aliwambia watu kwamba Chadema ni chama cha wakristo sasa wanavuna walichopanda asante Mungu kwa kuwajibu hawa wanafiki kwa kile walichokitenda.
 
i disagree 100% with this talkings.lazima watanzania tubroad set mind yetu.hayo yote uliyotaja yana uhusiano gani na sensa?nchi iwe inaongozwa na CCM au Chadema sensa ni kitu cha lazima!hizi siasa ambazo hazina scope wala direction zisiharibu mambo mazuri ya kujenga mazingira mazuri ya kukua kwa nchi.Ni vigumu na sio vizuri kuingiza udini katika mambo ya sensa na hata ukabila.Lazima tuieleweshe jamii ya kiislam kuwa kazi ya kuhesabu idadi ya waumini ni kazi yao wenyewe msikitini kama ilivyo kwa wakristu pale makanisani.tusichanganye asilani na malengo na kazi za serikali.hatutengenezi wala hatuna mpango wa kuwa na serikali ya kidini hapa tanzania.
Inawezekana kabisa huelewi tunachokijadili hapa, soma upya thread ili upate tafsiri ya It's pay back time, inshort udini walioupandikiza CCM haujawai kuwa Threat kwao, sasa hii ni First Alarm kwao kwamba lile Zimwi walilolifuga sasa linahitaji damu na badly sharti la zimwi hili halitaki damu kutoka nje ya nyumba linataka damu ndani ya familia ili tambiko liwe sawa.

Tulipiga kelele tabia hizi za kuzidiwa hoja za kisiasa na kukimbili kwenye miamvuli ya kidini kwamba tunakokwenda siko watu hawakutuelewa, hii siyo sensa ya kwanza hapa Tanzania, kama una akili timamu ni lazima ujiulize why this?
 
Ivi kama serikari wangeweka icho kipengele cha dini kungekuwa na tatizo gani? Serikali imesema takwimu zitakazopatikana hazitatumika na serikali pekee bali zitatumika pia na taasisi mbalimbali,kwaiyo ata taasisi za dini zinaitaji izo takwimu kwa ajili ya mipango ya maendeleo.

Taasisi za dini zifanye sensa za waumini wake si juu ya seirkali.
 
Nchi yetu imeingizwa mkenge na hawa viongozi wa CCM. Unafiki, uongo na ghiliba ndani ya CCM imetufikisha pabaya. Chama hiki kimepoteza muda kushughulikia mambo ya kipuuzi badala ya mambo ya msingi sasa wanawaingiza hata watu ambao maisha yao yote wamejitahidi kuwa waadilifu. Chonde chonde ndugu zangu waislam makosa ya CCM siyo ya watanzania kwa ujumla wake. Tuungane kukitoa madarakani tuanze upya katika misingi ya haki. Aidha tukumbuke utawala wa CCM umejumuisha viongozi wa imani zote. Inasikitisha sana CCM imekuja kuwa adui mkubwa wa watanzania baada ya kuwapa ridhaa ya kutawala kwa zaidi ya miaka hamsini. Tushirikiane tuwang'oe watoke kwa aibu.
 
Sensa ni tatizo hapa nilipo kuna jirani zangu wamehamisha hata familia shauri ya sensa. Sijui wamekwenda wapi. Kila rafiki yangu wa kiislamu anasema wazi kuwa mimi sitahesabiwa kabisa. Lakini kwa suala kwa idadi ya watu ipo kwa mabalozi siyo kweli. Siku hizi daftari hilo linachakachuliwa tu. Mf. Mimi nimehamia hapa toka Julai 2011 lakini familia yangu haijaandikishwa, wapo wengi tu hapa hawaorodheshwa humo. Hizo daftari zilikuwa effective enzi za Mwalimu. Kila Mgeni alifahamika mtaani ndani ya saa 12.
 
Naunga mkono 100%. Si waislamu tu, habari nilizozipata toka Geita inaonekana watu wengi hawatahesabiwa, maana hata makarani wenyewe hawana vitambulisho, sare wala kitu chochote cha kuawatambulisha, wakati ofisi ya takwimu taifa inatangaza kuwa karani apewe ushirikiano mara atakapofika maana atakuwa na vazi rasmi na kitambulisho vitu ambavyo hawana na sidhani kama jamii itawaelewa. Mbaya zaidi wenyeviti wa mitaa wamegoma hawatawapa ushirikiano makarani hao kwa sababu mkuu wa wilaya (Bukombe) amewambia eti wao hawakupangiwa bajeti hivyo kazi yao ni ya kujitolea.
 
...Imetulia hii Mkuu...hata zile juhudi za Bakwata wapenda ubwabwa kupigia debe ushiriki wa sensa safari hii zimegonga ukuta....Sensa itaanguka chaliiii na hakuna wa kulaumiwa ila ni Serikali.
 
Ukitaka cha mtu sharti uliwe, Sasa ni zamu ya kuitafuna CCM. Mmeshatutumia vyakutosha tunadai nchi yetu na haki yetu kama Waislam. Tutaanza na la Sensa na tutayatimiza yote tunayotaka, rafiki wetu wakaribu tunae kama CCM.

1.Tunaanza na Sensa, ilikujua idadi yetu sisi Waislam na tukimaliza tunakuja na haya hapa
2. Kuirudisha mahakama ya Kadhi
3.Kujiunga na OIC
4. Kuitangaza Tanzania nchi ya Kiislam asiyetaka ahame, liwalo na liwe
5. Sharia Law
6. Wanawake kuvaa Hijabu, hutaki hama nchi
7. Kuwafukuza Wakiristu
8. Kurekebisha mfumo wa Elimu

Na mambo mengine yatafuatia taratibu, CCM tupeni Uhuru wetu, tumeshakusaidie sana na mmetutumia sana



unashangaza sana pale unaposhadadia dini ambazo zililetwa na wakoloni ili watutawale kirahisi, ningekuona wa maana endapo ungesema mtashugulikia swala la richmond epa meremeta nk ili fedha hiyo ikirudi ijenge shule, hospitali barabara ombaomba wapewe msaada watoto yatima wahifadhiwe n.k! Angalie usije kukuta Inakuwa jamhuri ya kikiristu!
 
Ukitaka cha mtu sharti uliwe, Sasa ni zamu ya kuitafuna CCM. Mmeshatutumia vyakutosha tunadai nchi yetu na haki yetu kama Waislam. Tutaanza na la Sensa na tutayatimiza yote tunayotaka, rafiki wetu wakaribu tunae kama CCM.

1.Tunaanza na Sensa, ilikujua idadi yetu sisi Waislam na tukimaliza tunakuja na haya hapa
2. Kuirudisha mahakama ya Kadhi
3.Kujiunga na OIC
4. Kuitangaza Tanzania nchi ya Kiislam asiyetaka ahame, liwalo na liwe
5. Sharia Law
6. Wanawake kuvaa Hijabu, hutaki hama nchi
7. Kuwafukuza Wakiristu
8. Kurekebisha mfumo wa Elimu

Na mambo mengine yatafuatia taratibu, CCM tupeni Uhuru wetu, tumeshakusaidie sana na mmetutumia sana



Ndoto za mchana hizo,tangu lini mtoto wa kambo akawa mtawala,waulizeni waarabu kwanini mikakati ya kuifuta israel hadi sasa imeshindwa,mkishapata majibu mjitathimini.
 
mimi nilianza kushangaa siku nyingi sana kwamba tunaingia msikitini tunapewa hotuba za kuilinda serikali dhidi ya wakristo na hata wakati mwingine tunaoneshwa kuwa rais wetu anapokosolewa anasakamwa sababu ni mwenzetu yaani mwislaam inatokea tunapewa hata tuition ya namna ya kupambana na wakristo lakini sasa wakristo hata hawana neno na sisi hata sasa kwenye sensa tumeona wakristo wameunga mkono sisi tumepinga maana tunaamini kila anachokubali mkiristo haramu
 

Mashekhe wetu wameshasema hakuna kuhesabiwa sisi waislamu, mpaka kipengele cha dini kiwepo, kama hakipo hatukubali kuhesabiwa. Hayo Madai unayoyakataa yapo kwenye agenda yetu sisi Waislam, hutaki hama nchi. Tunadai Mahakama yetu ya Kadhi pamoja na kujiunga na OIC na Sharia Law.

Mnadai kwa kafiri?
JITAMBUENI NDUGU ZETU KTK ADAM!
 
njiwa tayari jumuiya za Waislamu vipande vipande, CCM imeshawarubuni Masheikh na hivi ninavyotype post hii Sheikh Godi Godi na wenzake wamejitoa katika taasisi na jumuiya zilizokuwa zinapinga sensa wakiwemo wao wenyewe, na sasa hivi wako live wanahamasisha Umma wa Waislamu kushiriki sensa huku wakishusha na mistari mbalimbali ya koran.

I have said, serikali hii kamwe haiwezi kusikiliza madai ya waislamu kwa sababu viongozi wenu bei yao inajulikana, sasa kiko wapi ulichosema wewe waislamu ni wamoja? kati ya wewe na Sheikh Godi Godi nani anayetambuliwa kama mwanazuoni wa kiislamu anayetetea uislamu?

Njaa mbaya sana kamwe CCM na serikali yake haiwezi kulichezea kanisa, wewe kaa hapo endelea kuongea kama kasuku na huo ndio mtaji wao CCM utaishia kuishabikia CCM ila kikifika kipindi cha demand za Waislamu CCM inawanunuwa wale Masheikh wenye mdomo mchezo umekwisha, wajinga ndio waliwao.

kweli.mfumo kristo unafanya kazi
 
Last edited by a moderator:
Wakuu hapa JF

Kama ambavyo tayari kuna baadhi ya members wametoa taarifa hapa jamvini juu ya mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, umemalizika saa 12 jioni ambapo viongozi mbalimbali na wabunge kadhaa wa CHADEMA, wote wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa wamehutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Igunga na vitongoji vyake.

Kama ilivyo kawaida kwa Watanzania, mwitikio wa wana-Igunga pia kwa chama chao, kinachobeba matumaini yao na ya Watanzania wenzao ndani na nje ya nchi ulikuwa mkubwa, wakiendelea kudhihirisha utayari wao wa kushiriki na kumiliki mchakato wa mapambano haya ya awamu ya pili, ambapo kupitia M4C, Watanzania wanajiandaa kwa mabadiliko makubwa ya kimfumo na kikatiba.

Dkt. Slaa ametoa shukrani kwa wananchi wa Igunga kwa mshikamano mkubwa waliouonesha kwa chama chao CHADEMA na kwa mwanachama mwenzao, Joseph Kashindye (aliyekuwa mgombea ubunge Igunga), pia shukrani za dhati kwa mawakili, Profesa Abdallah Safari na Gasper, walioonesha na kudhihirisha hazina ya utaalam mbalimbali ambao chama hicho kinao.

Kisha akatoa salaam za pekee kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Kamanda Freeman Mbowe ambaye yuko nje ya nchi (Houston Marekani) kikazi, akisema yuko pamoja na wana Igunga katika harakati za kudai haki zao, salaam kutoka kwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Prof. Safari ambaye hakuwepo (akisema anawapenda sana watu wa Igunga) na salaam kutoka kwa wanachama wa tawi la Reading, Uingereza.

Baada ya shukrani na salaam hizo, Dkt. Slaa akarudia kauli yake ambayo ameitumia katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro katika mikutano ya Operesheni Sangara-M4C, kuwasisitiza wananchi, bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kushiriki katika zoezi la sensa litakalofanyika kuanzia usiku wa leo, Agosti 26, huku akirusha kombora kuwa mvurugano unaondelea juu ya suala hilo, ni matokeo ya 'sera' ya CCM na Rais Kikwete, kupandikiza udini, wakati kwa Watanzania hiyo haijawahi kuwa 'issue' kwao.

"Wananchi na Watanzania wenzetu wa Igunga napenda kutumia fursa hii kuwasihi Watanzania wote kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ambalo litafanyika usiku wa leo. Natoa mwito wa Watanzania wote bila kujali tofauti zao zozote zile, zikiwemo za dini, kushiriki shughuli hii muhimu. Ni muhimu tukajua idadi ya watu na makazi yao ili iwe rahisi kuweza kupanga mipango yetu.

"Itakuwa rahisi kuibana serikali hii inayoelekea siku zake za mwisho mwisho, kwa mfano kila eneo lenye idadi ya watu 5000 inatakiwa kuwa na zahanati, kila eneo lenye watu wanaofikia 25,000, linatakiwa kuwa na kituo cha afya, hivyo ni rahisi kuweza kuwabana na kuhoji kwa nini wananchi hawa hawana huduma muhimu za jamii.

"Lakini pia wananchi, sisi au watoto wetu wakikosa huduma muhimu kama elimu, maji au afya, haitaangalia dini, sote tutakosa bila kujali dini zetu, elimu yetu, wala huduma za afya hazitolewi kwa kufuata misingi ya dini, tukikosa tunakosa wote bila kujali wewe ni dini gani, bila kujali wewe ni shehe au wewe ni askofu, tukikosa tutakosa wote.

"Haya yanayotokea hivi sasa katika suala la sensa, masuala ya dini ni matokeo ya sera za CCM na akina Kikwete kupandikiza udini kwa Watanzania. Tunawaambia CCM na Kikwete kuwa suala la udini wamelilea sasa linawapata vizuri. Kikwete ameendekeza udini sasa yamempata mwenyewe, wakati sisi tunakemea udini, CCM walikuwa wanaupalilia kwa propaganda zao.

"Kuendekeza udini ni kukiuka misingi yenyewe ya dini maana hakuna dini yoyote, hata katika Quran inazuia mtu kumbagua mwenzake kwa sababu ya dini yake, nimesoma juu ya comparative religion, hakuna dini inakubali ubaguzi, kuendekeza ubaguzi wa kidini ni kukiuka misingi ya dini yenyewe, vitabu vitakatifu vinazuia. Haya ni matokeo ya CCM kumomonyoa misingi yetu ya utaifa, huko nyuma sisi hatukuzoea haya, Watanzania wote tuliitana ndugu, hakuna mtu aliuliza au kujali dini ya mwenzake," amesema Dkt. Slaa.

More...

 
Tumaini Makene
kama dk Slaa kweli mzalendo. atambie. ccm inatoa kiasi gani cha fedha kwa makanisa (MOU) na kwanini iwe siri kubwa na tufichwe watz ?
 
Last edited by a moderator:
mimi nachojua lilongwe ni mji asa mtu anapoamua kujiita jina la mji of all plenty things! hapo hamnazo.
 
dk Slaa ''amelipuka''..hili neno amelipuka huwa linanikerakweli sijui kama ni sahihi maana ccm ndio huwa wanalipuka bili kufkiri na kuongea utumbo
 
Back
Top Bottom